Je, unatafuta FURAHA maishani? Soma hapa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, unatafuta FURAHA maishani? Soma hapa...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 11, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hivi sasa nikiangalia, naona watu wengi wasio na furaha ni wale wanaojaribu kushindana na hali halisi. Mawazo yao iwe wanajua au hawajui huwaambia kwamba wanaweza kuthibiti hali halisi. Ukweli ni kwamba haiwezekani, hakuna anayeweza kudhibiti au kubadili hali halisi. Kama mazingira yanabadilika na huwezi kuyadhibiti, unachotakiwa kufanya ni kukubaliana nayo, kukubali kusogea nayo pamoja, hiyo ndiyo siri ya kuyamudu, bila ya kujali yako kwenye sura gani.

  Kujaribu kudhibiti jambo au kitu ambacho hatukiwezi, ni kujiumiza kiakili, kihisia na kimwili pia, ni kujinyima furaha. Jambo muhimu zaidi ni mtu kujua kwamba, anachoweza kukidhibiti au kukibadili ni yeye mwenyewe, siyo kingine chochote kilicho nje yake. Kuna kitu kimoja tu, ambacho mtu anaweza kukidhibiti hapa duniani, nacho ni yeye mwenyewe. Huwezi kudhibiti hali ya hewa, hivyo kuumia mvua inaponyesha na biashara yako kushindwa kuuzika ni kuzidi kujiumiza bure.

  Huwezi kumdhibiti mkeo au mumeo, hivyo kukerwa na mambo yake ni kujiumiza zaidi tu. Nje ya imani zako, mawazo yako, mitazamo na matendo yako, hakuna kingine unachoweza kukidhibiti. Jaribu kujifunza namna utakavyoweza kudhibiti imani, mawazo, mitazamo na matendo yako ili visikupe maumivu. Vile vyote vilivyo nje yako ambavyo huna uwezo wa kuvidhibiti, viache vitokee, visikusumbue. Ukimudu kufanya hivyo, hakika utaanza kuhisi tofauti. Halafu fanya uamuzi kuhusu kile unachokitaka maishani mwako, kisha ng'ang'anie hapo. Ni vema mtu kuishi akiwa anajua anataka kitu gani hasa, anataka maisha yake yawe vipi hasa, kwani kubahatisha maisha huondoa sana furaha ya mtu. Bila kujua twendako maisha ni vurugu tupu. Ni vema kuchagua kile ambacho mtu anapenda kukifanya bila kutoka nje. Kumbuka kwamba mara nyingi hatuna furaha kwa sababu hatujawahi kuwafanya wengine wafurahi.

  Tukishawafanya wengine wafurahi ni wazi na sisi tutakuwa kwenye furaha kubwa kuliko wao. Ukitaka kuwa na furaha unapaswa kuwa na marafiki wenye kutia moyo na kufikiri kwa mkabala mzuri. Watu ambao wanaaminika na wenye hekima na busara anapokuwa karibu na wewe, hakuna kitu chenye kufurahisha kama hicho. Kuna mambo kama uimara wa ndoa au uhusiano na mpenzi. Kama unataka kuwa na furaha ya kweli ni lazima uhakikishe kwamba umejitahidi na kujenga uhusiano mzuri na mke, mume au mpenzi wako. Juhudi hizi kwa sehemu kubwa ni lazima zitokane na wewe kumkubali mwenzio kama alivyo ili uweze kusaidiana naye karibu kwa kadiri inavyowezekana.

  Kuna mengi ambayo yanaweza kumsaidia mtu kuwa na furaha ya kweli maishani, lakini yote hayo yanategemea mtu anavyojiona mwenyewe na alivyo tayari kukubaliana na yanayomtokea kila sekunde, dakika , saa na maisha yake yote. Furaha ipo, ni suala la mtu kuichukuwa na kuitumia.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Post hii ni dedication kwa mpwa wangu mpendwa mama Angelina aliyeko Kibaha ambaye ndoa yake imekumbwa na kisirani na kuvunjika rasmi jana. Nakusihi usivunjike moyo, wewe bado ni binti mdogo na mrembo, tukio hilo lisikuvunje moyo bali likupe shime ya kusonga mbele na maisha, kwani huenda kuna jambo ambalo umeepushiwa na Mwenye enzi Mungu. kukosa furaha na kujuta hakuwezi kukusaidia kwa sasa, bali kufurahia maisha ndio njia pekee itakayokuwezesha kufikiri kwa mkabala tofauti kwa ustawi wa maisha yako na mwanao Angelina.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi nakubaliana kabisa na hili,lakini nina sijui ni swali au ni kitu gani,lakini wacha niseme halafu utaliweka katika namna inavyotakiwa.Kwenye suala la mazingira na yanavyobadilika,hapo kwenye kukubaliana nayo nina tofautiana napo.Mi nadhani sio kukubaliana nayo yote,lakini pale unapoyakataa iwe ni kwa namna isiyokuumiza.Mfano,kwenye maisha haya kuna mambo kama wanandoa kuhalalisha cheating bila sababu za kimsingi,vijana wengi kupenda usharobaro na umarioo,wanawake kupenda kutokuvaa mavazi ya kujisitiri,uonevu kwa wanawake na masikini n.k.Haya ni baadhi ya mambo ni kama yameshahalalishwa na jamii na ni kawaida kuyaona yanatendeka.Na pia nadhani ni moja ya mabadiliko ya mazingira.Kiukweli haya ni moja ya mambo sikubaliani nayo na sitayasapoti kwani naamini yako kinyume na ubinadamu.Labda tukubaliane yapo ya kuyakubali na mengine siyo.Naomba unisahihishe if am wrong!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  naunga mkono hoja hasa hapo kwenye bold! Waswahili wanasema, raha jipe mwenyewe!
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Asante sana kwa somo lako zuri mzee Mtambuzi. Nitazingatia ushauri wako.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Hivi sasa nikiangalia, naona watu wengi wasio na furaha ni wale wanaojaribu kushindana na hali halisi. Mawazo yao iwe wanajua au hawajui huwaambia kwamba wanaweza kuthibiti hali halisi. Ukweli ni kwamba haiwezekani, hakuna anayeweza kudhibiti au kubadili hali halisi. Kama mazingira yanabadilika na huwezi kuyadhibiti, unachotakiwa kufanya ni kukubaliana nayo, kukubali kusogea nayo pamoja, hiyo ndiyo siri ya kuyamudu, bila ya kujali yako kwenye sura gani.
  Mtambuzi nakubaliana na wewe kwani ultimate goal ya yote tunayofanya hapa duniani (kutafuta elimu, kazi nzuri, kufanikiwa kibiashara n.k) ni kwa sababu ya kupata furaha katika maisha japokuwa wengi wanachacharika huku na kule wakiamini wanataka kuwa na maisha mazuri lakini ukishatimiza lengo la kuwa na maisha mazuri maana yake lengo la kutafuta furaha litakuwa limetia. Tatizo linakuja watu wanakosa furaha kwa kuwa wanashindwa kukubaliana na hali halisi na mwisho wa siku wanakuwa watu wa mawazo mengi. Na hii yote inatokana na watu kujipa hadhi ambazo sio zao kwa kuishi maisha kwa kuongozwa na hisia za watu wengine (mfano mtu budget yake kwa mwezi laki 2 lakini anajiweka katika budget ya laki 4 ili marafiki na jamaa zake wasimwone kapigika). Katika situation kama hii mtu atabaki na furaha fake pindi anapokuwa na jamaa zake lakini anapokuwa peke yake ni majuto na kujifyonza kila mara
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold ndipo ndipo lilipo jibu lako.

  Lakini pia waweza kuchota busara katika uzi huu niliowahi kuuweka hapa:

  BADILI:
  Unapojikuta kwenye hali usiyoipenda, unaweza kufanya jitihada za kuibadili au kubadili mtazamo wako kuhusu hali hiyo. Ikiwa uko katika uhusiano unaodhani haukusaidii kwa mfano, unaweza kwenda kwa washauri nasaha, unaweza kuzungumza na mwenzi wako na kujaribu kuufanya uhusiano huo uwe bora zaidi ama waweza kubadili mtazamo wako wa namna uhusiano wenye faida unavyotakiwa kuwa.

  Mara nyingi huu ni uchaguzi mgumu sana kuufanya kwa sababu inaweza ikalazimu kumkabili mtu mwingine kutoka katika tabia isiyo na faida kwako. Kubadilika kunatuondoa kwenye nafasi yetu tuliyoizoea na ambayo tunaiona inatufariji na kunahitaji ujasiri mkubwa kufanya hivyo.

  Kuamua kuacha kumtegemea mpenzi kukupa furaha na kutafuta furaha kutoka vyanzo vyenye kuaminika zaidi siyo jambo rahisi, lakini ni muhimu.

  JIONDOE: Kama umeshindwa kubadili hali kwa sababu yoyote ile umeshindwa kumfanya mtu abadili tabia yake kwa mfano, ni bora kujiondoa, ondoka kabisa. Kujiondoa kunakufanya uondokane na hali isiyofurahisha na kunasafisha njia kwako kwa ajili ya kuchagua jambo jingine mbadala. Ni wazi,watu wengi hukimbilia kuchagua njia hii, hukimbilia kujiondoa kwa sababu huogopa sana kujaribu njia ya kwanza ya kubadili hali ama kubadilika wao wenyewe.

  Lakini ingawa kukimbilia hatua hii bila kujaribu ya kwanza si busara, kuna wakati ambapo kujiondoa ni hatua pekee ifaayo kuchukua. Hata hii nayo inahitaji ujasiri mkubwa kwa sababu, mara nyingi akili zetu hutuweka katika nafasi ya kutumia methali ya ‘Zimwi likujualo' kama utetezi wa kuendelea kuvumilia madhila yasiyo muhimu tunayokumbana nayo.

  KUBALI: hatua ya mwisho unayoweza kuchukua kukubali. Ziko hali ambazo huwezi kuzibadili na kukwepa ukweli wa jambo hilo, ni sawa na wendawazimu. Hebu mfikirie mfungwa wa kisiasa kama ilivyokuwa kwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini na wenzake. Wakati alipokuwa akishikiliwa jela, asingeweza kuibadili hali ile, wala asingeweza kuamua kuondoka. Hakuna jingine aliloweza kufanya ila kukubali hali halisi na kufanya kila analoweza kuishi katika hali hiyo. Kuna wakati kukubali linakuwa ni chaguo la kwanza tunalopaswa kuelekeza macho yetu, wakati tukiwa tunafikiria njia bora ya kubadili hali au kujiondoa.

  Nina hakika kila mtu anapotazama mambo yanayozunguka maisha yake, atakutana na moja ambalo haridhishwi nalo kwa asilimia 100. Utafanya nini kushughulikia hilo, utajaribu kubadili hali au mtazamo wako wa hali? Uko tayari kujiondoa ikiwa una hakika huwezi kubadili hali au uko tayari kubadili mtazamo wako kuhusu jambo hilo ili uweze kuendelea nalo? Uko tayari kukubali kile ambacho huna uwezo wa kukibadili na wala huwezi kujiondoa?


  Nafasi ni yako kutumia busara zako kuchagua.
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Mtambuzi nimekusoma ila hiyo name calling sijui kama inaruhusiwa JF Mama Angelina tena aliyeko Kibaha?????
   
 11. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nielekeze hiyo namna ya kudhibiti imani, mitazamo na matendo. Nataka kujifunza sasa.
   
 12. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mtambuzi, nakubaliana na wewe katika hili.

  Kwa maisha haya ya sasa uwe wewe, tena uwe wewe kabisa.
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Dena Amsi, habari ya siku dadaa!
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Nzuri niko mzima wewe je????
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mzima kabisa, umepotea sana!
   
 16. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 80
  Asante kwa somo zuri Ndugu.Mtambuzi nina matarajio makubwa ya kuwa na furaha baada ya kusoma thread hii nimevutiwa na baadhì ya aya hizi katika thread yako naamini kama mtu yeyote atakayezisoma aya hizi chache na kuzielewa itamsaidia sana-watu wanaojaribu kushindana na hali halisi huwa mara nyingi hawana furaha. -hakuna mtu yeyote anayeweza kudhibiti au kubadili hali halisi. -kujaribu kudhìbiti jambo au kitu ambacho hatukiwezi ni kujiumiza kiakiakili,kihìsia na kimwili pia ni kujinyima furaha. -jambo muhimu zaidi ni mtu kujua kwamba kitu pekee anachoweza kukidhibiti au kukibadili ni yeye mwenyewe na si hali halisi.-Nje, ya imani yako,mawazo yako,mitazamo na matendo yako hakuna kingine unachoweza kukidhibiti. -kumbuka kwamba mara nyingi hatuna furaha kwa sababu hatujawahi kuwafanya wengine wafurahi....hapa ndipo uliponikuna hasa unaposema "Furaha ipo,suala ni mtu kuichukua na kuitumia" Thanks Bw.Mtambuzi somo limeeleweka vyema,,..May Allah right your dreams.
   
 17. M

  Mzee wa fund JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika jinalako sawa na wewe.
   
Loading...