Je, Urusi itaivamia Ukraine

Je, Urusi itaivamia Ukraine

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,152
Reaction score
3,967
LENGO LA PUTIN LIMEANGUKIA PUA?

Putin alijua akitishia kuivamia kijeshi Ukraine Basi NATO wataogopa na kukubali matakwa ya Urusi ili asiivamie Ukraine. Malengo ya Urusi yalikuwa Kama ifuatavyo;

1. Marekani na Washirika wake wa NATO wasaini mkataba na URUS ambao utaipiga Marufuku nchi ya Ukraine kujiunga na NATO mazima.

NATO wamekataa takwa Hilo la URUS wakisema Uanachama wa Ukraine kujiunga NATO ni jukumu la uamuzi wa Mataifa 30 wanachama wa NATO. NATO imeongeza kwa kusema,URUS Haina mamlaka ya kuzuia Sera ya NATO ya OPEN DOOR POLICY hata Kidogo. Ukraine ikikidhi vigezo itajiunga na NATO.

2. Marekani na Washirika wake wa NATO waondoe Siraha zao ambazo wameipa nchi ya Ukraine tangu mwaka 2014. URUS imedai kuwa Ukraine ametumia Siraha hizo kuwapiga Washirika wa Urusi kwenye majimbo ya CRIMEA, DONBASS, LUHANSK na DONETSK.

Marekani na Washirika wake wa NATO inaonekana kabisa wamepuuza matakwa hayo badala yake Marekani na Uingereza wameongeza msaada wa Siraha kwa Ukraine hivi Karibuni.

3. Marekani na Washirika wake wa NATO wasijitanue kwa kuweka Majeshi yake na Siraha kwenye nchi za Ulaya Mashariki ambazo zilijiunga na NATO Kabla ya mwaka 1997. Hapa Urusi ilimaanisha nchi za ROMANIA, HUNGARY, LITHUANIA na LATVIA.

Marekani na Washirika wake wa NATO wamepuuza matakwa hayo. Hivi Karibuni rais wa Marekani JOE BIDEN ameiamuru wizara ya Ulinzi ya Pentagon kuwaweka Wanajeshi 8,500 tayari kupelekwa Ulaya Mashariki mda wowote ule. Tunavyoongea hivi Sasa,Wizara ya Ulinzi PENTAGON imeanza kuwapelekwa Wanajeshi 2,000 nchini Poland kutoka Marekani na Wengine 1,000 walioko Ujeruman imeanza kuwapeleka nchini ROMANIA.

Nchi za POLAND na ROMANIA zote Zina mpaka wa moja kwa moja na nchi ya Ukraine. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema wazi kwamba NATO haitapeleka Wanajeshi wake nchini Ukraine ambayo sio wanachama lakini itatoa usaidizi wa vifaa vya kijeshi vya kujilinda kwa Ukraine.
 
Kuna taarifa kwamba, Marekani imetoa 'ofa' ya mazungumzo na Urusi kuhusiana na masuala ya udhibiti wa silaha pamoja na Ukraine endapo Urusi itaondoa majeshi yake Crimea, Abkhazia na Ossetia Kusini (Georgia) pamoja na Transnistria (Moldova).
 
Kwanza urusi haijasema inataka kuivaimia ukraine mbaya zaid kila siku viongozi wa ulaya wanaenda kulilia kwa putin sasa ukraine ikataka ku test mitambo ikaingizia drone yake juu ya anga la belarus. Belarus ikaitungua ile drone kwa kutumia
img_1_1643134944301.jpg
electronic warfare system
 
1. Putin hatabiriki. Hakuna uhakika wa100% kuwa ataivamia Ukraine ila pia haiondoi possibility kuwa anaweza kuivamia na USA na Nato wasifanye kitu.

2. USA ana matatizo ya kutosha na vita na superpower tena mwenye full support ya China na North Korea, sio kitu anachowaza. Ukraine sio member Nato, USA hana atakachopata Russia.

USA anaplay hardball tu kujaribu kufanya deterrence ila game ikibuma ataishia kwenye sanctions na Ukraine inaweza bebwa kirahisi tu!
Kuna taarifa kwamba, Marekani imetoa 'ofa' ya mazungumzo na Urusi kuhusiana na masuala ya udhibiti wa silaha pamoja na Ukraine endapo Urusi itaondoa majeshi yake Crimea, Abkhazia na Ossetia Kusini (Georgia) pamoja na Transnistria (Moldova).
 
Kuna taarifa kwamba, Marekani imetoa 'ofa' ya mazungumzo na Urusi kuhusiana na masuala ya udhibiti wa silaha pamoja na Ukraine endapo Urusi itaondoa majeshi yake Crimea, Abkhazia na Ossetia Kusini (Georgia) pamoja na Transnistria (Moldova).
Jiandae kisaikojia

#S400 system equipment transported by rail in Belarus. Note the 51P6 TEL (capable of employing 400km-range 40N6 SAMs). This may be the first sighting of this TEL being moved in Belarus. https://t.co/SuXIGujoOB
 
Kinachonoshangaza ni kwamba. ....USA na washirika wake ndio wanaomba mazungumzo yafanyike .....ila Putin wala haongei sana
Acha fix naona umeigeuzakasome vizur Russia ndo anataka mazungumzo na watu wamekataa demand zake.....
 
1. Putin hatabiriki. Hakuna uhakika wa100% kuwa ataivamia Ukraine ila pia haiondoi possibility kuwa anaweza kuivamia na USA na Nato wasifanye kitu.

2. USA ana matatizo ya kutosha na vita na superpower tena mwenye full support ya China na North Korea, sio kitu anachowaza. Ukraine sio member Nato, USA hana atakachopata Russia.

USA anaplay hardball tu kujaribu kufanya deterrence ila game ikibuma ataishia kwenye sanctions na Ukraine inaweza bebwa kirahisi tu!
Urusi kuivamia Ukraine kwa sasa ni technically infeasible.

Putin yuko China hivi sasa. Ukifuatilia hotuba yake ya hivi karibuni na hii ziara yake, moja ya sababu ni kutafuta kuungwa mkono katika 'uwanja wa kimataifa' kwenye mgogoro wake na Ukraine.

So far, sijaona commitment ya maana ya China kuisapoti Urusi kwenye mgogoro wake na Ukraine zaidi ya deals za kibiashara. Isitoshe, China ina maslahi makubwa ya kibiashara na Ukraine pia.

Mtu pekee ambaye ameonesha kwa uwazi kumuunga mkono Putin katika huo "uvamizi" unaotarajiwa ni Lukashenko wa Belarus.
 
China kwa sababu za kibiashara hawezi kuiunga mkono Russia dhidi ya nchi za magharibi kwani anafahamu kufanya hivyo sio kwa maslahi yake na inaweza kumgharimu vilivyo.

Russia amebanwa kila kona na muda si mrefu ataomba poo.
 
Putin huwa hana maneno mengi....alianza hivyo hivo wakat ana imega CRIMEA....USA walikuja juu ..but hakuna kitu walimfanya .....Zaid ya vikwazo ambavyo jamaa bado tu anavimba

So hata hili NATO wanapiga tu kelele kupima kina cha uzito.

Hizi ni moja ya dhana za kivita zilizo pelekwa ....mpakaniView attachment 2108272
 
Ukraine wakidanganywa na US na NATO kwa kuwasaidia visilaha vidogo vidogo wakati huyu ni jirani yao anasema wazi yeye akiruhusu hawa Wakae mlangoni kwake wataleta shida kwake hilo liko wazi...Ina maana Ukraine ni ama ipigwe au isijiunge NATO....Iikishindikana ni kuipindua serikali uchwara inayotii masuala ya NATO...
 
Back
Top Bottom