Je, wachezaji wa Afrika kucheza mpira Ulaya ni aina ya Utumwa?

Dotori

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
544
23
Blatter condemns European clubs

Sepp Blatter has accused Europe's richest clubs of 'despicable' behaviour and engaging in 'social and economic rape' as they scour the developing world for talent.

His comments echoed those made before this month's World Cup preliminary round draw in Frankfurt when the 67-year-old Fifa boss railed against the many wrongs he sees in the world game.

"I find it unhealthy, if not despicable, for rich clubs to send scouts shopping in Africa, South America and Asia to 'buy' the most promising players there," Blatter wrote in a column in Britain's Financial Times newspaper on Wednesday.

"This leaves those who trained them in their early years with nothing but cash for their trouble."

"Dignity and integrity tend to fall by the wayside in what has become a glorified body market.

Blatter added: "Europe's leading clubs conduct themselves increasingly as neo-colonialists who don't give a damn about heritage and culture, but engage in social and economic rape by robbing the developing world of its best players.

"If we're not careful, football may degenerate into a game of greed - a trend I will vigorously oppose."

In the past, many African players promised untold riches by unscrupulous football agents have been greatly exploited by the very people who are supposed to be looking after them.

The phrase 'football slavery' was even coined to describe footballers who ended up living in poor conditions and on insufficient salaries many miles from their homeland.
SOURCE: BBC
 
Ndio, watumwa. Na wala si hao wacheazaji mpira wa ulaya tuu, hata sisi hapa, tupo watumishi wa serikali, watumishi wa ndani, watumishi wa mungu, watumishi wa... utajaza mwenyewe.

Kutuma au kutumwa si dhambi bali kudhalilisha mtumishi ndio dhambi, kiduniya na kidini.
 
Ndio, watumwa. Na wala si hao wacheazaji mpira wa ulaya tuu, hata sisi hapa, tupo watumishi wa serikali, watumishi wa ndani, watumishi wa mungu, watumishi wa... utajaza mwenyewe.

Kutuma au kutumwa si dhambi bali kudhalilisha mtumishi ndio dhambi, kiduniya na kidini.

Sepp Blatter, Rais wa FIFA anataka wachezaji wa Africa wabaki Afrika na kuendeleza mpira wakiwa Afrika.
Ukiangalia ligi za Ulaya, idadi ya wachezaji wa Afrika imeongezeka na pia ukitazama mashindano yanayofanyika hapa Afrika kiwango cha mchezo nacho kimepanda. Kwa mtazamo wangu kuna faida tatu kuu za wachezaji hawa kwenda ulaya:
1. Wanatangaza nchi
2. Wanaingiza kipato cha kigeni kwa nchi na kuwekeza nchini mwao
3. Kiwango cha mpira Afrika kinakua.
 
Kwa nini tunaongelea tu Wachezaji mpira? Hawa wanadhambi gani???

Madaktaji je, Mainginia je? Manesi je, Wanafunzi je? Waalimu Vyuo Vikuu je?? N.k

And may be hata mimi na wewe.. wengi tumeweza hata kuchangia hapa JF kwa kuwa tuko ungenini? Kwa nini nasi tusirudi nyumbani kuimarisha uchumi unaokuwa kama ilivyo ktk soka?
 
Kwa nini tunaongelea tu Wachezaji mpira? Hawa wanadhambi gani???

Madaktaji je, Mainginia je? Manesi je, Wanafunzi je? Waalimu Vyuo Vikuu je?? N.k

And may be hata mimi na wewe.. wengi tumeweza hata kuchangia hapa JF kwa kuwa tuko ungenini? Kwa nini nasi tusirudi nyumbani kuimarisha uchumi unaokuwa kama ilivyo ktk soka?

There you are.
ukute aliyeanzisha mada hii naye yuko huko huko "Utumwani" ama kama wao wanavyokuita "Ukimbizini" Mie nilisharudi, naendeleza Afrika tu.
 
There you are.
ukute aliyeanzisha mada hii naye yuko huko huko "Utumwani" ama kama wao wanavyokuita "Ukimbizini" Mie nilisharudi, naendeleza Afrika tu.

Wachezaji hawa walio nje nao wameonyesha moyo wa kuzipenda nchi zao. Wameamua kurudi Afrika na kuwakilisha nchi zao na kuacha ligi za Ulaya zikiendelea. Kiwango cha mpira nacho kinaonekana kupanda.

Vile vile watanzania professionals waliopo nchini na wale waliopo ughaibuni nao wanaleta mtazamo mbadala katika kuchanganua/ kushughulikia masuala mbali mbali yanayohusu nchi yetu.
 
3. Kiwango cha mpira Afrika kinakua.
Kuna madai kuwa Wachezaji hao wakiwa Afrika hucheza chini ya viwango vyao vya Ulaya. Hii ni kauli tosha kusema kuwa Wachezaji hao hawaongezi chochote katika upandaji wa Kiwango cha soka Afrika
Former Nigeria striker Daniel Amokachi says some European-based African players do not match their club form whilst playing for their countries.

Zaidi unaweza kucheki hapa
 
So far wachezaji wanaocheza Ulaya wameweza kung'ara kwenye mashindano haya. Imekuwa burudani kuyafuatilia.
 
Nafikiri "so long as", kila mtu yuko chini ya tawala ya aina yoyote ile iwe ya kijima, kibeberu au kibepari basi wao,mimi na wewe wote ni watumwa.

Wote ni watumwa kwa sababu tunatimiza matakwa ya kupatikana faida kwa walio na biashara zao katika mifumo yote niliotaja hapo juu.

Nikianza na ujima mpaka leo pale katika msitu wa Borneo na Amazon bado yale makabila yanayoishi katika zama za ujima, wanatumikishwa kukata magogo ambayo yanafika ulaya yakiwa ni samani ya aina mbalimbali tena vikiuzwa kwa bei ya juu.

Tukiingia katika ubeberu, wachezaji wa Afrika wanaanzia mchangani wakicheza na kibaraka wa mabeberu anatafuta wachezaji wenye vipaji kama walivotafutwa Emanuel Ebue na wengine.

Baada ya hatua hii inafuata hatua ya kupelekwa Belgium au France ambako wanachezea timu za madaraja ya chini huku yule aliwachukua Afrika akipata ujira wake na kuwagawia hawa wachezaji kiasi kidogo cha kujikimu na maisha ya Ulaya.

Endapo mchezaji wa Kiafrika anaonekana na timu kubwa ambayo inafuata mfumo wa kipebari kama wa Uingereza iwe Man United au Arsenal, basi wachezaji kama Ebue wana nafasi kubwa ya kutumikishwa kucheza mpaka atakapochoka na akitaka anaweza kuanzisha shule ya michezo kama yule Abedi Pele wa Ghana na wengine au kuishi maisha ya anasa na kusahau alikotoka.

Katika mfumo wa kibepari wenyewe ndio kuna songombingo la uhakika ambapo kuna vibarua wa kulipwa kwa walichofanya iwe Mc-Donalds, au kwingine kama kwenye maboksi na hata kusafisha hospitali na mahoteli.

Lakini wanaofaidi ni CEOs wote ambao wanalipwa kutokana na performance yao na kuwa na uhakika wa pensheni ya maisha.

Lakini all in all sisi wote, na yeye bwana Blater ni watumwa na hakuna mwenye haki ya kutawala mwenzake halafu asimjali.

Walio katika mifumo mizuri ya kipebari( chi zilizoendelea ambako kuna wachejazi wa kiafrika), wanawatumikisha wengine kufanya kazi ili walipe kodi,ili itumike kuendesha nchi.

Lakini pia at the same time wanahakikisha zile basic needs zote kama nyumba, maji, umeme, elimu na afya zinapatikana.

Kwa hio tuachane na huyu bwana Blater.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom