Je,unapenda nini katika mavazi? Juu,kati au chini..

Malingumu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
616
429
Habarini wapenda mitupio..

Ni ukweli kuwa mavazi yapo ya aina na namna mbalimbali kulinganga na mahali panapositiriwa.

1.Kuna Juu zaidi (hapa ni kofia,mizula n.k)
2.Kuna katikati., (Hapa ndipo mahala pa T-shirts,mashati,vitop na viblauzi kwa wenzetu KE na aina nyinginezo)
3. Chini karibu na chini zaidi ...(Hapa ni mahala pa suruali,kaptula,pensi, sketi...)
4. Chini zaidi...( Hapa viatu vinahusika. vyaweza kuwa vya wazi au vya kufunika)

Je, kati ya hizo wewe ni sehemu ipi ambayo unapenda sana mavazi yake/ mavazi gani wewe hupendelea?

Mimi binafsi napenda sana viatu, vya aina zote vya kufunika au vya wazi(sandals), yani navipenda mno. Yani kwangu viatu ni vingi kuliko idadi ya suruali...

Karibu tushee....
 
No. 2 katikati kutupia vikoti na viblauzi vya ukweli nikienda job...naweza vaa sketi au suruali moja mwezi mzima but hapo kati nabadilisha daily na hakuna atakaye note kwamba chini ni mrudio
 
No. 2 katikati kutupia vikoti na viblauzi vya ukweli nikienda job...naweza vaa sketi au suruali moja mwezi mzima but hapo kati nabadilisha daily na hakuna atakaye note kwamba chini ni mrudio
Kumbe wewe ni KE nilikuwa najua ME
 
Binafsi napenda kuanzia juu mpaka chini nitoke chicha...ila kofia inategemea na sehemu husika ninayotoka
 
Sipendelei kofia.

Mashati napenda ya draft, yenye pattern zisizokufanya ushindwe kuelewa na rangi zilizotulia rangi kali kama orange, nyekundu, kijani sivai. Matirio ya mtelezo sivai, napendelea cotton.
Fulana za V au golfer napendelea kushindia singlendi ova saizi ambazo zitaonyesha mwili wangu kwa ukubwa.

Kutegemea na eneo lakini kama eneo linaruhusu pensi nitavaa pensi.

Mguuni, sipendelei soksi. Navaa kiatu chochote kitakachoendana na juu ila kisiwe mdosho.

Na hayo mavazi yote napendelea yakiwa mtumba (naambiwa kwa kua sina hela.)
 
Me viatu ndio kila kitu.... raba na boots huhuhuhuhu nikiona kiatu kizuri afu sina hela hua naumwa kabisaaa ila nguo sina makuu sana.
 
Sipendelei kofia.

Mashati napenda ya draft, yenye pattern zisizokufanya ushindwe kuelewa na rangi zilizotulia rangi kali kama orange, nyekundu, kijani sivai. Matirio ya mtelezo sivai, napendelea cotton.
Fulana za V au golfer napendelea kushindia singlendi ova saizi ambazo zitaonyesha mwili wangu kwa ukubwa.

Kutegemea na eneo lakini kama eneo linaruhusu pensi nitavaa pensi.

Mguuni, sipendelei soksi. Navaa kiatu chochote kitakachoendana na juu ila kisiwe mdosho.

Na hayo mavazi yote napendelea yakiwa mtumba (naambiwa kwa kua sina hela.)

nimekupenda !hasa unaposema huvai kofia jaman sijui ni malez au nn sipend men anayevaa kofia !naona km uhuni fulan !arghhhh !
 
Mara nyingi MVUTO huanzia SHIRT/TISHIRT......na CHINI kwenye Kiatu....hapo kwenye kiatu ndy kunaonyesha UMETEMBEA KILOMETRES ngp ....hata mtu anapokutazama anatazama juu na kiatu....
 
Unaeza penda chini juu kaharibu yanini nipate shida napenda kote kuanzia juu hadi chini zaidi
 
Back
Top Bottom