Je, wajua kuna bata wa mayai na nyama pia?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Watanzania wengi kwa sababu ya kuigana yaani no kuumiza kichwa wote tuna fuga kuku wa mayai au Nyama.

Kuna Bata special wa Mayai hawa utagaji wao hakuna Kuku anaye fuata, kuna layers Ducks wanakiwa ni weupe wanataga mayai hadi 280 kwa mwaka.

Kuna Khaki Campbell hawa huwa ni wa kaki kaki kama jina lao hawa hutaga mayai hadi 300+ kwa mwaka na hivyo kiwafanya kuwa moja ya ndege wenye uwezo mkubwa sana wa kutaga.

Khaki Campbell Duck hakuna Kuku anaye wafikia kwa utagaji.

MATUMIZI YA MAYAI YA BATA
Mayai ya Bata ndo bora kwa kufanyia Backing Duniani, huko mbele kwa wanao fanya backing wanatumia mayai ya bata ambayo huwa na ute mwingi sana.

Mayai ya kuku hutumika kwa sababu hakuna mayai ya Bata ila kama kungekuwa na mayai ya bata basi hakuna mtu anaye back angetumia mayai ya kuku.

Pamoja na kwamba ni bora zaidi ya ya kuku kwenye kula ila bado kwenye Backing ndo ubora zaidi ulipo.

NYAMA
Bata wa nyama kuna Jumbo Pekin hawa ni wakubwa mno na majogoo wake hiwa ni balaa kwa ukubwa, hawa ni Brouler Bata na wana mature ndani ya wiki 6 tu.

Wazungu, Wachina wanapenda mno nyama ya Bata na huwa wanakula kuku kwa sababu tu hakuna nyama ya Bata ila ukiwawekea sokono nyama ya Bata na ya kuku basi wana opt ya Bata.

Sio lazima wote wafuge kuku, wengine fugeni Bata commercialy hasa bata wa mayai na wa nyama.

NB: Kwa sasa kuna Muingiliano wa watu wengi sana kife style zina badilika kwa kasi sana

images%20(42).jpeg
images%20(43).jpeg
images%20(44).jpeg
 
Moja kati ya ufugaji mzuri ikiwa mtu atapata mbegu ambazo hazijachakachuliwa kwa upande wa bata wa mayai, maana kama wakichakachuliwa kuna uwezekano wa kutokufikia hata nusu ya utagaji wao kwa mwaka.
 
Ni zipi changamoto nitarajie kukutana nazo iwapo nitaamua kufuga mabata wa nyama?
Kaka changamoto ni zakawaida kabisa sio kama za kuku, bata Bukuni wao wanahitaji kuwa na bwawa la maji na kusafishiwa maji kila mara pindi yakiwa machafu, Perkini hali kadhalika lazima wawe na bwawa la maji masafi kila mara, hizi aina 2 zote zinapendelea kula majani zaidi kuliko chakula kingine, bata wa kawadia hali kadhalika wanahitaji mlo kamili na maji ya kuoga na kunywa safi kila mara, kumbuka jamiizote hizo za bata hazina magonjwa mengi kama kuku. Usafi wa vyombo vya kulia na maji ya kuogelea na sehemu nzuri kwaajili ya ufugaji ni muhimu sana.
 
Unatakiwa upate BATA F1 kabisa
Moja kati ya ufugaji mzuri ikiwa mtu atapata mbegu ambazo hazijachakachuliwa kwa upande wa bata wa mayai, maana kama wakichakachuliwa kuna uwezekano wa kutokufikia hata nusu ya utagaji wao kwa mwaka.
 
Waliopo quality ni zero na walicha chakachuliwa sana, ukitaja Bata ni kuagiza nje kabisa unapata F1 asa hawafai kabisa
Zipo zinapatikana kwa wingi ni ww kujiandaa juu ya ufugaji wako maana uangalizi wa chakula mazingira ya bwawa la kuogelea ni muhimu sana kwao, ulaji wao ni kama wa bukini wanapenda majani na matunda mbali mbali kuliko pumba.
 
Wanauza kihubu na wengi wanauza ile inaitwa Farmer to Farmer yaani anaue uziwa na yeye anaenda kufuga na yeye aje auze,

Huwezi muuzia mtu bata wa kula sh 70,000.

Pia hakuna mwenye commercial duck Tanzania,
Shida ninayoiona wanauzwa bei saba Hao bata
Mmoja 70 000, labda u target ktk supermarkers
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom