Magoya2000
JF-Expert Member
- May 7, 2017
- 641
- 1,266
Najua vijana wengi wamekata tamaa ya kuona kutoka na challenges zinazotokea. Lakini napenda kuwaosia hii sio wanawake wote ni capable kuolewa ni sawa na maisha ya kawaida haiwezekana wote tukawa matajiri. Mke mwema kumfahamu ni process, mojawapo unatakiwa kumuangalia mama yake. Nazungumza hili maana wamama wengi wamechangia ndoa nyingi kuvurugika. Kuna dada alikuwa anagombana na mumewe everyday when, ugomvi wake alikuwa anaupeleka kwa mama yake, mama yake alikuwa anamwambia vumilia leo they are happy no more conflict. Maisha ya mama mkwe yanareflect ya mkeo mtarajiwa. Kama mama kavurugwa jua wazi watoto nao watavurugwa, note mama ndo mlezi wa familia. Pia hofu ya Mungu ni jambo muhimu la kuangalia wengine wana pretend hapa watch out. Angalia kwenye mahusiano yako je mwanamke au mwanaume anapokosea yupo tayari kujishusha na kuomba msamaha. Maana watu wengi wenye tabia ya kuomba msamaha ni watu wapatanishi hawapendi ugomvi. Kuna wengine ugomvi kwao surnah. Haya ni baadhi nakawasilisha