somo la hesabu limekua chukizo Kwa wanafunzi wengi dunia nzima, hali hii huwapa ugumu walimu WA somo hili kwakua wanafunzi hulichukia sana. Mwalimu Mmoja huko afrika ya kusini ameamua kutumia njia mbadala kuwafundisha wanafunzi wake somo hili. Mwalimu huyu ameamua kuandika formulae za hesabu kwa mfumo WA nyimbo za hiphop na nyimbo hizo huchukua sekunde 60 hivyo yeye huchukua nyimbo hizo na kuziweka kwenye laptop yake na pindi afikapo darasani huanza kuwaimbia wanafunzi wake. aliongeza kuwa hua anaruhusu kucheza pia ili kuongeza umakini darasani. Anasema Mwalimu Kurt kwamba juhudi zake zimeonesha matokeo chanya sana maana wanafunzi asilimia 100 Wanafaulu na wote hufika darasani tofauti na hapo awali
njia hii inaweza kutumika hata hapa kwetu Tanzania kutokana na wanafunzi wengi kuwa wapenz WA muziki na kushika sana mistari ya sanaa hii ambayo pia ni burudani kwao
He he hee hongera zake uyo mwalimu kwa kuwa na kipaji na kuwa tayari kukitumia kwenye kaz yake.Swali je wasio na vipaji hivyo wafanyeje? Na vipi kuhusu maadili ya taaluma husika?
He he hee hongera zake uyo mwalimu kwa kuwa na kipaji na kuwa tayari kukitumia kwenye kaz yake.Swali je wasio na vipaji hivyo wafanyeje? Na vipi kuhusu maadili ya taaluma husika?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.