Je, unajua? Shetani anaweza kukupa mapesa, lakini...

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,707
Reaction score
7,433
Kuna watu wanakiri kwamba wamepata utajiri baada ya kupewa "dawa" na waganga wa kienyeji au wachawi. Kulingana na Maandiko, inawezekana shetani akakupa mali lakini lazima ukubali kumsujudia. Katika Luka 4:5–7 imeandikwa:
"Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."

Hii inaonyesha kuwa Shetani ana uwezo fulani wa kutoa "fahari" na "enzi" ya kidunia — mali, mapesa, heshima — lakini kwa masharti kwamba lazima umsujudie na kumwabudu — kwa kushiriki mambo ya uchawi/ushirikina.

Shetani anajulikana kama baba wa uongo na muuaji.(Yohana 8:44). Akikupa mapesa au fahari ya dunia hii, ujue amekutega. Amekutega umwabudu mungu mwingine kinyume na agizo la Mungu. Mungu alisema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” (Kutoka 20:3)

Ukiabudu miungu mingine maana yake unajitakia laana(Kum 28:15). Hivyo mali yoyote itakayokupeleka kwenye ibada nyingine ni laana hata kama inaonekana kama "baraka."

Hivyo ndugu yangu, kama unawaza kwenda kwa waganga ili upate utajiri, futilia mbali mawazo hayo. Shetani anakutega umsujudie halafu siku ya mwisho uangamie pamoja na yeye motoni.

cc: Nomadix
 
Kumbuka tena: shetani ni muuaji. Kabla hajakupa mali atakuambia na wewe uwe muuaji -uwatoe kafara ndugu zako au wazazi wako. Wauaji hawawezi kuurithi ufalme wa Mungu.
Ufunuo 21:8
"Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na madini ya kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili.”
 
Shetani akikupa mapesa ujue pia yataambatana na hofu, mateso, na huzuni.

Katika Mithali 10:22 tunaambiwa: "Baraka ya BWANA hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni.”

Ikiwa baraka za Mungu hazina huzuni, basi ni wazi kuna "baraka" nyingine ambazo huja na huzuni — hizo ni zile zisizotoka kwa Mungu, yaani za kishetani. Hivyo ukipata “mapesa” kutoka kwa shetani ujue yatakuja na kifurushi cha huzuni, hofu, ndoto mbaya na mateso. Unaweza usione mateso kwa sasa, lakini usisahau siku ile ya mwisho utatupwa jehanam na kuteseka milele na milele, motoni.
 
Hakuna pesa zinazopatikana kwa waganga, au njia za kishirikina, na kama zipo mwisho wake ni mbaya sana unatisha! Tamaa ndio imefanya watu kuamini kuna utajiri wa njia hio. Tamaa ya pesa ni mbaya sana, ndio chanzo cha mabaya.

1 Tim 6:10
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi

Tufanyeje basi:
1 Tim 6:11
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.(kwa theological reasoning)

Kama waganga na washirikina wengine wana uwezo wa kufanya mtu akapata pesa, kwanini basi wao wasijifanyie huo utaalamu wapate hizo pesa, badala yake wanataka uende wewe mteja wao utoe pesa, ni utapeli wa waziwazi kama utapeli mwingine.
 
Kuna watu wanakiri kwamba wamepata utajiri baada ya kupewa "dawa" na waganga wa kienyeji au wachawi. Kulingana na Maandiko, inawezekana shetani akakupa mali lakini lazima ukubali kumsujudia. Katika Luka 4:5–7 imeandikwa:
"Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."

Hii inaonyesha kuwa Shetani ana uwezo fulani wa kutoa "fahari" na "enzi" ya kidunia — mali, mapesa, heshima — lakini kwa masharti kwamba lazima umsujudie na kumwabudu — kwa kushiriki mambo ya uchawi/ushirikina.

Shetani anajulikana kama baba wa uongo na muuaji.(Yohana 8:44). Akikupa mapesa au fahari ya dunia hii, ujue amekutega. Amekutega umwabudu mungu mwingine kinyume na agizo la Mungu. Mungu alisema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” (Kutoka 20:3)

Ukiabudu miungu mingine maana yake unajitakia laana(Kum 28:15). Hivyo mali yoyote itakayokupeleka kwenye ibada nyingine ni laana hata kama inaonekana kama "baraka."

Hivyo ndugu yangu, kama unawaza kwenda kwa waganga ili upate utajiri, futilia mbali mawazo hayo. Shetani anakutega umsujudie halafu siku ya mwisho uangamie pamoja na yeye motoni.

cc: Nomadix
Na shetani nae anae da motoni...
 
Hakuna pesa zinazopatikana kwa waganga, au njia za kishirikina, na kama zipo mwisho wake ni mbaya sana unatisha! Tamaa ndio imefanya watu kuamini kuna utajiri wa njia hio. Tamaa ya pesa ni mbaya sana, ndio chanzo cha mabaya.

1 Tim 6:10
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi

Tufanyeje basi:
1 Tim 6:11
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.
Sasa mbona bible inatuchanganya tena.....tusipende fedha na nsio chanzo cha mambo mabaya. Lakini wakati huo huo inasema pesa ni ulinzi.
Mie hapa ndio ngachoka kabisa mwanawane
 
Kuna watu wanakiri kwamba wamepata utajiri baada ya kupewa "dawa" na waganga wa kienyeji au wachawi. Kulingana na Maandiko, inawezekana shetani akakupa mali lakini lazima ukubali kumsujudia. Katika Luka 4:5–7 imeandikwa:
"Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."

Hii inaonyesha kuwa Shetani ana uwezo fulani wa kutoa "fahari" na "enzi" ya kidunia — mali, mapesa, heshima — lakini kwa masharti kwamba lazima umsujudie na kumwabudu — kwa kushiriki mambo ya uchawi/ushirikina.

Shetani anajulikana kama baba wa uongo na muuaji.(Yohana 8:44). Akikupa mapesa au fahari ya dunia hii, ujue amekutega. Amekutega umwabudu mungu mwingine kinyume na agizo la Mungu. Mungu alisema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” (Kutoka 20:3)

Ukiabudu miungu mingine maana yake unajitakia laana(Kum 28:15). Hivyo mali yoyote itakayokupeleka kwenye ibada nyingine ni laana hata kama inaonekana kama "baraka."

Hivyo ndugu yangu, kama unawaza kwenda kwa waganga ili upate utajiri, futilia mbali mawazo hayo. Shetani anakutega umsujudie halafu siku ya mwisho uangamie pamoja na yeye motoni.

cc: Nomadix
Kiukweli nimesikitika sana kuona shetani ana ukwasi kiasi hicho cha kutajirisha watu na kuwapa maisha bora, tofauti na mungu tunaye hubiriwa kila siku ambapo waamini huombwa pesa kwaajili ya kuchangia kufanikisha kazi za huyo mungu.
Nimeanza kujiuliza vipi anayenadiwa ni muweza wa yote anashindwa kumudu operation cost ya shughuli zake ilihali shetani ambaye tunatangaziwa ni mdhaifu yeye ndiyo ashiriki kuwajaza watu mkwanja.
Kuna sehemu tumepigwa pakubwa sana.
 
Sasa mbona bible inatuchanganya tena.....tusipende fedha na nsio chanzo cha mambo mabaya. Lakini wakati huo huo inasema pesa ni ulinzi.
Mie hapa ndio ngachoka kabisa mwanawane
Pesa ni ulinzi imeandikwa wapi, mkuu?
 
Shetani akikupa mapesa ujue pia yataambatana na hofu, mateso, na huzuni.

Katika Mithali 10:22 tunaambiwa: "Baraka ya BWANA hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni.”

Ikiwa baraka za Mungu hazina huzuni, basi ni wazi kuna "baraka" nyingine ambazo huja na huzuni — hizo ni zile zisizotoka kwa Mungu, yaani za kishetani. Hivyo ukipata “mapesa” kutoka kwa shetani ujue yatakuja na kifurushi cha huzuni, hofu, ndoto mbaya na mateso. Unaweza usione mateso kwa sasa, lakini usisahau siku ile ya mwisho utatupwa jehanam na kuteseka milele na milele, motoni.
Uliwahi kumuona shetani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom