Je, Wajua Rais wa JMT Hayuko Juu ya Katiba? Anaweza Kulazimishwa Kumtengua Makonda, Akigoma, Bunge Linamtegua Urais?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,681
119,317
Wanabodi,

Baada ya mahojiano ya jana ya mtu kukwepa kuzungumzia suala la kufoji vyeti vya elimu, kuna watu wanaliona hili ni jambo dogo, hivyo kujitokeza kule, kumelimaliza rasmi, no its not over until it is over!.

Japo kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT ndio mamlaka kuu kupita zote, lakini sii wengi wanaotambua kuwa mamlaka ya juu kabisa ni katiba ya JMT, na rais wa JMT, japo amejiweka juu ya katiba, lakini kiukweli yuko chini ya katiba, hivyo hili suala la mteuliwa Daudi Bashite, watu wanalichukulia kimzaha mzaha au kiutani utani, lakini tungekuwa ni nchi nyingine yenye watu wanaojielewa, jee unajua suala kama hili lingeweza kabisa kumng'oa rais Magufuli pale Ikulu kwa mujibu wa sheria akaondoka na Bashite wake?.

Tanzania ni nchi inayoongozwa na Katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Ikithibika beyond reasonable doubt kuwa Daudi Albert Bashite ni kweli alifeli kisha akafoji vyeti na kufoji jina, kujiendeleza kielimu hadi kuteuliwa, then huyu ni muhalifu kama wahalifu wengine wote, then hata rais wa JMT ampende vipi, anaweza kulazimishwa kutengua uteuzi wake kwa kuamrishwa, na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, na rais asipofanya hivyo, then rais anaweza kushitakiwa na Bunge na kuondolewa madarakani!.

Watanzania tumekuwa ni watu wa kupiga sana kelele, kulaumu, kulalamika, kushutumu bila kuchukua hatua zozote ili hali sharia zipo lakini hatuzitumii.

Sakata la Bashite ni jambo dogo sana kulishughulikia kisheria.

Hatua za kufuata.
1. Any interested party mwenye ushahidi usio shaka kuwa Daudi Albert Bashite ni muhalifu wa kufoji vyeti na kuiba jina, kupitia kwa mwanasheria binafsi anaweza kufungwa mashitaka ya kijinai dhidi ya Daudi Albert Bashite as a private investigations. Atapewa vibali vyote toka ofisi ya DPP. Kuanzisha uchunguzi.

2. Uchunguzi utaanzia kwa Daudi Bashite mwenyewe kuitwa kwa samansi ya kuhojiwa kijinai chini ya kiapo. Na akikiri tuhuma, suala la uchunguzi wa kijinai unaishia hapa, mtuhumiwa anaandika barua ya kujiuzulu na issue hii inamalizika rasmi.

3.Kwenye mahojiano hayo kama atakanusha kuwa yeye si Daudi Bashite kama alivyodanganya jana pale Star TV, then kazi ya kukusanya ushahidi inaanza kwa kutolewa samansi ya kuwahoji wahusika wote wakuu isipokuwa mke, mzazi, walimu, hospitali kufuatia kitu kinachoitwa "fiduciary relationship" ambapo sheria inampa kinga ya kuhojiwa kijinai mtu wa karibu kama mke dhidi ya mume, mzazi na mtoto, mwalimu na mwanafunzi, daktari na mgonjwa, mwanasheria na mteja, padri na muumini etc. Hivyo kuanzia hospitali aliyozaliwa utakusanywa ushahidi wa documentary evidence aliandikishwa kwa majina gani?. Kisha Vizazi na Vifo kupata cheti cha kuzaliwa. Shule alipoandikishwa darasa la kwanza. Shule ya sekondari, Necta, vyuo, ajira alipitia, hadi idara ya uhamiaji alikopata passport alitumia majina gani na aliwasilisha vyeti gani na affidavits za wazazi gani, ambapo documents zote hizi ni legal documents za kiapo mtu akidanganya ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha jela, faini au vyote viwili.

4. Baada ya kukamilisha kukusanya ushahidi wa documentary evidence, usio tia shaka kuwa Daudi Bashite amefoji vyeti vya elimu kwa kutumia vyeti na jina la mtu mwingine aliyehitimu kihalali, then linafunguliwa shauri linaloitwa "quo warranto" kuwa rais amemteua muhalifu, hivyo mahakama inajiridhisha na ushahidi uliiowasilishwa mbele yake.

5. Ndipo mahakama inatoa hati ya Quo Warranto kumlazimisha rais wa JMT, atake asitake, kutengua uteuzi wa Daudi Bashite kwa makosa ya uhalifu wa kijinai. Kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hana mamlaka ya kumteua muhalifu kwenye utumishi wa umma. Kama anampenda sana anaruhusiwa kumchukua na kuishi naye Ikulu ikiwemo kula naye na kunywa nae chai, lakini sio kuhudumu kwenye utumishi wa umma.

6. Kama rais atetengua uteuzi huu, then DPP atakuwa huru kumpandisha kizimbani Daudi Bashite kujibu tuhuma za jinai zinazomkabili na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.

6. Iwapo Rais wa JMT asipotekeleza amri halali ya mahakama, anakuwa amepoteza sifa za urais zilizoainishwa na katiba ya JMT ya mwaka 1977. Hivyo rais anashitakiwa bungeni na kuondolewa kwenye urais kupitia process ya impeachment.

NB.
7. Process nilizoziweka hapo ni kwa mujibu wa katiba, sasa suala kama mahakama zetu zina weza kutoa amri ya Quo Warranto au laa linabaki kwenye utelelezaji, kitu cha muhimu ni kuelimishana kuwa rais wa JMT sio kila kitu, katiba ndio kila kitu. Maadam sheria zipo, suala la sheria kufuatwa au kutofuatwa hili sio langu.

8. The same applies to impeachment process, kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa rais wa JMT, anaweza kujifanyia lolote analotaka, no! . Urais wa JMT ni kwa mujibu wa katiba, rais wetu atatekeleza majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba, na ili kumkinga asibuguthiwe, ndio maana katiba yetu imempa kinga ya kutokushitakiwa mahakamani, lakini hakuna kinga ya kutokushitakiwa na Bunge pale anaposhindwa majukumu yake ya urais ikiwemo kututeulia wahalifu wa makosa ya jinai if proved beyond reasonable doubt, rais anashitakiwa na Bunge na anang'olewa na kuondoka na Bashite wake. Sasa suala la Bunge letu kama linauwezo wa kufanya hivi au laa, hili sio langu ni la wabunge wenyewe. Kitu cha muhimu hapa ni kujua kuwa hata rais anaweza kung'olewa madarakani na Bunge.

9. Hili sio lazima lifanywe na sheria, hata sisi media tunaweza, tukiwa na strong media yenye uzalendo usiatia shaka yenye kujua wajibu wake kwa umma, unaweza kuchunguza ukweli wa tuhuma hizi na kuziripoti, hivyo ama kumlazimisha rais wa JMT atimize wajibu wake, au kile kiti akione kichungu na kuachia kwa aibu kama ilivyowahi kutokea nchini Marekani kwa rais Richard Nikson kuachia ngazi kwenye kashfa ya Watergate.

10. Nawahakikishia hata mimi mwenyewe tuu kupitia kampuni yangu ya PPR, hili naliweza kabisa, ila kwa bahati mbaya sana, siwezi kulifanya kwa sababu kampuni yangu ya PPR, imejikita kwenye habari za kimaendeleo tuu zenye maslahi kwa taifa, yaani developmental news za Tanzania hapa tulipo, tufanyeje ili tufike kule tulikopaswa na sio habari kama hizi za vyeti vya Bashite.

Jumanne Njema.

Paskali
 
Just watching and listening!!

Hata hivyo, ninachofahamu ni kwamba, kwa watu wenye mawazo chanya bila kujali itikadi za chama; hili suala ni doa baya kuliko yote kwa JPM!!!

Ni ngumu kuamini kama kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kutetea uozo kama huu kwa sababu yoyote ile!!!

Mbaya zaidi, nae kama wale maju'ha wanaomtetea! Kila unapomminya kwenye hoja anakimbilia "...wauza dawa za kulevya!" Na bado kuna misukule wanamuamini kwamba ni kampeni za wauza dawa za kulevya!!!

Watu wanafahamu waliokuwa wamemshikia bango Bashite kuhusu vyeti ni Askofu Gwajima na Mange Kimambi!!!

Ukija kwa Gwajima, watawala wenyewe wamesema hahusiki na uuzaji wa mihadarati!!

Ukija kwa Mange; yeye ameanza kuwaripua wauza mihadarati hata kabla ya huyo Bashite!!!

Halafu mtu na akili zake anakuja hapa eti wanaomwandama Bashite ni wauza dawa za kulevya!!!

Hivi mtu kama Kinje na uswahiba wote ule na Le Mutuz anaweza kumwandama Bashite!!!

Hivi GSM ambao nao waliwahi kutuhumiwa kuhusika na mihadarati wanaweza kumuhujumu Bashite wakati ni kijana wao!!!!

Amini amini nawaambia... ni kheri ukose mali kuliko kukosa akili ya kuchambua na kujua ukweli upi na uongo ni upi!!

Ukikosa akili ya namna hiyo, unaweza kuishi hata na mume mwenzako nyumbani kwako kwa sababu tu mkeo alikuambia huyo ni mtoto wa ma'mdogo!!!!

Lakini niishie tu kusema kwamba, hayo uliyopendekeza ni ngumu kufanyika kwenye nchi ambayo kiongozi wake mkuu anataka yeye awe ndie alpha na omega!!!

Hata watu binafsi wakiamua kufanya hivyo, kesi itapigwa danadana mahakamani kwa sababu Mkulu hatakubali kamwe aumbuliwe!!!!

Hata Mkulu anafahamu wazi kwamba, endapo uchunguzi huo unafanyika sasa na kubainika yanayosemwa juu ya RC wa Dar ni kweli; aibu hiyo haitakuwa tena ya Bashite bali itakuwa aibu ya Mkulu ambae ameonesha wazi kutaka kumlinda kwa gharama yoyote ile!!!!

Itakuwa ni aibu ya Mkulu ambae nae bila aibu amefikia kusema wanaomsakama RC wanafanya hayo kwa sababu ya ajenda zao za siri!!!
 
Wanabodi,

Baada ya mahojiano ya jana ya mtu kukwepa kuzungumzia suala la kufoji vyeti vya elimu, kuna watu wanaliona hili ni jambo dogo, hivyo kujitokeza kule, kumelimaliza rasmi, no its not over until it is over!.

Japo kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT ndio mamlaka kuu kupita zote, lakini sii wengi wanaotambua kuwa mamlaka ya juu kabisa ni katiba ya JMT, na rais wa JMT, japo amejiweka juu ya katiba, lakini kiukweli yuko chini ya katiba, hivyo hili suala la mteuliwa Daudi Bashite, watu wanalichukulia kimzaha mzaha au kiutani utani, lakini tungekuwa ni nchi nyingine yenye watu wanaojielewa, jee unajua suala kama hili lingeweza kabisa kumng'oa rais Magufuli pale Ikulu kwa mujibu wa sheria akaondoka na Bashite wake?.

Tanzania ni nchi inayoongozwa na Katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Ikithibika beyond reasonable doubt kuwa Daudi Albert Bashite ni kweli alifeli kisha akafoji vyeti na kufoji jina, kujiendeleza kielimu hadi kuteuliwa, then huyu ni muhalifu kama wahalifu wengine wote, then hata rais wa JMT ampende vipi, anaweza kulazimishwa kutengua uteuzi wake kwa kuamrishwa, na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, na rais asipofanya hivyo, then rais anaweza kushitakiwa na Bunge na kuondolewa madarakani!.

Watanzania tumekuwa ni watu wa kupiga sana kelele, kulaumu, kulalamika, kushutumu bila kuchukua hatua zozote ili hali sharia zipo lakini hatuzitumii.

Sakata la Bashite ni jambo dogo sana kulishughulikia kisheria.

Hatua za kufuata.
1. Any interested party mwenye ushahidi usio shaka kuwa Daudi Albert Bashite ni muhalifu wa kufoji vyeti na kuiba jina, kupitia kwa mwanasheria binafsi anaweza kufungwa mashitaka ya kijinai dhidi ya Daudi Albert Bashite as a private investigations. Atapewa vibali vyote toka ofisi ya DPP. Kuanzisha uchunguzi.

2. Uchunguzi utaanzia kwa Daudi Bashite mwenyewe kuitwa kwa samansi ya kuhojiwa kijinai chini ya kiapo. Na akikiri tuhuma, suala la uchunguzi wa kijinai unaishia hapa, mtuhumiwa anaandika barua ya kujiuzulu na issue hii inamalizika rasmi.

3.Kwenye mahojiano hayo kama atakanusha kuwa yeye ni Daudi Bashite kama alivyodanganya jana pale Star TV, then kazi ya kukusanya ushahidi inaanza kwa kutolewa samansi ya kuwahoji wahusika wote wakuu isipokuwa mke, mzazi, walimu, hospitali kufuatia kitu kinachoitwa "fiduciary relationship" ambapo sheria inampa kinga ya kuhojiwa kijinai mtu wa karibu kama mke dhidi ya mume, mzazi na mtoto, mwalimu na mwanafunzi, daktari na mgonjwa, mwanasheria na mteja, padri na muumini etc. Hivyo kuanzia hospitali aliyozaliwa utakusanywa ushahidi wa documentary evidence aliandikishwa kwa majina gani?. Kisha Vizazi na Vifo kupata cheti cha kuzaliwa. Shule alipoandikishwa darasa la kwanza. Shule ya sekondari, vyuo, idara ya uhamiaji.

4. Baada ya kukamulisha kukusanya documentary evidence, usio tia shaka kuwa Daudi Bashite amefoji vyeti. Then linafunguliwa shauri lunaloitwa "quo warranto" kuwa rais amemteua muhalifu, hivyo mahakama inajiridhisha na ushahidi uliiowasilishwa mbele yake.

5. Ndipo mahakama inatoa hati ya Quo Warranto kumlazimisha rais wa JMT, atake asitake, kutengua uteuzi wa Daudi Bashite kwa makosa ya uhalifu wa kijinai. Kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hana mamlaka ya kumteua muhalifu kwenye utumishi wa umma.

6. Kama rais atetengua uteuzi huu, then DPP atakuwa huru kumpandisha kizimbani Daudi Bashite kujibu tuhuma za jinai zinazomkabili na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.

6. Iwapo Rais wa JMT asipotekeleza amri halali ya mahakama, anakuwa amepoteza sifa za urais zilizoainishwa na katiba ya JMT ya mwaka 1977. Hivyo rais anashitakiwa bungeni na kuondolewa kwenye urais kupitia process ya impeachment.

NB.
7. Process nilizoziweka hapo ni kwa mujibu wa katiba, sasa suala kama mahakama zetu zina weza kutoa amri ya Quo Warranto au laa linabaki kwenye utelelezaji, kitu cha muhimu ni kuelimishana kuwa rais wa JMT sio kila kitu, katiba ndio kila kitu. Maadam sheria zipo, suala la sheria kufuatwa au kutofuatwa hili sio langu.

8. The same applies to impeachment process, kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa rais wa JMT, anaweza kujifanyia lolote analotaka, no! . Urais wa JMT ni kwa mujibu wa katiba, rais wetu atatekeleza majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba, na ili kumkinga asibuguthiwe, ndio maana katiba yetu imempa kinga ya kutokushitakiwa mahakamani, lakini hakuna kinga ya kutokushitakiwa na Bunge pale anaposhindwa majukumu yake ya urais ikiwemo kututeulia wahalifu wa makosa ya jinai if proved beyond reasonable doubt, rais anashitakiwa na Bunge na anang'olewa na kuondoka na Bashite wake. Sasa suala la Bunge letu kama linauwezo wa kufanya hivi au laa, hili sio langu ni la wabunge wenyewe. Kitu cha muhimu hapa ni kujua kuwa hata rais anaweza kung'olewa madarakani na Bunge.

9. Hili sio lazima lifanywe na sheria, hata sisi media tunaweza, tukiwa na strong media yenye uzalendo usiatia shaka yenye kujua wajibu wake kwa umma, unaweza kuchunguza ukweli wa tuhuma hizi na kuziripoti, hivyo ama kumlazimisha rais wa JMT atimize wajibu wake, au kile kiti akione kichungu na kuachia kwa aibu kama ilivyowahi kutokea nchini Marekani kwa rais Richard Nikson kuachia ngazi kwenye kashfa ya Watergate.

10. Nawahakikishia hata mimi mwenyewe tuu kupitia kampuni yangu ya PPR, hili naliweza kabisa, ila kwa bahati mbaya sana, siwezi kulifanya kwa sababu kampuni yangu ya PPR, imejikita kwenye habari za kimaendeleo tuu zenye maslahi kwa taifa, yaani developmental news za Tanzania hapa tulipo, tufanyeje ili tufike kule tulikopaswa na sio habari kama hizi za vyeti vya Bashite.

Jumanne Njema.

Paskali
Hii movie ndio sasa inaanza,kuna mambo yanakuja,na tusubiri kwanza,lakini bado kuna masuala mengi ya kuyatizama na Ni mchezo wa hatari sana,sijui niseme vipi,kwamba ni Fisi au panya amenasa katika mtego,time will tell us.
 
Paskali hapa tatizo si Rc bali mfumo mzima wa kuwekana uongozini (vetting).Andiko lako kama ni kufanyiwa kazi ni lazima lisimamiwe na mawaziri muhimu watatu, yaani wa Mambo ya Ndani, wa Katiba na Sheria na yule wa utumishi aliyekwishasema cheti si lazima kwa viongozi.Sasa ukiwaangalia kwa jicho la tatu hawa mawaziri wana maslahi sawa na Rc ktk mambo haya ya utata wa vyeti, unategemea "wafanye nini?".Ukilipeleka hili jambo bungeni si ajabu ukamkuta ni Kibajaji "pekee" ambaye cheti chake hakina utata maana yeye anacho KIMOJA tu!
 
Quo Warranto - nimeipenda hii... Pascal, kuna wakati Mayor wa Dar na Lissu walikusudia ku file mashtaka ya Bashite Mahakamani! Sijui hata yameishia wapi...Lakini ulichokisema ni sahihi na ni dhahiri kamba Raisi wetu anatumia ubabe na jeuri ya dola ambayo ipo loyal kwake kuendelea kumkumbatia Bashite na hata kufika hatua ya kupindisha sheria na matakwa ya kisheria ya Katiba ya nchi.
 
Paschal yaani katika Master piece ulizowahi kuzileta humu JF, hii inaingia katika top 10, nakupa kongole za kufa mtu!. Atleast kupitia kalamu umechallenge dhana dhaifu kwamba Raisi ni Alfa na Omega katika nchi hii kitu ambacho siyo kweli hata kidogo.

Kinachonisikitisha ni kwamba Bashite anaiharibia hadhi taasisi ya Uraisi, Anaifanya taasisi ionekane kama ina double standards ktk kudili na tabia za wateule, maana kuna watu walitumbuliwa just kwa kugongo vyombo tu kwa raha zao, kuna waliotumbuliwa kwa kupeleka data za uongo juu ya watumishi hewa, Pia kwa watumishi wa umma wametumbuliwa kwa vyeti feki!. Sasa Bashite anatumia identity nyingine kinyume cha sheria, Elimu yake ni utata mtupu, Kavamia ofisi za watu na mitutu ya bunduki, Lakini hafanywi chochote, Je unadhani kwa hali hii umma unaichukuliaje taasisi ya uraisi ktk maamuzi yake?
 
Back
Top Bottom