Je, unajua kwanini Biashara nyingi zinafeli hali yakuwa msimamizi ni mwenyewe mmiliki?

Masterplan

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
209
348
Kwanza kabisa, mapambano yaendelee siku ya kufanikiwa ipo tu, tusikate tamaa.

Mfano huu utajumuisha Biashara nyingi Sana, kwa hiyo wewe mwenyewe utakuwa unalinganisha na Biashara yako.

Naomba nianze na mfano wa Duka liwe ni la vitu ambavyo unaweza ukavitumia nyumbani kwa matumizi ya kila siku labda mfano Sukari, Mchele na Unga na vinginevyo.

Ipo hivi, wewe kama muuzaji, je, unajua lazima uwe unaheshimu Biashara yako?, kwa maana una uza lakini ndugu amekuja umempa labda soda au Chochote kile kwa bila malipo, je unajua unawezaje kurudisha faida ya kilichotoka?

Kutoa kitu kumpa ndugu ni vizur ila lazima uandike hiyo kama wewe umejikopesha ili ufanye ufanyavyo hiyo hela irudi dukani hapo na hiyo hela inatakiwa itoke kwenye vyanzo vingine tofauti na Dukani, ili iweze kuziba hiyo hasara ambayo ungeipata hapo, kwa sababu kesho tena utachukua vitu wewe vya kwako lakini umejiuliza ni kwa namna gani unaweza kurudisha hiyo faida uliyoitoa ili hesabu ya Duka iende Sawa.

Kwa hiyo lazima uandike pembeni kuwa umetoa kitu na lazima ukilipe, mwishoni tukianza kutafta faida ili tuende Sawa kabisa.

Ushawahi kujiuliza wewe unayeuza hapo inatakiwa ujilipe pia kuachana tu na kujikopesha

Najua itaonekama kama ajabu sana, lakini kila mwisho wa mwezi lazima uangalie kwenye ulichoingiza unajilipa vipi. Kwa sababu nadhani kabla hata ya kuanza Biashara, lazima uweke expectations zako utakachoingiza na hivyo inatakiwa uweke namna ya kujilipa, ukiwa unajua hilo lazima utakuwa serious Sana kwenye kazi maana mwisho wa mwezi lazima Faida ionekane na ya kujilipa wewe.

Kuna mwingine atasema Sasa najilipaje? kama ndio nimeanza si nitaua mtaji? Hapana.

Jiulize ungemuajiri mtu, lazima ungemlipa kwa hiyo biashara ingeendaje au ndio ungefunga?

Sawa je, hela nitakayojilipa nafanyia nini labda?

kama Biashara bado inahitaji mtaji fanya kujikopesha mwenyewe, yes Najua Kuna watu wataona ajabu Sana pia kujikopesha mwenyewe kama nilivyokuwa nimesema mwanzo, inatakiwa uwe na daftari lako ambalo utakuwa unaandika madeni ya kwako mwenyewe unayojikopesha hivyo ikifika Mda inatakiwa ujilipe mwenyewe.

Chukua mfano labda unajilipa
Tsh. 400,000/=, unaweza ukajikopesha
Tsh. 300,000/= kutoka kwenye hiyo laki nne uliyojilipa ili uongeze kwenye Biashara yako,ili ukiendelea na biashara yako uwe unajua unadaiwa 300,000/= mwisho WA siku faida itakuja na utajua unajidai kiasi gani then unarudisha kwanza Deni na unaendelea na Biashara.

Kwa hiyo kikubwa ni kuogopa Biashara yako, kamwe usitumie vitu vya kwenye Biashara hovyo kwa kuwa eti ni vyako, maana ukiishiwa utaanza kutafta mchawi Nani, kumbe wewe mwenyewe haukuweza kupanga namna nzuri ya kuweza kudeal na Biashara yako.

Alafu hii system itakusaidia pia kujua Biashara kama inalipa au hapana, Maana kitendo cha kutoa mshahara kuweka pembeni hali ya kuwa wewe ndio mmiliki ni njia nzuri hiyo itakayo kuonyesha kunafaida katika biashara yako au Hakuna.

Kama Kuna cha kuongezea unakaribishwa, kama hamna endelea kuchukua point mhimu.
 
Yaani biashara.. daaah ina mambo mengi sana ili ikubebe.. mengi sana.. hili lako ni thruthi katika 100.. daaah acha tu.. haya Asante kwa dini hili.
 
Yaani biashara.. daaah ina mambo mengi sana ili ikubebe.. mengi sana.. hili lako ni thruthi katika 100.. daaah acha tu.. haya Asante kwa dini hili.
Yes ni kwel, kwenye Biashara inatakiwa uzingatie mambo mengi Sana ili uweze kufanikiwa
 
Back
Top Bottom