Je vipindi vya bunge vinahesabiwaje? Naomba msaada

Sharp lady

Senior Member
Feb 23, 2011
129
13
Hi wadau wa JF!
Naombeni muongozo wanamna gani vipindi vya bunge vinaheasabiwa, mfano tunaposema bunge la sita huwa tunaanzia wapi kuhesabu??
 
Hi wadau wa JF!
Naombeni muongozo wanamna gani vipindi vya bunge vinaheasabiwa, mfano tunaposema bunge la sita huwa tunaanzia wapi kuhesabu??

Tangu tuanze kuwa na uchaguzi wa Rais na wabunge nadhani kuanzia 1965 ndo Bunge la kwanza linaanzia hapo. Kila baada ya mika mitano kutoka 1965 mpaka uchaguzi wa 2010 kuna vipindi 10 vya miaka mitano mitano, na kila kipindi ina bunge lake. Bunge la sasa ni Bunge la 10 (Kama nimekosea, nisahihishwe). Katika Bunge kuna mikutano ya Bunge ambapo nadhani kila mwaka Bunge linakutana mara nne au tano. Katika kila mkutano kuna vikao kadhaa. Kwa mfano kwa sasa Bunge liko kwenye mkutano wake, na linafanya vikao vyake kila siku kwa kipindi cha miezi mitatu kulingana na ratiba. Hivyo ndivyo ilivyo! Kwa hiyo utakuwa na kitu kama kifuatacho kwenye kumbukumbu za Bunge
1. Bunge la 10 (2010-2015)
2. Mkutano wa (Namba zinahesabiwa kuanzia mkutano wa kwanza wa Bunge la kwanza)
3. Kikao cha .. (Namba zinahesabiwa kuanzia kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la kwanza)
 
Back
Top Bottom