Je, Unaiamini hadithi ya mnara wa Babeli?

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,508
99,299
Kwamba hapo mwanzo binadamu waliamua kujenga jengo kubwa na refu katika mji ule na kilele chake ni kifike mbinguni.

Kwamba Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyewachanganyia lugha watu hao, wakashindwa kuelewana na baadae walilazimika kuachana na mradi huo.

Nawasilisha🙏
 
Mkuu, unadhani haiwezekani au haipo kihistoria?

Je, unaamini kwamba Nuhu alijenga safina iliyotumika kuwahifadhi watu 8 dhidi ya Gharika?

Je, unaamini kwamba enzi ya Nuhu kabla ya Gharika ulimwengu ulikuwa na mabilioni ya watu, tena wenye akili ndefu (in Manara's voice) na teknolojia bora mno?

Je, unaamini kwamba Adamu na Hawa ndio wazazi wetu wa kwanza?

Je, unaamini kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi, na kwa muda wa siku sita akaratibu mazingira yake na kuwahuluku viumbe hai?

Je, unaamini kwamba Mungu yupo?

Sijui unanielewa???
 
Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu.

Biblia na maandiko yote ya kidini ni sawa na Hekaya za Abunuwasi, riwaya za Alfu Lela ulela, vitabu vya hadithi za kusadikika kama mbuzi anasoma, pepo za mizimu.View attachment 2943702
Screenshot_20231226-175555_1.jpg
View attachment 2943701
 
Kwani walishindwa kutumia sign language na kuendeleza libeneke ? Yaani wana technology ya kutengeneza skyscrapers bila technology ya steel kama ya sasa wanashindwa kutumia sign language ?

Kwahio walishindwa kujenga mnara sababu ya communication lakini wakaweza kuendelea na issue nyingine za kimaisha
 
Kwamba hapo mwanzo binadamu waliamua kujenga jengo kubwa na refu katika mji ule na kilele chake ni kifike mbinguni.

Kwamba Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyewachanganyia lugha watu hao, wakashindwa kuelewana na baadae walilazimika kuachana na mradi huo.

Nawasilisha🙏
Hadithi ya mnara ni upuuzi,

Imagine Mungu mjuzi wa yote alipelekewa taarifa kwamba watu wanajenga mnara wakufikie ndio akastuka.

Swali kuu ni kwamba, je mnara huo ulifikia urefu gani kiasi cha kutaka kufikia mbinguni kwa huyo jamaa,

Nauliza hivi kwamaana tunashuhudia rockets na ndege zikiruka kwa kimo kirefu na kwa hali ya kawaida tu mnara huo usingeweza hata kufikia kimo cha ndege.

Wagonjwa wa psychology tu ndio wanaweza kuichukulia hadithi hii kama ukweli.!!
 
Sio kwamba kitu usichokubali/usichokielewa hakiwezi kuwepo/kutendeka ..

Ni sawa na watu walioishi miaka 1000 iliyopita ungekuja na idea kama simu unaweza Kuongea na Mtu na sauti inasafiri hewani wangekataa kabisa haiwezekani
 
Kwamba hapo mwanzo binadamu waliamua kujenga jengo kubwa na refu katika mji ule na kilele chake ni kifike mbinguni.

Kwamba Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyewachanganyia lugha watu hao, wakashindwa kuelewana na baadae walilazimika kuachana na mradi huo.

Nawasilisha🙏
Kwahiyo Mungu aliogopa kwamba asipowachanganya lugha huo mnara utamfikia mbinguni?
 
Na wewe leta uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu sio kauli tu za kwenye biblia.

Otherwise wewe na hiyo biblia yako ni pumba tupu.
Niliwahi kukuuliza kwenye ule uzi wa Israeli vs Palestina iwapo unaamini kuna UWEZEKANO wa uwepo wa Mungu, ukasema Ndiyo.

Sasa hizi taarifa zingine kuhusu Babeli na zinginezo ni baadhi tu ya vithibitisho husika.

Labda nikuulize na hili leo.

Je, unadhani upo uwezekano wa wanadamu kuujenga mnara mrefu kwenda angani kama isemavyo Biblia?

NB: Sikuulizi iwapo mnara ulijengwa au la. Nazungumzia uwezekano kwa kipindi tajwa katika Biblia.

Jibu kisomi. Achana na hoja mkataa (dismissive arguments), maana hazisaidii kitu.
 
Ni uongo mkuu, hakuna mbingu angani.
Nashawishika kudhani kwamba maana ya uongo kwako ni kitu chochote usichojua au kilicho nje ya upeo wa uelewa wako.

Kwa mantiki hiyo, hata mavumbuzi na magunduzi mengi ya sayansi pengine yalikuwa uongo kwako hadi pale yalipogundulika.

Au, mwenzetu, huenda umewahi kuzurura huko angani kote ukathibitisha hakuna mbingu?

Ni upumbavu usioponyeka kujitia upumbavu kimakusudi.
 
Kwani walishindwa kutumia sign language na kuendeleza libeneke ? Yaani wana technology ya kutengeneza skyscrapers bila technology ya steel kama ya sasa wanashindwa kutumia sign language ?

Kwahio walishindwa kujenga mnara sababu ya communication lakini wakaweza kuendelea na issue nyingine za kimaisha
Hiyo ndiyo maana halisi ya ule msemo kwamba Mungu asemapo siyo, hakuna yeyote wa kupingana Naye.

Wakati wa vita vya pili vya dunia, Adolf Hilter alikuwa amekusudia kuwa mfalme wa dunia nzima.

Lakini alishindwa vibaya sana licha ya kuwa na jeshi imara, lenye ari na silaha madhubuti na za kisasa wakati huo.

Kwa nini? Kwa sababu Mungu alikuwa ameshatabiri kwamba himaya kubwa ya dunia baada ya Dola ya Rumi ingekuwa Marekani chini ya hisani ya upapa.

Hata China au Urusi tunayoiona leo ikielekea kama kuipiku Marekani, wote hao hawataweza kamwe kushinda.

Wataishia kuunda silaha nzito, za kutisha ambazo hazijawahi kuwepo ulimwenguni, lakini mwisho wa siku watatokomea kwa fedheha kama Adolf Hitler.

Marekani atabaki kuwa kinara ili kutimiza unabii pamoja na hisani wake Mvatikano.

Marekani yupo kuutekeleza mpango wa Mungu kwa mema au kwa mabaya hadi mwisho wa wakati.

Na anafanya hivyo vizuri sana ama anajua au hajui.

Mungu asemapo Ndiyo, hakuna mwanadamu wa kumpinga!
 
Hiyo ndiyo maana halisi ya ule msemo kwamba Mungu asemapo siyo, hakuna yeyote wa kupingana Naye.

Wakati wa vita vya pili vya dunia, Adolf Hilter alikuwa amekusudia kuwa mfalme wa dunia nzima.

Lakini alishindwa vibaya sana licha ya kuwa na jeshi imara, lenye ari na silaha madhubuti na za kisasa wakati huo.

Kwa nini? Kwa sababu Mungu alikuwa ameshatabiri kwamba himaya kubwa ya dunia baada ya Dola ya Rumi ingekuwa Marekani chini ya hisani ya upapa.

Hata China au Urusi tunayoiona leo ikielekea kama kuipiku Marekani, wote hao hawataweza kamwe kushinda.

Wataishia kuunda silaha nzito, za kutisha ambazo hazijawahi kuwepo ulimwenguni, lakini mwisho wa siku watatokomea kwa fedheha kama Adolf Hitler.

Marekani atabaki kuwa kinara ili kutimiza unabii pamoja na hisani wake Mvatikano.

Marekani yupo kutekeleza mpango wa Mungu kwa mema au kwa mabaya hadi mwisho wa wakati.
Eti Mungu anatumia USA kukamilisha maneno yake, hizi ni chai, kikubwa ni kuamini tu ilimradi siku zisonge.
 
Hadithi ya mnara ni upuuzi,

Imagine Mungu mjuzi wa yote alipelekewa taarifa kwamba watu wanajenga mnara wakufikie ndio akastuka.

Swali kuu ni kwamba, je mnara huo ulifikia urefu gani kiasi cha kutaka kufikia mbinguni kwa huyo jamaa,

Nauliza hivi kwamaana tunashuhudia rockets na ndege zikiruka kwa kimo kirefu na kwa hali ya kawaida tu mnara huo usingeweza hata kufikia kimo cha ndege.

Wagonjwa wa psychology tu ndio wanaweza kuichukulia hadithi hii kama ukweli.!!
Mkuu, namna yako ya kuisoma Biblia ni ya mashaka sana.

Hebu nukuu andiko lako ili watu wakusaidie kufafanua; vinginevyo utaendelea na ujinga wako katikati ya bahari ya maarifa.
 
Back
Top Bottom