Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Sisi hatukumteua kwa sababu ya vyeti vyake mkuu kama alifoji ndiyo unatuambia leo hata hivyo bado tunasisitiza kuwa issue ya vyeti hatuna muda nayo maadamu kazi zetu anafanya basi ni sawa na wale walioko jeshini na vyeti bandia umesikia wanaguswa jiulize kwa nini kisha pigia mstari kwa Paul Makonda
Once a criminal is a criminal hata akiwa rais, akifunguliwa kesi lazima aende kujibu hata kama ana perform wonders.
 
Yupo mnene mmoja, Ole, inadaiwa F.VI ana zero. Huyu hakuna anayehoji uhalali wa vyeti vyake kwa sbabu ni vyake beyond reasonable doubts. Ole, pamoja na 0 yake, vyeti vyake ni halali ila huyu mwingine vyeti vyake inadaiwa ni vya kufoji na forgery ni uhalifu; ni kosa la JINAI na kwa mujibu wa sheria mahali pake ni JELA.
Ni kweli kabisa Ole anatembea kifua mbele na hana wasiwasi wa CHETI amekubaliana na uwezo wa akili yake ila huyo aliyefoji anastahiki JELA. Nashangaa bado analindwa na vyombo vya Usalama wakati hivi sasa anatakiwa awe MUNG'ANDA!
 
Hapa jukwaani huenda mimi pekee ndo mwenye elimu ya darasa la saba.Huwa nashangaa inakuwaje wasomi mnashindwa kumuelewa Pasco na mimi wa darasa la saba namuelewa vizuri tu?
Sababu ya Elimu yako ndogo hata uwezo wako wa kupambanua jambo ni mdogo. Ungekua na Elimu kubwa ungeweza kupambanua kwa nini Pasco hayupo sahihi
 
Yaani Pasco kaamua kujitoa ufahamu labda kimakusudi au vinginevyo. I'll tunawajua wengi ambao elimu zao no za kusoma name kuandika wapo kwenye system y'all serikali aunt kwenye siasa, piano wako walio zungusha eidha form four aunt six weapon!! Tunacho zungumzia hapa no vyeti vya kuforge... Pasco hapo ndipo tupo sisi.....
Kama unatumia vyeti vya udanganyifu keep unastahili Kuwait kiongozi wa umma???
Mkuu hebu disable auto correction kwenye keypad setting ya simu yako...
 
Under Criminal procedure Act forgery is a criminal offence tatizo si kuwa unaelimu gani tatizo kutumia cheti cha mtu na kukufanya uchaguliwe kwenye nyadhifa fulani kwa mfano mimi niitwe Ally Juma lakini nitumie cheti cha Hemed Ally na niteuliwe nafasi ya ubunge kwa jina la Hemed Ally Achual natakiwa segerea au keko napasua kuni na shoka au upanga ambao haukati vizuri yaan butu na si kukimbizana na media
 
Mbowe hayupo serikalini usihamishe magoli, Watumishi wote wa serikali ni lazima vyeti vyao vihakikiwe ...
Kiongozi; nikurekebishe kidogo. Issue kubwa kwenye kadhia hii ya vyeti sio mtu yuko Serikalini au la. Awepo au asiwepo Serikalini ni lazima vyeti vyake viwe authentic as long as anadai ni vyake. Kosa la huyu jamaa inadaiwa ni FORGERY ambayo ni jinai hata kama asingekuwa Serikalini ilitakiwa sheria ichukue mkondo wake!

Yupo mwingine maarufu, Ole anayedaiwa kupata 0 (zero) F.VI lakini vyeti vyake havina mashaka; ni vyake. Huyu wala hakuna anyehoji uteuzi wake kwa sababu mamlaka ina uwezo huo. Angetudanganya alipata THREE wakati ana ZERO hapo wananchi wangekuwa na haki ya kuhoji hata kama angekuwa anachunga ng'ombe huko maporini.

CC: Pascal Mayalla
 
Cheti chake kinasaidia nini? Kwani hatuna jambo lingine la maana kuongelea katika mustakabali wa nchi yetu zaidi ya vyeti? Na tukienda kwenye kuchunguza vyeti sijui kama atabaki nani
 
Wanabodi,

Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM vetting kabla ya teuzi fulani fulani, hawajui kuwa vetting is nothing!, rais ana mamlaka ya kumteua yoyote regardless vetting imesema nini, na hauhusiwi kuhojiwa na yeyote!.

Hii ni kufuatia tabia ya baadhi ya wana jf kuhoji kila kitu, ama kwa kujua, ama kwa kutokujua, sasa sii wengi wanaojua kuhusu mamlaka ya rais ya uteuzi, anaweza kumteua mtu yoyote, mwenye elimu yoyote, hata ya darasa la saba, katika nafasi yoyote, bila kuwa sifa zozote, au kwa vigezo vyovyote, bila kuhojiwa na mamlaka yoyote, au mtu yoyote, popote!, who are you jf members kuhoji mamlaka ya rais ya uteuzi!.

Moja ya sifa kuu za jf ni kuelimishana, katika kuelimishana huku, tunajikuta tunasaidiana kwa kuongezeana maarifa kwa mambo watu wasioyajua.

Mamlaka ya rais ya uteuzi inaitwa presidential appointment powers ambapo katiba yetu yetu imempa mamlaka rais wetu kumteua mtu yoyote kwenye nafasi yoyote, bila kufuata ushauri wa yeyote, na bila kuhitajika kutoa sababu zozote kwa yeyote.

Ukiondoa teuzi ambazo rais anapaswa kuwateua watu wenye sifa fulani maalum, zilizoainishwa, mfano Jaji Mkuu lazima awe mwanasheria, Mwenyekiti wa NEC lazima awe Jaji Mstaafu, CDF lazima awe ni mwanajeshi, IGP lazima awe polisi, Director wa TISS lazima awe ni "wale jamaa", Msajili wa vyama ni Jaji, CAG mtu wa mahesabu, au wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma katika positions za utendaji, lazima wawe na sifa fulani za kielimu na kitaaluma, lakini katika positions za kisiasa, rais anaweza kumteua yoyote, kwa kumuokota popotena bado akawa yuko right. Hivyo hizi kelele za mkuu wa mkoa fulani kufoji cheti, kufoji jina au kutokusoma sekondari, hata ikikutikana ni yote yanayosemwa kuhusu elimu ya mkuu huyo ni ya kuunga unga, bado uteuzi wake unabaki kuwa ni halali, kwa sababu ana deliver, na sio majina wala sio macheti!.

Sifa za Kuteuliwa na Rais.
Sifa kuu pekee za mtu kuteuliwa na rais kuwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au mbunge wa kuteuliwa au nafasi nyingine yoyote ya uongozi na sio ya utendaji, wakiwemo wenyeviti wa bodi mbalimbali ni
1. Kuwa Mtanzania
2. Kutimiza umri wa miaka 18
3. Kujua kusoma na kuandika.

Hivyo rais ana mamlaka ya kumteua mtu yoyote mwenye sifa hizo, kwa kushauriana na mamlaka elekezi, kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa wilaya, au uteuzi mwingine wowote, hivyo rais yuko very right hata kuteua mtu wa darasa la saba, hivyo hata ikitokea, ikathibitishwa mteuliwa fulani aliishia darasa la saba, bado uteuzi wake ni halali.

Rais Halazimishwi Kupokea Ushauri Wowote kwa Yeyote. na ana Haki ya Kuupuuza Ushauri Wowote
Rais wetu, ana wasaidizi mbalimbali kuanzia Makamo wa rais, waziri mkuu, mawaziri, wataalamu mbalimbali wanaomshauri kwenye kila nyaja.

