Je viboko kufutwa mashuleni ni sahihi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je viboko kufutwa mashuleni ni sahihi!!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mageuzi1992, May 18, 2012.

 1. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba kwa sasa shule nyingi zimefuta adhabu ya viboko Mashuleni na nikweli kwamba hata mwanafunzi akikosa ni nadra sana kuona mwalimu anachukua kiboko kumpiga. Zaidi ya hilo kelele zimeendelea kuwa nyingi kwa shule ambazo bado zinaendeleza adhabu ya viboko!! Je ni kwamba viboko ni vibaya sana kiasi cha kuvizuia? Je wanafunzi kama sisi wa miaka ya 60s,70s,80s,90s tulionewa sana pale tulipokuwa tunachapwa viboko? je uelewa wa wanafuzi wa sasa ambao hawachapwi na wale wazamani wenzangu na mie ambao tulikula mboko za kutosha ni wapi wenye upeo?!
  Nawakilisha tu!
   
 2. s

  sugi JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kufuta viboko ni sahihi kabisa!kulingana na malengo yetu,kwa kweli kama ni zero tutazitengeneza mpaka basi maana watoto hawana discipline,hivyo kuondoa viboko kwa lengo la kumake sifuri ni sahihi kabisa
   
 3. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Funguka mkuu, haueleweki!
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mh! Ndo tutakuwa na vijana wa aina ya lusinde wengi zaidi ya huyu mmoja tuloko nae sasa
   
 5. s

  sugi JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Watoto wetu bila viboko hawaendi mkuu,matokeo yake ni discipline kushuka na kushusha performance pia
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  wanawajemgea kaburi watoto wetu, nakumbuka tulikua tunachimba visiki na kuchanja kuni kwa mita square huko kunakoitwa SeKuCo by then ilikua secondary school
   
 7. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mimi ni mpenzi wa nidhamu kwa watoto. wangu nahakikisha nidhamu ipo hata ikibidi kuwapiga(japo tunabaki marafiki wakubwa thereafter), hata mwalimu wao nimemwambia wakibidi kupigwa awapige. Lakini mimi ni mtetezi mkubwa watoto nakumbuka mwanangu wakati nikimuuliza kama alikuwa anafurahia shule yake mpya alisema hapana -aliniuliza wewe baba mtu akikuita mjinga utajisikiaje?
  Tulibidi tukae na mwalimu kuliweka sawa na baada ya hapo akaendelea kuifurahia shule.
  Tatizo la nidhamu na viboko ni kubwa kuliko tunavyolichukulia ila Tanzania ni wepesi wa kuiga. Katika shule zetu tujifunze mazingira yake na tuweke utaratibu muafaka wa kuhakikisha nidhamu bado inatunzwa sivyo tunalipoteza taifa la kesho kwa kuiga... haya majadialiano niliyosema hapa kati ya mwalimu mimi na mtoto hayawezekani kila wakati kwa hiyo tujenge utaratibu enedelevu na unaotilia maanani mazingira ya shule zetu nyingi(ratio ya teacher: pupil) tuwe practical tusiige tu
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,904
  Trophy Points: 280
  Haya ni matokeo ya kuiga sera za magharibi ili hali hazifit katika mazingira yetu. Ukiangalia kwa makini waalim wa sasa tunakoma huko mashuleni jamani lol! nidham ni mbaya sana maadili hakuna na kama sisi wengine hatuhitaj hata kuuliza unampotezea kama kawa ishu ni kwa wazazi wake na yy mwenyewe. Ukijaribu kufanya upembuzi yakinifu utagundua kuwa kama watanzania wa leo tungelelewa kama enzi zile ni wazi kuwa watot wa leo wangekuwa na nidham siyo tu ya maisha bali pia na ya kazi. sasa wazungu walipoona haya waliamua kutuletea haya wanayoita haki za binadam na sisi tuka adopt pasi kutafakar mazingira, nia yao has ilikuwa kupunguza responsible citizens, na kilichofanyika kibaya zaid wakaleta michezo kama pool table ikaenezwa kila mahali kwenye vijiwe so ikazidi zaid kudidimiza nafasi ya kumrekebisha mtoto.

  leo hii huwez kuamin wanafunzi hatuwachapi, na hata huko shulen what teacher cares is kuingia darasan, kufundisha na kutimiza wajibu wake mwingine. swala la mwanafunzi kaandika notsi, au kafanya tests, kaigia darasani siyo kazi ya mwalim kujua. manake ukimfualtilia pasi adhabu hakuelewi. mavuno yake ni haya ya watoto wasio na maadili. Halafu wafalsafa waliotangulia walisema " Behaviour change is the product of learning process, and this bahaviour should be in a positive way" and this positive way is pronounced as ethics" .

  sasa pia you can not attain behaviour change if you can not reinforce and motivate. Reinforcement is either +ve or -Ve. if it is -ve it means you induce something bitter forthe sake of attaining positive behaviour change. +ve reinforcement you remove something good from the said victim for the sake of attaining behaviour change. ukiangalia sasa utajua vitu ambavyo ni bitter ni pamoja na viboko na adhabu nyingine sasa najiuliza hivi watoto wa siku hizi ambao hawapati hivi vitu unategemea nini? Eti tumeshikilia tu motivational theory which yes it works but it has to go together with reinforcement kwani watoto wanatofautiana sana. ok tuangalie tuone
   
 9. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kukosa viboko shuleni ni sawa na kuandaa mapoyoyo na mavuta bangi ya kutosha kwa Taifa hili.
   
 10. d

  damashizo Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 13
  Swala hili la kama viboko vinasaidia au havisaidii hakika linasugua sana vinywa vya watu na mimi nikiwemo lakini sitaacha kuendelea kutoa mtazamo wangu kama ifuatavyo. Kwanza labda tuangalie hapahapa bongo kwa kulinganisha shule za international primary schools na nyingine za kawaida vip ufaulu wake? je zinatofautiana vip katika kufaulisha wanafunzi? je nini kinachangia shule za sent flan au internationa school kufanya vizur? je ni kwasababu wanachapa sana viboko? mi nafikiri ili mwanafunzi asome na kufaulu vizuri kazi moja tuu inahitajika hasa ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa ujumla wake. Mwanafunzi wa shule za msingi anavutiwa kwenda shule na kusoma kutokana na mazingira yaliyopo mfano wakipelekewa magari ya kusafiria kwenda shule hakika hakuna atakae toroka, akifika shule walimu wapo competent katika kufundisha na kushughulikia matatizo ya wanafunzi itasaidia sana, mazingira yote yaboreshwe yawe ya kuvutia sana kwa mwanafunzi hakika atasoma hata bila viboko. lakini unapo piga viboko ni kama kumpeleka punda mtoni na kujarib kulazimisha anywe maji
   
 11. The_Emperor

  The_Emperor JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 884
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Viboko ni lazima,hao wenyewe wanaopinga viboko mashuleni,walitandikwa ndio wakakaa kwenye mstari!!!live long viboko a.k.a stiki
   
Loading...