Nina ndoto ya muda mrefu juu ya kufungua NGO je ni mambo gani nizingatie ili niweze kufungua NGO
Katika masuala ya NGO, kuwa na ndogo ni jambo la kwanza ila kuwa na sababu na nia ni muhimu kuliko ndoto.
Kwa nini ninasema hivyo? Sababu kubwa ni namna namna unavyoweza kuitegemeza asasi yako katika kipindi kigumu cha kusubiri.
Unapoanzisha asasi ndogo unapaswa kujua siku za mwanzoni itatumia gharama nyingi za msingi ambazo zitatoka kwa waanzilishi.
Sasa kwa kuwa umeuliza mambo ya kuzingatia naomba niyaweke katika makundi mawili.
Kundi la kwanza ni mahitaji ya kisheria, taratibu na miongozo.
1. Unapaswa usajili asasi yako serikalini. Hapa unaweza usajili kwa level ya wilaya, mkoa, au nchi. Zoezi la usajili ni zoezi lenye changamoto zake maana utapitia mlolongo wa ofisi za serikali za mitaa hadi wizarani. Zoezi gumu la wizarani ni katiba kuwa sawa na viwango vyao. Hapa unaweza kurudi mara kadhaa.
2. Baada ya usajili, sasa unaingia katika ulimwengu halisi wa asasi za kiraia. Hapa utatakiwa kuhakikisha kuwa mifumo yako IPO sawa. Sera na miongozo mbalimbali mfano HR manual, sera za fedha manunuzi, za mazingira, za watoto ni nyingi kulingana kazi zenu. Zote zinatakiwa ziwepo. Pia job descriptions na mafail ya staff, barua za Ajira na terms zao za ajira.
3. Baada ya hapo sasa ni utafutaji wa ufadhili. Hapa waweza tafuta ufadhili wa ndani au nje ya nchi. Hili nimelieleza vzr katika mada yangu iliyopita.Ila vitu muhimu hapa ni
a.Kupata taarifa sahihi za ufadhili.
b. Networking ukitaka uwe na mafanikio ni muhimu uwe vzr hapa.
c. Muandishi mzuri wa proposal
d. Lobbying - Technical know who & how
Nadhani maelezo haya yatakusaidia.