Je, unamkumbuka faru John?

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,520
2,000

Faru John....! Mnyama ambaye alijipatia umaarufu mkubwa sana baada ya kifo chake, Umaarufu wake huo ulitokana na madai ya Mh. Waziri mkuu Kassim Majaliwa kuwa kumekuwapo na taarifa ya kwamba mnyama huyo alihamishwa kwa siri kutoka Ngorongoro na kupelekwa pori tengefu Gurmeti, huku baadhi ya watumishi wakipewa Ml. 100 na Ml. 100 nyingine zikitolewa kwa ahadi ya kufuata hapo baadaye, hapa ndipo kasheshe na maneno mbali mbali yalipoanza kuzuka, mara alikufa na akazikwa mara kaburi lake halipo, visanga hivyo vilizidi kuchochea sana mnyama huyu kujitengenezea umaarufu mkubwa katika mipaka na nje ya mipaka ya Tanzania.

LAKINI JE UNAFAHAMU FARU JOHN ALIKUWA NANI ?

Ili umfahamu vyema nitakurudisha tena Ngorongoro huko ndiko ambako mnyama huyu yalikuwa makazi yake, akiwa na utajiri wa marafiki na majike wa kutosha, katika hifadhi hiyo asilimia 70.2 ya faru walioko huko yeye ndio alikuwa baba, idadi ya faru wote ngorongoro ni 35 tuu na kati ya hao 26 ni wanaye wa kuwazaa, alikuwa ni faru Mzee na mwenye heshima kubwa sana, pembe zake zilikuwa na uzito mkubwa iliyo kubwa ilikuwa na uzito wa kg 3.6 na ndogo ilikuwa na uzito wa kg. 2.3, hivyo ukimuondoa Faru Fausta ambaye ni Mzee kuliko faru wote Afrika ni wazi John naye alikuwa yumo.

Ulinzi aliokuwa akipewa ulikuwa si wa kitoto, mbali na kufungwa vifaa vya GPS, Camera na kufuatiliwa kwa saa zote 24, ni takribani laki mbili na ishirini na tano (225,000/=) zilikuwa zinatumika kwa siku kwa ajili ya uangalizi wake ambapo ni sawa na Tsh 81,000,000 kwa mwaka.

JE KIFO CHAKE KILITOKANA NA NINI ?

Kwa heshima kubwa aliyokuwa nayo uchunguzi wa kifo chake ilibidi ukafanyikie huko Pretoria South Africa, Ambapo wataalamu toka ofisi ya mkemia mkuu wakiongozwa na Prof Manyele walirejea na majibu yafuatayo :

1.Mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu na udhaifu wa wizara na taasisi zake.
2. Kukosa Matibabu alipoumwa.
3. Matunzo na uangalizi wa mnyama huyo.

HAPA UNAWEZA JIULIZA JE NI MATUNZO GANI HAYO HALI YA KUWA WANYAMA HUJITEGEMEA WENYEWE.

Safari ya kifo cha Faru John ilianzia tarehe 17,Dec mwaka 2015, ambapo faru John alikuwa anaondolewa katika hifadhi ya Ngorongoro na kuhamishiwa katika pori tengefu la Grumeti huko Serengeti, ikumbukwe kwamba Faru John katika hifadhi ya Ngorongoro alikuwa anaishi kwa raha mustarehe kwa kuwa jilani na familia yake kubwa, Mzee mwenzie Faru Fausta, achilia mbali maeneo kadha wa kadha ambayo alikuwa anavinjari na mshikaji wake marehemu yaani Faru George.

Kizaazaa kilianza alipofika huko Grumeti ambapo kulikuwa na Faru jike al maarufu kwa jina la Faru Khadija, kwa mara ya kwanza walikutana mtoni walipokuwa wamefuata maji baridi, Faru John asijue ya kwamba kwa kipindi hicho Faru Khadija bado alikuwa na majonzi ya kupoteza dume lake ambalo lilipokea kipigo kikali toka kwa kundi la Tembo mpaka akapoteza maisha.

Faru john alianza kufunguka ya moyoni akitaka kumrithi Faru Khadija ambaye ndio kwanza bado alikuwa mbichi mbichi, Faru Khadija macho yake yalipomtizama John, moyo wake haukuridhia, kwanza hakusita kumkataa kwa sababu ya uzee wake, ngozi yake iliyojikunja Khadija alijesemea moyoni mwake ya nini magonjwa mimi, na kama haitoshi alijitenga naye kwa jeuri hali iliyoleta tafsiri ya kwamba ujana wako ule na nani mpaka uzee wako uniletee mie ?

Kwa hayo ambayo alikuwa anakumbana nayo Faru John, alianza kudhoofu mwili, mawazo yalimtesa, kula kukawa shida, kulala kwa tabu, mapenzi yakawa mwiba mkali kwa Faru John huku Khadija akitambaa tuu viwanja mbalimbali vya Grumeti Serengeti.

Hata hivyo pamoja na maumivu makali hayo ya ndani kwa ndani, bado wahusika walikuwa hawachukui hatua za makusudi za kumuokoa mzee huyo aliyeacha watoto wa kutosha huko Ngorongoro mpaka pale ambapo umauti ulimfika, Mzee mwenzie Faru Fauster kwa sasa naye ni mgonjwa kiasi cha kupangiwa diet maalum kutoka nje ya nchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom