Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,717
- 13,443
Sijui ni kwanini mnakuwa na mawazo kuwa elimu ni kitu cha maana kwa kiasi hicho kwenye maisha ya binadamu wakati hiyo elimu imetoka kwenye mfumo wa kufikiri wa binadamu halafu binadamu asiekuwa na hiyo elimu anaonekana wa ajabu
Elimu,kwa namna ninavyojua mimi elimu ni moja kati ya "zimwi" linalopendwa sana na watu ambalo limewanyang'anya uwezo wao wa kawaida wa kutafakari mambo
Nani amekudanganya Ulaya na Marekani hakuna uchawi?
Danganyaneni wenyewe lakini sio mimi!
Msaada please;Shida moja hapa ni kwamba watu wanachanganya uchawi, ulozi, mazingaombwe uganga wa kienyeji! hivi vyote ni vitu vinavyofanana lakini pia vikitofautiana
Msaada please;
Nisaidie tofauti kati ya uchawi, ulozi na uganga wa kienyeji.
Msaada please;
Nisaidie tofauti kati ya uchawi, ulozi na uganga wa kienyeji.
Iwe vyovyote iwavyo bado elimu ni tatizo kwa jamii zetuHapo kwenye elimu ni zimwi, una point lakini ni kama umeshindwa kuiweka bayana pointi yako, but I can feel it, you have something there meaningfully, labda ulitaka kuzungumzia mifumo mibovu ya elimu,labda, mifumo inayokaririsha tu watu na kutotoa fursa ya watu kuweza kufikiri, mifumo ya elimu ambayo inapima ufanisi wa elimu kwa kuangalia ni wangapi wamepata grade gani, bila kujali wanaelewa nini, labda unamaanisha hicho, lakini ukisema tu "elimu" ni zimwi, unakuwa umegeneralize sana.
Unaweza kuishi Mwanza lakini bado ukawa hujui kama kuna watu wanaishi kwa mlo mmoja na ukaja kuambia ukadhani ni hadithi tu!
Mkuu sijui ....
Lakini kuna ambavyo imeshindwa lakini nina hakika vipo!
Sasa mbona una equivocate kitu ambacho hata hujui?
Mtu anakurupuka na kudai uchawi haupo kwa sababu sayansi imeshindwa kuthibitisha wakati anajua kabisa sayansi hiyo hiyo inakiri kuna isiyoweza kuyajua
Watu wengine wa ajabu sana!
Ulichoandika hapa ni a logical non-sequitur. You are concluding Z from A while A and Z have no logical connection.
Ni kama vile umeambiwa "Gari hili lililo Dar kuna barabara nyingine haliwezi kupita, kutokana na uimara wake". Halafu ukalikuta gari lile Kibaha na kusema "haiwezekani hili gari liwe Kibaha kwa sababu tushaambiwa lilivyokuwa Dar kuna barabara nyingine haliwezi kupita". Bila hata kuuliza barabara hizo lisiloweza kupita ni zipi na kutoka Dar mpaka Kibaha kuna barabara gani!
Kwamba sayansi kuna mengine imeshindwa kuthibitisha haina maana kwamba isitumike katika kupima uwezekano wa kimantiki wa uchawi kuwapo.
Sayansi pia imeshindwa kuthibitisha kwamba kuna kiumbe mwenye macho matatu anayekaa juu ya mlima Kilimanjaro na ku control ulimwengu wote.
Je, hilo linamaanisha kwamba kiumbe huyo yupo? Kwa sababu tu sayansi imekiri kuwa kuna mengine haijayajua?
Unavaa kiatu kimoja na kuacha kuvaa kingine makusudi
Tatizo langu mimi sio watu kuitumia sayansi kupimia mambo ikiwemo na uchawi
Tatizo langu ni kuhitimisha kuwa kitu fulani hakipo kwasababu tu sayansi imeshindwa kukithibitisha
Najua kuwa gari linaweza kupitia barabara nyingine kufika linakokwenda kwani barabara ambayo lilitarajiwa kupitia imeshindwa kuhimili uzito wa gari
Kwa upande mwingine tunaweza kusema gari ni uchawi kwa mfano na barabara ni kile ambacho kinaweza kuthibitisha uwepo wa uchawi,barabara ya kwanza ambayo tulitegemea gari kupita [sayansi] gari [uchawi] limeshindwa kupita,lakini hiyo haimaanishi gari hilo haliwezi kupitia njia nyingine kufika huko linakotaka kwenda
Kwa maana hiyo basi tunaweza kuthibitisha uwepo wa uchawi bila kutumia sayansi kwakuwa uchawi upo na tunaona matokeo ya uwepo wake!
Unathibitisha uchawi upo au haupo kwa kutumia nini?
Kwa kushuhudia matokeo ya uchawi ..!!
Kushuhudia kwako kunajua yote au kuna mengine hakuyajui?
Yote yapi?
Yanayohusiana na nini?
Yote yaliyopo, yanayohusiana na yote.