Expedito Mduda
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 522
- 240
Hakuna asiyejua mtu aliyetuingiza kwenye mkenge wa ajabu wa jitu linaloitwa Richmond ambalo sasa linazaa jitu kubwa zaidi linanyonya damu yetu linaloitwa Dowans.
Hapo zamani tuliambiwa na PCCB kuwa mkataba na Richmond haukuwa na shida yoyote mpaka pale kamati ya Mwakyembe ilipotoa ukweli ulivyo. Sakata la Richmond limejadiliwa bungeni mwisho mmiliki wa kampuni hiyo hakupatikana maana hatukusikia jina lolote la nani anamiliki kampuni hiyo.
Kila kukicha tunaambiwa TANESCO inalipa mabilioni ya mapesa kwa makampuni yanayozalisha umeme hapa nchini kama vile IPTTL.
Leo hii tunaambiwa kuwa tunatakiwa kuwalipa Dowans Tsh. bilioni 185. Jamani, hivi sisi Watanzania tumekosa nini? Kwani hawa viongozi tunaochagua kutuwakilisha, wanawakilisha matumbo yao au wanataka sisi wenye nchi yetu tuseme nini!
Jana au juzi tunamsikia waziri mkuu akikataa gari lenye gharama kama ya Tsh. 280! Hee nyela! Kwa kweli tumekwisha. Kwani Pinda hakujua kama atapewa gari hilo mapema? Nilitegemea asema waziri mkuu amekaza ununuzi wa magari ya kifahari! Eti wameshanunua gari halafu ya wananchi imeshaliwa kikubwa kwake ni kukataa gari!
Serikali yetu unaundwa na watu gani jamani? Je, ni watu wa kawaida tu kama mimi kweli? Nahisi kama ni binadamu wa kawaida wangeshikwa na uchungu na hivyo kutanguliza maslahi ya nchi mbele. Wangeweza kuhakikisha huduma za jamii zinaboreshwa badala ya kujikita kwenye ununuzi wa magari ya kifahari kiasi hicho!
Kila kunapokucha tunasikia upotevu wa mabilioni ya fedha za walipa kodi na wavuja jasho wetu. Hivi ndugu zetu viongozi hamuoni hali hii inatutisha sisi wananchi wenu?
Mimi ninachoshangaa ni hiki hapa! Mmiliki wa Richmond hajulikani, na wakati huo huo mmiliki wa Dowans anajulikana na anatakiwa kulipwa hizo fedha, Je, Dowans hawezi kuulizwa amtaje Richmond maana Dowans ni mtoto wa Richmond?
Tunawaomba taasisi zote za kututetea muone na msimame kidete kuhoji mambo haya yanakwenda kwa mtindo upi maana wavuja jasho wa nchi hii sasa wamechoka kuonewa!