Katika powers za rais za uteuzi, katiba inampa mamlaka rais kabla ya kuteua baadhi ya watu, atashauriana na fulani, mfano uteuzi wa Waziri Mkuu, rais atashauriana na Makamo wa Rais. Wakurugenzi wa bodi, na wakuu wa taasisi za umma, rais atashauriana na mawaziri husika

Kazi ya washauri wote hawa ni kushauri tuu, na sio kumlazimisha rais kufuata ushauri. Hivyo katiba imempa rais mamlaka ya kupokea ushauri wowote, au kutopokea ushauri wowote ikiwepo mamlaka ya kupuuza ushauri wowote na rais akaamua vyovyote yeye mwenyewe na bado yuko right.

Zoezi la Uhakiki wa Vyeti Kwa Watumishi wa Umma.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, linawahusu waajiriwa wote wa utumishi wa umma, ambao ajira zao, ziliwahitaji kuwa sifa na vigezo vya elimu ya kiwango fulani,ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, lakini zoezi hili haliwahusu wateule wa rais kwa sababu mamlaka ya rais kufanya uteuzi wowote, haukuweka sifa wala vigezo vya rais kuteua, hivyo rais anaweza kuteua hata mtu asiyejua kusoma wala kuandika, na akamuwekea mtu wa kumsomea na kumuandikia, yeye kazi yake ikabaki kusaini kwa dole gumba na bado rais akawa yuko right.

Waliohitimu Vyuo Vikuu Kwa Majina ya Wengine.
Elimu ya Chuo Kikuu anayeipata ni mtu yule aliyehudhuria masomo, na jina la yule alihudhuria, na anayehesabika aliyehiti ni yule mtu na sio lile jina, jina niutambulisho tuu, mfano mimi Paskali, nilipokuwa mdogo niliitwa Kashinde, jina la utotoni, nikaandikishwa shule kwa jina la ubatizo Paskali. Nikajiunga chuo kikuu kwa jina la Kiti Moto, na nikahitimu kama Kiti Moto, mwenye hiyo elimu ni mimi in person, regardless natumia jina gani, au nilitumia jina gani, kilichohitimu ni mimi na sio jina, hivyo naweza kwenda kwa wakili yoyote nikatengeneza affidavit ya kubadili jina na kutumia jina lolote, hivyo jina doesn't matter, haijalishi kama nilisoma sekondari au sikusoma, lakini nikaingia chuo kikuu na kuhitimu, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa the end justifies the means.

Hivyo nawaomba watu humu jf, msihamanike sana na majina ya watu waliotumia, ama kama walisoma sekondari au laa, as long as waliohitimu chuo kikuu ni wahitimu halali wa chuo kikuu na kuteuliwa kushika wadhifa wowote ni halali.

Paskali.
ahahahahahha! kumbe raisi anayejipambanua kuwa amechukua muda na wakati mwingine hata hakulala usiku ilikupata watu wasomi na waadilifu aweze kuwaweka kama wakuu wa mikoa na wilaya,kumbe mojawapo ni huyu anayemiliki vyeti feki! tunataka kipimo kilichotumika kuwahakiki kada zingine zitumike pia kwa huyu Daudi a.ka makonda kwa sasa, na aache ulaghai na ufisadi
 
Cheti chake kinasaidia nini? Kwani hatuna jambo lingine la maana kuongelea katika mustakabali wa nchi yetu zaidi ya vyeti? Na tukienda kwenye kuchunguza vyeti sijui kama atabaki nani
Cheti chake kinasaidia nini? Kumiliki cheti kisichokuwa chako ni kosa tena la jinai na mahali pake ni jela. Hata ungekuwa mtendaji mzuri namna gani; forgery ni kosa.
 
Pascal mayalla Najua wewe ni mwanahabari na pia una uzoefu katika taaluma yako ya habari pia nafahamu kuwa umeingia darasani yaani wewe sio (kanjanja).

Naomba tuzungumzie dunia ya kileo dunia ya sayansi teknolojia, dunia ya maendeleo ya kielimu ,dunia yenye kuhitaji umakini stahiki na wenye mchanganyiko na elimu dunia.

Nafahamu unajua faida za mtu kuwa na taaluma yenye ufaulu na isiyo na kona nyingi , naomba wewe usimame useme tu kwa bandiko hapa JF kuhusu idadi ya waandishi wasio na elimu kwa sasa hivi jinsi walivyojazana mtaani je unahisi elimu isingekuwa na faida tungekuwa tunahaja gani ya kuwa na madaraja ya ufaulu?.

Elimu ingekuwa ni suala la kawaida kila aliyethubuthu kugusa daftari na kalamu basi leo angekuwa na anaitwa msomi ila kutokana na utofauti kwenye uelewa wa mtu basi kila mmoja anapata daraja la matokeo kulingana na jitihada zake kwenye usomaji.

Nakuja sasa kwenye mada, Katika taifa hili kuna makosa ya madai na jinai kosa la jinai linakuwa ni zito sana na linaloweza kumweka mtu kwenye uangalizi mkubwa sana ,mfano leo nikikamatwa na noti nilizozichapa (bandia) nitakamatwa kwa sababu ni jinai kuwa na noti ambazo sio halali ,na ingekuwa kuwa kuna mambo ya jinai yanaruhusiwa basi hata nadhani watu wangeruhusiwa kuwa na noti zisizo halali ili mradi wawe na pesa ( natumia lugha ngumu, ila naelekea kwenye suala hili ambalo sasa linaonekana kuwa mwiba kwake yeye).

Sidhani kama tunaweza kufumba macho kisa mfalme ameteuwa mwizi wa nafaka awe mlinzi wa ghala la kijiji, tunajua huyu ni mwizi ambaye amekuwa akiiba nafaka zetu bado tu tunasema mfalme hata akiteuwa mwizi ni sawa maana hakuna mtu wa kumuuliza ,ni sawa maana nchi nyeusi zimekuwa na utaratibu wa kunyenyekea sana wafalme ila kama zingekuwa zile nchi nyeupe zenye kuona furaha kusema ukweli hili lingekuwa ni suala la furaha kwao kusema ukweli na kila mmoja angesikia furaha sana.

Kwa vile mfalme ndie mwenye usemi wa mwisho nakubali hakuna mwenye kupanga aseme nani na afanye vipi ila katika hali ya kawaida inafika muda mwendo wa mfalme unatisha wale ambao wanamtumikia.

Kijiji chetu ni kidogo sana ila mambo ya jinai yanapaswa kukemewa ili haya mayai yatakayoanguliwa kesho yakute kuna nidhamu kubwa sana katika utunzaji wa nafaka sio mwizi wa nafaka ndiye apewe ulinzi wa nafaka.

Lazima tukubali kuwa Kufoji,kunakiri, kazi yeyote ile au kitu cha mtu ni kosa kisheria hapa sina neno lolote kuhusu teuzi ila kosa ni lipi "KUDANGANYA NA KUTUMIA KILE KISICHO CHAKO"
 
Kosa la Jinai!! Ana kesi ya kujibu.....vipi wengine maelfu waliotolewa kazini kw style ka yake?????
Pascal umejitahidi kumsafisha Daudi-hongera sana. May be I had been missing the point katika huu mjadala wa Bw. Daudi na kutumia cheti kisicho chake katika kujaribu kupata ajira na kujiendeleza. Nilivyoelewa mimi; watu hawalalamiki kwamba elimu yake ni ndogo (Std VII) kuwa Mkuu wa Mikoa. Mjadala umejikita katika uadilifu wake kama mtumishi wa umma.
 
Cheti chake kinasaidia nini? Kwani hatuna jambo lingine la maana kuongelea katika mustakabali wa nchi yetu zaidi ya vyeti? Na tukienda kwenye kuchunguza vyeti sijui kama atabaki nani
swala la cheti kina saidia nini ungemwuliza Ndalichako.hivi ndo vitu vya msingi vyakujadili,acha kujaribu kututoa nje ya reli
 
Zote mbwembwe sisi tunataka cheti chake cha form 4 nalasaba" hatuhoji mamlaka ya rais katika teuzi zake Bali makonda kutuhadaa

301b5c7a0ea61e5365148b40b1fabed0.jpg

Kama hauhoji uteuzi wa rais na unataka cheti chake, simple, mfuate kwake, lakini kama unataka cheti chake kama mkuu wa mkoa ni kupoteza muda kwani haina impact na uteuzi wake labda kumkosesha raha tu
 
Wanabodi,

Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM vetting kabla ya teuzi fulani fulani, hawajui kuwa vetting is nothing!, rais ana mamlaka ya kumteua yoyote regardless vetting imesema nini, na hauhusiwi kuhojiwa na yeyote!.

Hii ni kufuatia tabia ya baadhi ya wana jf kuhoji kila kitu, ama kwa kujua, ama kwa kutokujua, sasa sii wengi wanaojua kuhusu mamlaka ya rais ya uteuzi, anaweza kumteua mtu yoyote, mwenye elimu yoyote, hata ya darasa la saba, katika nafasi yoyote, bila kuwa sifa zozote, au kwa vigezo vyovyote, bila kuhojiwa na mamlaka yoyote, au mtu yoyote, popote!, who are you jf members kuhoji mamlaka ya rais ya uteuzi!.

Moja ya sifa kuu za jf ni kuelimishana, katika kuelimishana huku, tunajikuta tunasaidiana kwa kuongezeana maarifa kwa mambo watu wasioyajua.

Mamlaka ya rais ya uteuzi inaitwa presidential appointment powers ambapo katiba yetu yetu imempa mamlaka rais wetu kumteua mtu yoyote kwenye nafasi yoyote, bila kufuata ushauri wa yeyote, na bila kuhitajika kutoa sababu zozote kwa yeyote.

Ukiondoa teuzi ambazo rais anapaswa kuwateua watu wenye sifa fulani maalum, zilizoainishwa, mfano Jaji Mkuu lazima awe mwanasheria, Mwenyekiti wa NEC lazima awe Jaji Mstaafu, CDF lazima awe ni mwanajeshi, IGP lazima awe polisi, Director wa TISS lazima awe ni "wale jamaa", Msajili wa vyama ni Jaji, CAG mtu wa mahesabu, au wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma katika positions za utendaji, lazima wawe na sifa fulani za kielimu na kitaaluma, lakini katika positions za kisiasa, rais anaweza kumteua yoyote, kwa kumuokota popotena bado akawa yuko right. Hivyo hizi kelele za mkuu wa mkoa fulani kufoji cheti, kufoji jina au kutokusoma sekondari, hata ikikutikana ni yote yanayosemwa kuhusu elimu ya mkuu huyo ni ya kuunga unga, bado uteuzi wake unabaki kuwa ni halali, kwa sababu ana deliver, na sio majina wala sio macheti!.

Sifa za Kuteuliwa na Rais.
Sifa kuu pekee za mtu kuteuliwa na rais kuwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au mbunge wa kuteuliwa au nafasi nyingine yoyote ya uongozi na sio ya utendaji, wakiwemo wenyeviti wa bodi mbalimbali ni
1. Kuwa Mtanzania
2. Kutimiza umri wa miaka 18
3. Kujua kusoma na kuandika.

Hivyo rais ana mamlaka ya kumteua mtu yoyote mwenye sifa hizo, kwa kushauriana na mamlaka elekezi, kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa wilaya, au uteuzi mwingine wowote, hivyo rais yuko very right hata kuteua mtu wa darasa la saba, hivyo hata ikitokea, ikathibitishwa mteuliwa fulani aliishia darasa la saba, bado uteuzi wake ni halali.

Rais Halazimishwi Kupokea Ushauri Wowote kwa Yeyote. na ana Haki ya Kuupuuza Ushauri Wowote
Rais wetu, ana wasaidizi mbalimbali kuanzia Makamo wa rais, waziri mkuu, mawaziri, wataalamu mbalimbali wanaomshauri kwenye kila nyaja.

Katika powers za rais za uteuzi, katiba inampa mamlaka rais kabla ya kuteua baadhi ya watu, atashauriana na fulani, mfano uteuzi wa Waziri Mkuu, rais atashauriana na Makamo wa Rais. Wakurugenzi wa bodi, na wakuu wa taasisi za umma, rais atashauriana na mawaziri husika

Kazi ya washauri wote hawa ni kushauri tuu, na sio kumlazimisha rais kufuata ushauri. Hivyo katiba imempa rais mamlaka ya kupokea ushauri wowote, au kutopokea ushauri wowote ikiwepo mamlaka ya kupuuza ushauri wowote na rais akaamua vyovyote yeye mwenyewe na bado yuko right.

Zoezi la Uhakiki wa Vyeti Kwa Watumishi wa Umma.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, linawahusu waajiriwa wote wa utumishi wa umma, ambao ajira zao, ziliwahitaji kuwa sifa na vigezo vya elimu ya kiwango fulani,ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, lakini zoezi hili haliwahusu wateule wa rais kwa sababu mamlaka ya rais kufanya uteuzi wowote, haukuweka sifa wala vigezo vya rais kuteua, hivyo rais anaweza kuteua hata mtu asiyejua kusoma wala kuandika, na akamuwekea mtu wa kumsomea na kumuandikia, yeye kazi yake ikabaki kusaini kwa dole gumba na bado rais akawa yuko right.

Waliohitimu Vyuo Vikuu Kwa Majina ya Wengine.
Elimu ya Chuo Kikuu anayeipata ni mtu yule aliyehudhuria masomo, na jina la yule alihudhuria, na anayehesabika aliyehiti ni yule mtu na sio lile jina, jina niutambulisho tuu, mfano mimi Paskali, nilipokuwa mdogo niliitwa Kashinde, jina la utotoni, nikaandikishwa shule kwa jina la ubatizo Paskali. Nikajiunga chuo kikuu kwa jina la Kiti Moto, na nikahitimu kama Kiti Moto, mwenye hiyo elimu ni mimi in person, regardless natumia jina gani, au nilitumia jina gani, kilichohitimu ni mimi na sio jina, hivyo naweza kwenda kwa wakili yoyote nikatengeneza affidavit ya kubadili jina na kutumia jina lolote, hivyo jina doesn't matter, haijalishi kama nilisoma sekondari au sikusoma, lakini nikaingia chuo kikuu na kuhitimu, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa the end justifies the means.

Hivyo nawaomba watu humu jf, msihamanike sana na majina ya watu waliotumia, ama kama walisoma sekondari au laa, as long as waliohitimu chuo kikuu ni wahitimu halali wa chuo kikuu na kuteuliwa kushika wadhifa wowote ni halali.

Paskali.
Mimi sina shida na hili uliloandika hapa. shida yangu ni kwamba kama mtu ni wa elimu ya darasa la saba basi akubali kuwa ni darasa la saba na kama ni wa degree na awe wa degree. lakini hili la ulaghai na ujanja ujanja wa kutudanganya halikubaliki popote na ndio maana ni kosa la jinai la kifungo kama ikithibitika kwamba umefanya fojari. mbaya zaidi umeidanganya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na AMIRI JESHI MKUU
 
Once a criminal is a criminal hata akiwa rais, akifunguliwa kesi lazima aende kujibu hata kama ana perform wonders.
Ha ha ha! Hata kama aliiwezesha Tanzania kwa mara ya kwanza kurusha chombo anga za mbali jela inamhusu as long as alifoji vyeti. Sijui kwanini watu hawaelewi hili.
 
Back
Top Bottom