Je, unaifahamu HONOR?

Je, unaifahamu HONOR?

HONOR Tanzania

New Member
Joined
Mar 31, 2026
Posts
4
Reaction score
6
Kwanza kwa niaba ya Familia nzima ya HONOR Tanzania (inatamkwa HONA) tunashukuru Timu ya 'Jamii Forums' kuturuhusu kuja huku kwaajili ya kuendeleza elimu na ubadilishanaji wa ujuzi na kuchangia mijadala ya matumizi ya teknolojia pamoja na ku-share changamoto mbalimbali zinazohusu vifaa vya mawasiliano; simu, tablets n.k.

Kwa ufupi kabisa HONOR ni kampuni ya kimataifa inayoongoza katika vifaa vinavyotumia teknolojia ya akili bandia/Akili mnemba (AI).

HONOR imejikita kubadilisha kabisa namna binadamu wanavyowasiliana na vifaa vyao, kwa kuunganisha mfumo wa AI na mazingira halisi yaani ecosystem.

HONOR ilianza mwaka 2013 ikitokea kampuni mama ya HUAWEI. Lakini la muhimu ni kwamba HONOR inalenga kumuwezesha kila mtu kufaidi teknolojia ya AI kupitia vifaa vyake ambavyo kwa sasa imeshaingia Tanzania na simu mbili "HONOR X6C", "HONOR Play 10" na hivi karibuni italeta matoleo mengine zaidi.

HONOR inasifika kwa ubora wa bidhaa zake huku bei yake ikiwa nafuu sana, mfano simu ya HONOR X6C ina uwezo wa kuhimili maji, na inaweza kuanguka mpaka umbali wa mita moja na nusu bila kupasuka. HONOR Tayari ipo Tanzania rasmi kuanzia mwezi Januari mwaka huu 2026.

Mengi zaidi yanakuja.
 
Biashara za kichina zmekaa kitapeli sana mtu anasema bei ndogo ya bidhaa bila kuweka actual digits...WINGA ENDELEA KUDADAVUA
 
Back
Top Bottom