Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Wanabodi, baada ya Rais Magufuli kutoa amri ya kuzuia kusafirishwa nje kwa mchanga wa makinikia ya dhahabu, kumezua mjadala mkubwa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kufuatia uamuzi huo kunapigwa kelele nyingi wanasiasa wakilia na kuingiza siasa kwenye kila kitu kwa hisia kuwa kuwa tunaibiwa. Wachumi wakizungumzia athari za kiuchumi na kwa upande wa kijamii watu kupunguzwa kazi.
Japo Beggars Can Not Be Choosers, Tuache Siasa Kwenye Uchumi. We Have to Choose Or. ..
Kwa kawaida kauli ya rais ni amri, ni sheria inahitaji utekelezaji tuu bila mjadala, hivyo
wengi kudhani katazo hilo la rais kupiga marufuku kusafirishwa kwa mchanga huo ni amri final and conclusive.Kauli ya Rais hutawala (final and conclusive)
Sio kila amri ya rais ni sheria na lazima itekelezwe, ili amri yoyote ya rais kuwa sheria, amri hiyo ni lazima iambatane na Presidential Decree na kutangazwa kwenye gazeti la serikali GN. Hii niliishawahi kuizungumza hapa
AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria
Hongera sana Spika Job Ndugai kulitumia Bunge kumsaidia rais. Naendelea kusisitiza rais wetu asaidiwe asiachiwe kila kitu yeye peke yake.Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .
Jumatatu Njema.
Paskali.
Wanabodi, baada ya Rais Magufuli kutoa amri ya kuzuia kusafirishwa nje kwa mchanga wa makinikia ya dhahabu, kumezua mjadala mkubwa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kufuatia uamuzi huo kunapigwa kelele nyingi wanasiasa wakilia na kuingiza siasa kwenye kila kitu kwa hisia kuwa kuwa tunaibiwa. Wachumi wakizungumzia athari za kiuchumi na kwa upande wa kijamii watu kupunguzwa kazi.
Japo Beggars Can Not Be Choosers, Tuache Siasa Kwenye Uchumi. We Have to Choose Or. ..
Kwa kawaida kauli ya rais ni amri, ni sheria inahitaji utekelezaji tuu bila mjadala, hivyo
wengi kudhani katazo hilo la rais kupiga marufuku kusafirishwa kwa mchanga huo ni amri final and conclusive.Kauli ya Rais hutawala (final and conclusive)
Sio kila amri ya rais ni sheria na lazima itekelezwe, ili amri yoyote ya rais kuwa sheria, amri hiyo ni lazima iambatane na Presidential Decree na kutangazwa kwenye gazeti la serikali GN. Hii niliishawahi kuizungumza hapa
AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria
Kitendo cha Spika Ndugai kutembelea bandarini, ni Kitendo cha kuitikia kwa haraka ule wito wangu wa juzi kuwa wasaidizi wa rais wamsaidie rais wetu. Ndugai ameamua kujitokeza Bunge kusaidia kuweka mambo sawa. Uamuzi huu hauna budi kuungwa mkono kwa dhati na waumini wote wapenda haki na waumini wa the doctrine of separation of powers and check and balance, wataunga mkono uamuzi huu.Amri hii ya kupiga marufuku kusafirishwa kwa mchanga wa makinikia ya dhahabu bado sio sheria hivyo sio final and conclusive. Amri hii inaweza kupingwa mahakamani na rais kulazimishwa kufuta kauli yake, au wavunje mikataba tukadaiane fidia. Tatizo kwa mahakama inayoongozwa na Kaimu Jaji Mkuu, bado sijui hili linawezekaje.
Tawala za nchi zinaundwa na mihimili mitatu rasmi ya dola na mihimili wa nne usio rasmi.
Mihimili hii mitatu rasmi ni Serikali, The Executive, Bunge, The Legislator na Mahakama, The Judiciary ambapo inatakiwa kuwa huru bila kuingiliana (independent) na wakati huo huo kila mhimili ukiwa ni mwangalizi na mdhibiti wa mihimili mingine isikiuke mamlaka yake katika kanuni inayoitwa The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balance.
Mihimili wa Serikali unaoongozwa na rais, kazi yake ni kutawala na kuendesha serikali na kutekeleza sheria zilizotungwa na Bunge na maamuzi ya mahakama na ni kazi yake kuzipa fedha Bunge na Mahakama lakini sii kuingilia utendaji wa Mihimili hii. Serikali ni watcher wa Bunge na Mahakama.
Mihimili wa Bunge unaongozwa na Spika kazi yake ni kutunga sheria zinazotafsiriwa na mahakama na kutekelezwa na serikali. Bunge ni watcher wa serikali na mahakama.
Mhimili wa Mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria zilizotungwa na Bunge na kutekelezwa na serikali. Hivyo ni watcher wa Bunge na Serikali. Naomba kukiri Mhimili wa Mahakama chini ya Kaimu Jaji Mkuu hauwezi kuicheck serikali, hivyo tumsisitizie rais wetu ateue Jaji Mkuu. Lengo la Katiba kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni kama Jaji Mkuu yupo ila yuko nje ya nchi au mgonjwa ndipo huteuliwa Kaimu, lakini nchi haina kabisa Jaji Mkuu aliisha staafu, unateua Kaimu Jaji Mkuu kama ishara ya kutumuamini au kutumuamini ile Tume ya Majaji, hivyo Kaimu Jaji Mkuu yuko on probation ,akikidhi ndipo athibitishwe, asipokidhi, atateuliwa mwingine. Kwa situation kama hii, hawezi kuutegemea mhimili wa mahakama kuicheck serikali.
Lengo la kila mhimili kuwa mlinzi wa muhimili mwingine ili kudhibiti hii mihimili usikiuke mamlaka yake. Hivyo serikali kulicheck Bunge na Mahakama, Mahakama kulicheck Bunge na Serikali, na Bunge kuicheck Serikali na Mahakama,
Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth!
Tangu serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani, mkuu wa mhimili mmoja wa serikali amekuwa ndie kiranja mkuu akifanya maamuzi mengi tuu ya kwa maslahi ya taifa japo baadhi ya maamuzi hayo ni maamuzi ya ajabu ajabu na mengine kufanywa kwa pupa na papara, huku yakikiuka hiyo separation of powers hivyo mhimili mmoja akiachiwa bila kuwa checked na mihimili mingine inaweza kulipeleka taifa letu kusiko haswa kwa kuzingatia mkuu wa mhimili huo kuamini mhimili wake umejichimbia chini zaidi hivyo kujidhania na kujiamini kuwa yeye ndio kila kitu!, kiukweli kila kitu ni Katiba na sio mtu.
Mfano wa maamuzi hayo
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!
Watanzania ni lazima tukubali matokeo: Tutake tusitake, utawala wa sheria lazima uheshimiwe
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?
Separation of Powers: Waziri Mkuu Majaliwa atofautiana na Rais Magufuli. Nani mkweli, Nani muongo?
Japo rais ndiye kila kitu na kauli yake ni ya mwisho ila sio final and conclusive, mamlaka yenye uwezo wa kutoa kauli final and conclusive ni Mahakama pekee.
Serikali inatakiwa kutenda haki wakati wote, ikitokea serikali kutoa amri zinazokiuka haki, inaweza kushitakiwa mahakamani na mahakama ikatoa amri za kimahakama ambazo ni final na conclusive zinazoitwa executives orders na kuiamuru serikali kutenda haki kwa lazima. Amri hizo ni Prohibition, Certiorari, Mandamus, Harbea Copos na Quo Warranto (maneno mengine ni Kilatini sijui Kingereza chake wala Kiswahili chake)
Hivyo amri ya rais kupinga kusafirishwa kwa mchanga wa dhahabu inaweza kupingwa mahakamani na mahakama ikatoa amri kuiamuru serikali kuruhusu mchanga huo kuendelea kusafirishwa kama kilichokuwa kinafanyika ni kitu sahihi kwa mujibu ya sheria na kwa mujibu wa mikataba yao.
Kama katazo la rais kuzuia kusafirishwa kwa mchanga huo ni kufuatia udanganyifu kuwa wanasafirisha mchanga wa dhahabu kumbe sio mchanga bali ni dhahabu, hivyo huo ni wizi kama wizi mwingine wowote, na wahusika wanapaswa kushitakiw na sheria kufuata mkondo wake.
Kama ni hivyo, sasa serikali ifanye ukaguzi mpya kupitia GST kupima kiwango chá madini kilichopo kulinganisha na kilichokuwa declared na serikali ndio iyasafirishe hayo makontena ya mchanga na kwenda kuyatindua na kupima dhahabu na madini mengine yatakayopatikana kisha kulinganisha na kile tulichokuwa tunalipwa, kisha kuwadai fidia na faini ya makontena yote zaidi ya milioni moja taifa tulio ibiwa tangu yaanze kusafirishwa kwa kutumia ile formular ya waiba maji au waiba umeme.
Kitendo cha Spika kuamua kuunda Kamati Teule ya Bunge, kufanya uchunguzi wa kinachoendelea kwenye issue ya madini, hii ndio mara ya kwanza sasa kwa Bunge hili kuicheck serikali.
Matokeo ya Kamati hiyo ya Bunge ndio yataonyesha kama hatua zilizochukuliwa na rais wa JMT kusimamisha usafirishaji wa mchanga wa dhahabu ni hatua sahihi. Ikikutikana rais alichemka, kamati hiyo itatoa maazimio ambayo serikali itatakiwa kuyatekeleza itake isitake. Hata kama rais alichemka, taarifa hiyo haitasema kuwa rais alichemka kwa heshima ya rais, bali itatoa maazimio tofauti na katazo la rais.
Kwenye kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba wa Richmond kwa jina maarufu la Kamati ya Mwakyembe, walikuta madudu kibao ya serikali, hiyo ili kuiokoa serikali, wakatafuta mbuzi wa kafara, ambapo kwa kuteswa kwake huyo mbuzi wa kafara, serikali ikaponywa.
Hongera sana Spika Job Ndugai kulitumia Bunge kumsaidia rais. Naendelea kusisitiza rais wetu asaidiwe asiachiwe kila kitu yeye peke yake.Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .
Jumatatu Njema.
Paskali.