Je Watu wa kale walikuwa "Vilaza"?.

Je Watu wa kale walikuwa "Vilaza"?.

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,867
Reaction score
5,064
Ukisoma maandiko ya kale hata kupitia Vitabu vyetu vya kiimani ni kama utaona Dunia ya kitambo hicho ilikuwa nyuma sana ki teknolojia.Hawakuwa na mashine za kuwarahisishia kazi.

Na ukifuatilia gunduzi nyingi zilizopo leo zinaanzia hapo miaka ya 1700 hivi,na kadri tunavyoenda na ndivyo gunduzi haswa za kisayansi nazo zinaenda mbio kwelikweli.

Leo tunazungumzia mambo kama AI n.k. Muda si mrefu yatakuja mengine tena ya kustaajabisha na kushangaza.

Sasa ni vipi kwa Walioishi miaka ya nyuma ya hapo?Ni teknolojia ipi ya kustaajabisha tuliyoipokea kutoka kwao?.Nini hatima ya hii spidi ya teknolojia maana kila siku kuna jipya, na kasi ni kubwa sana.

Na hapa tusichanganye teknolojia na miujiza.Watu wa kale wengi wanajivunia miujiza zaidi.
 
Watu wakale walijenga mapiramidi kule Misri.

Na mpaka leo bado inashangaza ni namna gani waliweza kubeba yale matofali makubwa nakuyapangilia vile.
 
Hata ujazo wa ubongo wa mtu wa kale ulikuwa mdogo kuliko mtu wa sasa kwa mujibu wa tafiti, ila neneo linasema nyakati za mwisho maarifa yataongezeka, kutakuwa na vita baina ya nchi na nchi, watoto hawatawatii wazazi wao n.k. ndizo hizi nyakati tulizopo
 
Watakaokuja miaka 100 tu ijayo watatuona sisi kuwa tulikuwa vilaza maana wakati huo kila kitu kitakuwa automated, watakuwa na koloni la kudumu Mars, AI sijui itakuwa imefikia hatua gani na si ajabu teknolojia ya propulsion itakuwa imewezesha kuunda vyombo vya usafiri vya kasi zaidi...

Ni dunia ya kuachiana hii
 
Walijua constellation za nyota vizuri walijua uwepo wa sayari ambazo hazionekani kwa macho,
Angalia Tablets za kale zilizopatikana utajua kuwa hawakua vilaza

Angalia jinsi derinkuyu (underground city) iliyopo uturuki jinsi ilivyojengwa kwa ustadi
 
Ukisoma maandiko ya kale hata kupitia Vitabu vyetu vya kiimani ni kama utaona Dunia ya kitambo hicho ilikuwa nyuma sana ki teknolojia.Hawakuwa na mashine za kuwarahisishia kazi.

Na ukifuatilia gunduzi nyingi zilizopo leo zinaanzia hapo miaka ya 1700 hivi,na kadri tunavyoenda na ndivyo gunduzi haswa za kisayansi nazo zinaenda mbio kwelikweli.

Leo tunazungumzia mambo kama AI n.k. Muda si mrefu yatakuja mengine tena ya kustaajabisha na kushangaza.

Sasa ni vipi kwa Walioishi miaka ya nyuma ya hapo?Ni teknolojia ipi ya kustaajabisha tuliyoipokea kutoka kwao?.Nini hatima ya hii spidi ya teknolojia maana kila siku kuna jipya, na kasi ni kubwa sana.

Na hapa tusichanganye teknolojia na miujiza.Watu wa kale wengi wanajivunia miujiza zaidi.
Jana nilikuwa nafuatilia habari za anti/pro natalist movement. Kitu kimoja kilichopigiwa mstari ni idadi ya watu ilivyofumuka miaka ya karibuni.

Kwamba miaka 10,000 iliyopita idadi ya watu dunia nzima ilikuwa milioni 5 tu.

Mpaka mwaka 1800 idadi ndiyo ikafika watu bilioni 1, na kufikia 1900 ikafika watu bilioni 2. Sasa watu yupo bilioni 8.

Unavyozidi kuwa na watu wengi ndiyo unazidisha vichwa vya kutatua matatizo. Zaidi, tatuzi zinategemeana hivyo watu wa awali wakifanya kazi wanaofuatia wanakuwa na sehemu nzuri kuendelea.

Kwa hiyo wati wa sasa wana advantage mbiki, kwanza wamewekewa misingi. Leo mtu akitaka kufanya kazi na GPS kuna kina Einstein na Dr. Daniel Kleppner washafanya kazi kugundua General Relativity na kujiongeza kwenye accuracy ya atomic clock huko. Lakini poa leo kuna researchers wengi zaidi kwenye haya mambo ukilinganisha na mwaka 1905 alipokuwa anaandika Einstein.

Hii hapa breakdown ya major milestones kwenye population.

8,000 BCE 5 million

AD
1804: 1 billion
1927: 2 billion
1960: 3 billion
1974: 4 billion
1987: 5 billion
1999: 6 billion
2011: 7 billion
2022: 8 billion
 
Watu wakale walijenga mapiramidi kule Misri.

Na mpaka leo bado inashangaza ni namna gani waliweza kubeba yale matofali makubwa nakuyapangilia vile.
Sasa kama walijenga na haikuwezekana kuacha taarifa ni vipi walijenga ndio haswa msingi wa hoja yangu.Ni kwa nini wameshindwa kurithisha taarifa?mbona teknolojia nyingine za kale zinapatikana vitabuni?.

Watu wa nyuma ya hapo walikwamishwa na nini?.Usikute nayo yanaangukia kwenye miujiza kama ya kina Musa ya kupiga fimbo baharini na maji kugawanyika na Watu kupita?.
 
Watakaokuja miaka 100 tu ijayo watatuona sisi kuwa tulikuwa vilaza maana wakati huo kila kitu kitakuwa automated, watakuwa na koloni la kudumu Mars, AI sijui itakuwa imefikia hatua gani na si ajabu teknolojia ya propulsion itakuwa imewezesha kuunda vyombo vya usafiri vya kasi zaidi...

Ni dunia ya kuachiana hii
Miaka mia si kesho tu,vipi miaka 1000 kutoka sasa?Hata kwa hiyo miaka 100 tu iliyopita taarifa zake mbona zinapatikana na kinachofanyika sasa ni kuendeleza tu,kwa mfano Tv,Camera,Simu,Redio n.k,ila huko 1700 kurudi nyuma taarifa za gunduzi za kiteknolojia ni hafifu sana.Watazungumzia zana za kale za mawe n.k.

Hakuna balance kabisa kiteknolojia kuanzia miaka ya 1800 mpaka leo na ile ya nyuma yake kuanzia Damu na Hawa.Ingaws kuna hoja ya kimaandiko kama alivyo mention mdau coscated hapo juu
 
Maarifa kwa sasa yanaongezeka eksiponenshale. Huko nyuma tulikuwa tunajikongoja. Hii AI na maendeleo katika immunology, microbiology, quantum computing, DNA splicing na fission propulsion yanakwenda kubadili kila kitu - ndani ya miaka 50 - 100 tu ijayo!
 
Back
Top Bottom