Je, unayajua maneno haya?

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
285
500
Katika mambo ya utawala na menejiment (administration and management), kuna istilahi mbalimbali zinazohusika ambazo huenda hazijajulikana kwa wengi. Kwa mfano:

1. Mrejewa – referee (unayemuweka kwenye barua yako ya maombi ya kazi). Pia anaitwa mdhamini.
2. Masurufu – imprest
3. Posho ya kujikimu – subsistence allowance
4. Posho ya takrima – entertainment allowance
5. Posho ya ukaimu – acting allowance
6. Sitirifu – confidential
7. Kadimisho la uteuzi – offer of appointment
8. Mwelekezi – consultant
9. Watoto tegemezi – dependent children
10. Bainifu – outstanding
………….
Kiswahili kinasonga mbele.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom