Je, uvaaji kofia ni kinyume na maadili ya mtanzania?

The August

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,080
2,024
Habari ya 'weekend' wakuu?

Mimi nimekuwa mpenzi sana wa uvaaji kofia. Na kofia ninayoipendelea zaidi ni zile wazungu waziitazo Ivy Caps.

Lipo jambo moja ambalo nimelishuhudia tangu ninakua, ni kuwa ukikutana na mtu aliyekuzidi umri then ukawa unamsalimia basi ile kofia unaivua, baada ya salamu unaivaa. Nami kwa kufuata mazoea basi huwa nafanya hivyo pia.

Basi leo nimemsaliamia mzee mmoja nikajisahau kuivua, yule mzee hakuonesha kukwazika, kinyume na nilichokitegemea.

Swali ninalouliza, je uvaaji kofia ni ishara ya uhuni kwa mila zetu watanzania? Au ni baadhi ya makabila tu?

Na kutovua kofia wakati wa salam je nao ni uhuni?

View attachment 1056316
images%20(3).jpeg
images%20(2).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijui kama ni movie tu au hata kwenye maisha halisi, kwenye sinema za marekani hua wanaonesha pale jeshi linapomtuma askari/ofisa wake kupeleka habari mbaya nyumbani kwa askari aliyepoteza maisha, basi yule askari mjumbe hugonga mlango na akifunguliwa huvua kofia ndipo anaanza kutoa pole na kuwasilisha hiyo habari ya msiba.
nadhani kuvua kofia ni ishara ya heshima
 
Kuna kipindi hubby alinunua cap..nikamwambia mbn unavaa kofia unakuwa km mhuni mhuni vile..akaniambia ninaficha upara...sasa sk 1 kaivaa..boss wake akamu0na akamwambia na ww ushakuwa mhuni sasa kwann unavaa kofia..???toka pale akaacha..kwakweli mwanaume anayevaa kofia awe btn 30 -50 mimi kwangu namchukulia MUHUNI..hana tofauti kbs na mdada anayechomekea dera kwa nguo za ndani!
Jitafakari best🤔🤔🤔🤔🤔
 
Jitafakari best
Sikutegemea ungekuja huku kuniabisha kiasi hiki....

Swali la Msingi, kwa unavyonifaham je kwa kuvaa kofia tu naweza kuwa categorized muhuni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushamba tu unakusumbua. Kofia ni kama miwani ya jua. Kazi yake ni kukulinda na jua dhidi ya mionzi ya jua. Watu wenye akili timamu na wenye madaraka na heshima kubwa kama vile Odinga, Obama, Museveni, Goodluck Jonathan, Waislamu na Obasanjo wanavaa pia. Na hata Magufuli pia huwa anavaa.

Back
Top Bottom