Je, unayajua maneno haya?

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Katika mambo ya utawala na menejiment (administration and management), kuna istilahi mbalimbali zinazohusika ambazo huenda hazijajulikana kwa wengi. Kwa mfano:

1. Mrejewa – referee (unayemuweka kwenye barua yako ya maombi ya kazi). Pia anaitwa mdhamini.
2. Masurufu – imprest
3. Posho ya kujikimu – subsistence allowance
4. Posho ya takrima – entertainment allowance
5. Posho ya ukaimu – acting allowance
6. Sitirifu – confidential
7. Kadimisho la uteuzi – offer of appointment
8. Mwelekezi – consultant
9. Watoto tegemezi – dependent children
10. Bainifu – outstanding
………….
Kiswahili kinasonga mbele.
 
Hiyo namba 10 ni msimama nje.
Sina uhakika na hiyo maana mkuu, :D:D lakini kwa muktadha wa utawala ni kama mtu akitaka kusema, kwa mfano:
This was an outstanding performance.

Basi tutasema: Huu ulikuwa ni utendaji bainifu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom