Je, unapenda kuwa mbunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni?. Jiunge na CCM au washirika wa CCM sasa

Mbuzimtu

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
355
178
Ndugu mwanaJF, Salam!.

Kwa namna hali ya kisiasa inavyozidi kuvuma ndani ya Ukawa na kuwa mbaya ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), naomba kutowa ushauri kwamba, wale ambao wanapenda kuwa wabunge wa upinzani kuanzia November 2015, wanashauliwa kujiunga na CCM kabla ya majina ya wabunge watarajiwa kupelekwa ofisi kuu kwaajili ya uchambuzi.

Ushauri huu ni zao la uwezekano mdogo CCM kubaki chama tawala ifikapo November mwaka huu. Kwasababu hiyo, natowa wito na ushauri kwa kila mtu mwenye malengo ya kuwa mbunge kupitia chama cha upinzani, asipoteze muda, CCM inazonafasi nyingi za kugombea . Watu wanashauliwa kujiunga na CCM au chama chochote ambacho kitashirikiana na CCM kuunda kambi ya upinzani bungeni.

Inaaminika kuwa, vyama vyote ambavyo havimo kwenye umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ni matawi ya CCM. Kwa hiyo kama ukiona CCM haitokufaa, unaweza kujiunga na vyama vingine tofauti na CCM ili kutimiza haja ya kuwa mbunge wa upinzani.


Utakayesikia taarifa hii mfikishie na mwenzako.


Ni mimi mwanaushauri. ukipenda fuata ushauri wangu kama hutaki komaa na msimamo wako.ushauri sio lazima uufuate.
 
Back
Top Bottom