Je, Unazijua sifa 10 za mke mwema?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,216
JE WAZIJUA SIFA KUMI ZA MKE MWEMA?

1. MKE MWEMA HUJAWA NA HEKIMA.
Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mwanaume anaempenda anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata mpaka marafiki wanatambua kuwa hali ni Mbaya. Mwanamke anaepiga kelele na mgomvi bibilia imemwita mwanamke mpumbavu
“Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.” MIT. 9:13
Ni vizuri kutofanya jambo kwa hasira na kuiruhusu hekima kukutawala

2. UVIVU SIO SEHEMU YA MAISHA YAKE.
Kuna wanawake ambao ni wavivu kupita kiasi hawawezi fanya jambo lolote wenyewe lazima kumtegemea dada wa kazi. Kila kitu huwa wanakua na sababu utasikia sipigi deki sababu kiuno kina mshituko, sifui nguo kuchazangu ni laini zinakatika, neno la Mungu linasemaje juu ya wanawake wa namna hii?
“Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu.” MIT. 22:13
Hawakosi sababu kwa kile wanachotakiwa kufanya,ili uwe mwanamke/mke mwema jifunze kujibiidisha na uache uvivu.

3. NI MSAFI, ANAYEJUA KUPANGILIA MAVAZI YAKE
Kuna wanawake ambao wanaamini wanaume wanaangalia tabia tuu. Sio kweli. Lazima avutiwe na wewe kwanza maana tabia haionekani kwa nje ni kitu cha ndani,so mwonekano wako ndio unaoweza kumfanya kutaka kujua tabia yako. Mwanamke/mke mwema anajua avae nini kwa wakati gani na anajua namna yakupangilia rangi za mavazi yake ili kuonekana akiwa na mvuto, Mwanaume anapomwangalia mwanamke anapata picha hata ya watoto wake watakavokua wanavalishwa.Sio tu mavazi hata mwili- ni vizuri kuwa msafi wa mwili sio kijasho cha hatari au harufu isiyo kuwa ya kawaida, kumbuka Mungu ndo anaangalia moyo ila mwanadamu anaangalia nje kwanza moyo badae kwa hiyo usafi wa mazingira na mwili ni jambo muhimu.“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.” 1 TIM. 4:12

4. HAKIKISHA UNATIMIZA MAHITAJI YA NDOA KWA MUME WAKO
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku.” Kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipiza visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama anapanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.

5. MWANAMKE ANATAKIWA KUJUA KUPIKA CHAKULA KITAMU, AMBACHO FAMILIA ITAFURAHIA.
Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani. Ni hatari mwanamke kuwaza ndoa wakati hata chai ukipika unaunguza

6. MWAMINI MUME WAKO WIVU NA HISIA MBAYA NI ADUI WA NDOA YAKO.
Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo, sio unaita watu nakuanza kusimulia madhaifu ya mumeo.
“Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu. Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka, Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao. Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,”
MIT. 9:13-16

7.MWANAMKE MWENYE HOFU YA MUNGU SIYO YA MUME
Ni hatari sana kuwa na mwanamke mwenye hofu ya mwanaume na siyo ya Mungu. Hofu ya Mungu itamfanya asifanye vitu kwa kificho maana anauhakika Mungu anaona kila sehemu, Mwanamke mwenye hofu ya Mwanaume ni janga maana machoni kwa mwanaume ni mwema kama kondoo akitoka hapo ni mbuzi mwenye pembe kali. Wakati mwingine wanaume wamekua wakijitia moyo watawabadilisha hao wanawake. Kama hakubadilika mkiwa rafiki usitegemee atabadilika ndoani.Mke akiwa mcharuko uwezekano mkubwa wa watoto kuwa kama mama ni mkubwa maana ndo anakuwa nao muda mrefu

8.MWENYE MATUMIZI MAZURI YA PESA
Hili ni jambo la msingi sana na wanawake wengi huwa hawajui wanaume wengi huwatega katika huu mtego na kuwapima. Siku zote usitake kukomoa kwasababu anaekununulia ni mwingine na sio wewe, mtu katolewa labda chakula cha jioni ataanza kuagiza vitu alivyokua anaviona kwa tv bila hata kujua bei yake mradi halipi yeye, au kama ni shoping atahakikisha kanunua kila kitu alichokuwaga anawaza maishani bila kujali gharama kwa alie mtoa. Lakini pia hata kama ni kwa hela yako mwenyewe jifunze kuwa na akiba. Ni aibu sana mwanamke/msichana mwenye zaidi ya miaka 20 kutokua na akaunti/fedha ya akiba.

