Je, wajua?

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
48,217
125,314
Kanuni ya dunia ipo hivi:

Kama hugusi Maisha ya watu ni ngumu sana kufurahia kuishi duniani. Ni ngumu sana kupata mafanikio ya kweli.

Maisha ni Raha kama una furaha, lakini ni Raha zaidi kama watu wanafurahia Maisha yako.

Kama Maisha yako hayagusi Maisha ya wengine. Kama Biashara yako haigusi Maisha ya wengine wewe ni jambazi Sawa Sawa na majambazi wengine.

Unawezaje kuishi duniani kwa Raha Wakati hakuna anayefurahia uhai wako?

Hakuna Baraka kubwa kama Maisha yako ni baraka kwa wengine.

Unajua kwanini watu wengi ni masikini?

Hii ni kwasababu wengi wanasubiri Maisha yao kuguswa na wengine. Wengi wanasubiri kubarikiwa. Hawajui kuwa baraka ya kweli ni pale Wewe unapokuwa baraka kwanza.

Tumeletwa duniani ili kuwa baraka kwa wengine.

Mto hauwezi kunywa Maji yake, mti wa matunda hauwezi kula matunda yake, jua halichomozi kwaajili yake, maua hayachanui na kupendeza kwaajili yake,

Kuishi kwaajili ya kuwa baraka kwa wengine ni kanuni ya dunia.

Hata kama una matatizo makubwa kupita milima, Usisahau kuwa baraka kwa wengine. Huwezi kujua, majibu ya matatizo yako yanaweza kupatikana kupitia wewe kugusa Maisha ya wengine.

Wengi waliofanikiwa sana Fahamu kuwa kuna huduma wanaitoa duniani. Wengi waliochini na masikini basi ujue wapo chini kusubiri wahudumiwe. Na wataendelea kubaki chini mpaka watakapotafuta kuwa baraka kwa wengine. Na kuhudumia wengi.
 
Life is really what you make it. Stop thinking too hard, take some time and give yourself a break. It's time to turn my year around and have in confidence in myself.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom