Hivi Utapeli ni Rukhsa tanzania? Maana naona mara nyingi watu wanafanya utapeli na hawakamatwi. Wanafanya utapeli Stendi, sokoni, kanisani, msikitini, barabarani, majumbani, mtandaoni n.k lakini hawakamatwi!
Hapa Arusha kuna wale matapeli wa bahati nasibu, japokuwa inajulikana kabisa wafanyacho ni wizi na utapeli tena hadharani lakini hawakamatwi!
Wapo matapeli nawajua takribani miaka ishirini na tano iliyopita. Wapo hapa Arusha na bado wanatapeli hadharani kabisa. Lakini hakuna wa kuwazuia maana walipo na polisi pia wapo.
Kiama yao yaja.
Nimeona niwanzishie uzi kabisa na ningeomba mamlaka inipe amri ya kuwaadhibu kama mwananchi mwenye hasira kali.