9.KUJISHUSHA NA KUOMBA MSAMAHA
Ugomvi mwingi kati ya mwanaume na mwanamke au mume na mke mara nyingi hutokana na wote kutaka kua juu hakuna aliyetayari kushuka. Kumbuka mwanamke ndio mlinzi wa ndoa. Wakati mwingine kushuka kwako ndio kunaweza pelekea mume/mwanaume naye kuona makosa yake lakini kutojishusha mara nyingi huleta magomvi ambayo mwishowe huleta aibu
“Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.”
MIT. 11:2

10.MWENYE MAWAZO YA KUENDELEZA FAMILIA.
Mwanamke mwenye upeo mpana wa kufikiri sio yule anaewaza namna ya kubadilisha ma dera, mwanamke mwema ni yule mwenye kukaa na kushauriana na mumewe juu ya mipango ya maendeleo na kumtia moyo mumewe juu ya mipango aliyonayo na sio kuwa kikwazo kwake na kumuonyesha kuwa hawezi kufikia malengo yake.

C&p.
 
Kwa hapa Dar hawapo hata wenye moja kati ya hizo
Watu wanakula kula kama Mbuzi
Vyumba vichafuuu
Nywele zinanukaaa
 
Ni ngumu kuwapata hawa,wanaweza wakapita hapa na wakayaona haya uliyoeleza lakini bado watasema mfume dume na matokeao yake wanabaki palepale,ni shida.
 
Kama Mi demu (sijamuoa)wangu ninayeishi naye hana ata sifa moja bora kati ya izo.yupo kinyume chake.yaan balaaa.
 
MAJIBU YA HIZO SIFA ZAKO ULIZOWAPA NI KAMA YAFUATAYO:

1. Leo Hii HEKIMA Ya Mkeo Utaijua Kama Una Pesa Ila Ukiwa Huna Tegemea DHARAU.
2. 85% Ya WANAWAKE Wa Leo Ni WAVIVU Kiasi Kwamba Hata CHUPI Zao Tu Wanafuliwa.
3. Hawa Tunaowaoa Leo Usafi Wao Uko Ktk USO Tu Lakini Kule " KUNAKO " Ni Jipu La Kutumbuliwa.
4. Wanawake Wa Leo KUKUPA PENZI Ni Mpaka Roho Mtakatifu Aseme Nae Vingine Utapiga Mno PUNYETO.
5. Wanawake Wa Leo Kupika Hawajui Na Wanaweka Oda Kwingine Ukirudi Unakuta Tu Chakula Mezani.
6. Hawa Tunaowaoa Leo Usipoonyesha Tu WIVU Kwake Utawajibika Kupima DNA Za Wanao Kila Mwaka.
7. Tunaowaoa Leo Hawatishiki Sana Na Mungu ILA Wanawaogopa Na Kuwaabudu Mno WAGANGA Wa Kienyeji.
8. Hawa Tunaowaoa Leo MATUMIZI Yao Yanazidi Hata Ya MALKIA Wa Uingereza Na Usipotimiza Utagongewa Mno.
9. Hawa Tunaowaoa Leo Akijishusha au Kuomba Msamaha Kwako Jua Anataka KUKUPIGA Mzinga Wa Hela.
10. Tunaowaoa Leo 95% Ya Mawazo Yao Ni Jinsi Tu Ya KUKUCHUNA Na Ikibidi AKUUE Arithi Mali Ale Dume Mwingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom