Sipendelei kofia.
Mashati napenda ya draft, yenye pattern zisizokufanya ushindwe kuelewa na rangi zilizotulia rangi kali kama orange, nyekundu, kijani sivai. Matirio ya mtelezo sivai, napendelea cotton.
Fulana za V au golfer napendelea kushindia singlendi ova saizi ambazo zitaonyesha mwili wangu kwa ukubwa.
Kutegemea na eneo lakini kama eneo linaruhusu pensi nitavaa pensi.
Mguuni, sipendelei soksi. Navaa kiatu chochote kitakachoendana na juu ila kisiwe mdosho.
Na hayo mavazi yote napendelea yakiwa mtumba (naambiwa kwa kua sina hela.)