celinawetu
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 1,331
- 1,059
Wanabodi,
Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM vetting kabla ya teuzi fulani fulani, hawajui kuwa vetting is nothing!, rais ana mamlaka ya kumteua yoyote regardless vetting imesema nini, na hauhusiwi kuhojiwa na yeyote!.
Hii ni kufuatia tabia ya baadhi ya wana jf kuhoji kila kitu, ama kwa kujua, ama kwa kutokujua, sasa sii wengi wanaojua kuhusu mamlaka ya rais ya uteuzi, anaweza kumteua mtu yoyote, mwenye elimu yoyote, hata ya darasa la saba, katika nafasi yoyote, bila kuwa sifa zozote, au kwa vigezo vyovyote, bila kuhojiwa na mamlaka yoyote, au mtu yoyote, popote!, who are you jf members kuhoji mamlaka ya rais ya uteuzi!.
Moja ya sifa kuu za jf ni kuelimishana, katika kuelimishana huku, tunajikuta tunasaidiana kwa kuongezeana maarifa kwa mambo watu wasioyajua.
Mamlaka ya rais ya uteuzi inaitwa presidential appointment powers ambapo katiba yetu yetu imempa mamlaka rais wetu kumteua mtu yoyote kwenye nafasi yoyote, bila kufuata ushauri wa yeyote, na bila kuhitajika kutoa sababu zozote kwa yeyote.
Ukiondoa teuzi ambazo rais anapaswa kuwateua watu wenye sifa fulani maalum, zilizoainishwa, mfano Jaji Mkuu lazima awe mwanasheria, Mwenyekiti wa NEC lazima awe Jaji Mstaafu, CDF lazima awe ni mwanajeshi, IGP lazima awe polisi, Director wa TISS lazima awe ni "wale jamaa", Msajili wa vyama ni Jaji, CAG mtu wa mahesabu, au wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma katika positions za utendaji, lazima wawe na sifa fulani za kielimu na kitaaluma, lakini katika positions za kisiasa, rais anaweza kumteua yoyote, kwa kumuokota popotena bado akawa yuko right. Hivyo hizi kelele za mkuu wa mkoa fulani kufoji cheti, kufoji jina au kutokusoma sekondari, hata ikikutikana ni yote yanayosemwa kuhusu elimu ya mkuu huyo ni ya kuunga unga, bado uteuzi wake unabaki kuwa ni halali, kwa sababu ana deliver, na sio majina wala sio macheti!.
Sifa za Kuteuliwa na Rais.
Sifa kuu pekee za mtu kuteuliwa na rais kuwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au mbunge wa kuteuliwa au nafasi nyingine yoyote ya uongozi na sio ya utendaji, wakiwemo wenyeviti wa bodi mbalimbali ni
1. Kuwa Mtanzania
2. Kutimiza umri wa miaka 18
3. Kujua kusoma na kuandika.
Hivyo rais ana mamlaka ya kumteua mtu yoyote mwenye sifa hizo, kwa kushauriana na mamlaka elekezi, kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa wilaya, au uteuzi mwingine wowote, hivyo rais yuko very right hata kuteua mtu wa darasa la saba, hivyo hata ikitokea, ikathibitishwa mteuliwa fulani aliishia darasa la saba, bado uteuzi wake ni halali.
Rais Halazimishwi Kupokea Ushauri Wowote kwa Yeyote. na ana Haki ya Kuupuuza Ushauri Wowote
Rais wetu, ana wasaidizi mbalimbali kuanzia Makamo wa rais, waziri mkuu, mawaziri, wataalamu mbalimbali wanaomshauri kwenye kila nyaja.
Katika powers za rais za uteuzi, katiba inampa mamlaka rais kabla ya kuteua baadhi ya watu, atashauriana na fulani, mfano uteuzi wa Waziri Mkuu, rais atashauriana na Makamo wa Rais. Wakurugenzi wa bodi, na wakuu wa taasisi za umma, rais atashauriana na mawaziri husika
Kazi ya washauri wote hawa ni kushauri tuu, na sio kumlazimisha rais kufuata ushauri. Hivyo katiba imempa rais mamlaka ya kupokea ushauri wowote, au kutopokea ushauri wowote ikiwepo mamlaka ya kupuuza ushauri wowote na rais akaamua vyovyote yeye mwenyewe na bado yuko right.
Zoezi la Uhakiki wa Vyeti Kwa Watumishi wa Umma.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, linawahusu waajiriwa wote wa utumishi wa umma, ambao ajira zao, ziliwahitaji kuwa sifa na vigezo vya elimu ya kiwango fulani,ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, lakini zoezi hili haliwahusu wateule wa rais kwa sababu mamlaka ya rais kufanya uteuzi wowote, haukuweka sifa wala vigezo vya rais kuteua, hivyo rais anaweza kuteua hata mtu asiyejua kusoma wala kuandika, na akamuwekea mtu wa kumsomea na kumuandikia, yeye kazi yake ikabaki kusaini kwa dole gumba na bado rais akawa yuko right.
Waliohitimu Vyuo Vikuu Kwa Majina ya Wengine.
Elimu ya Chuo Kikuu anayeipata ni mtu yule aliyehudhuria masomo, na jina la yule alihudhuria, na anayehesabika aliyehiti ni yule mtu na sio lile jina, jina niutambulisho tuu, mfano mimi Paskali, nilipokuwa mdogo niliitwa Kashinde, jina la utotoni, nikaandikishwa shule kwa jina la ubatizo Paskali. Nikajiunga chuo kikuu kwa jina la Kiti Moto, na nikahitimu kama Kiti Moto, mwenye hiyo elimu ni mimi in person, regardless natumia jina gani, au nilitumia jina gani, kilichohitimu ni mimi na sio jina, hivyo naweza kwenda kwa wakili yoyote nikatengeneza affidavit ya kubadili jina na kutumia jina lolote, hivyo jina doesn't matter, haijalishi kama nilisoma sekondari au sikusoma, lakini nikaingia chuo kikuu na kuhitimu, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa the end justifies the means.
Hivyo nawaomba watu humu jf, msihamanike sana na majina ya watu waliotumia, ama kama walisoma sekondari au laa, as long as waliohitimu chuo kikuu ni wahitimu halali wa chuo kikuu na kuteuliwa kushika wadhifa wowote ni halali.
Paskali.
Swala si ikiteuliwa Bali konda ashtakiwe kwa kigushi vyeti,hilo ndo kosa pekee LA huyu kinda wa UDART