Je umetolewa kazini? Fanya hivi ili ufanikiwe mtaani

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,203
157,375
Kwa wale rafiki zangu 10,000 walio achishwa kazi na wale watakao endelea kuachishwa hizi ni mbinu saba zitakazo kufanya uendelee kuwa imara kiuchumi.
1. Kubaliana na khali halisi , wala usione aibu na kuanza kujificha kwani kwa kufanya hivi utaingia kwenye mfadhaiko, kupoteza fursa na kuhatarisha afya yako
2. Pata mawazo kutoka kwa watu wako wa karibu waliokwisha kuachishwa kazi lakini wakaanza maisha upya na kufanikiwa tena.
3. Haraka sana jenga malengo mapya na yafanyie kazi kwa haraka pia, ili kujenga fursa ya kujiingizia pesa kwa haraka kabla hujatumia mafao yako yote.
4. Ikiwezekana tumia uzoefu ulioupata kutoka katika ajira uliyoachishwa, uhusiano, na utaalamu kujenga fursa mpya ya kukupatia pesa.
5. Kwa haraka sana watafute wadeni wako , ongea nao hali yako halisi ili muweze kukubaliana namna mpya ya kulipana kwani dawa pekee ya deni ni kulipa, ikiwezekana uza mali zako za anasa na zile usizo zihitaji kwa wakati wote kulipa madeni yako pamoja na kujenga mtaji.
6. Kwa haraka sana punguza gharama zako za kimaisha , ikiwekana hama makaazi uliyopanga kama ni ghali sana, jizoeshe kuishi maisha ya chini kabisa huku ukijenga namna mpya ya kupata pesa, hii itakuwesha kutumia mafao yako kwa muda mrefu.
7. Usikimbilie kutumia mafao yako yote kwa shughuli moja pekee ya kibiashara , wala kukimbilia kufanya biashara yeyote mpya pasipo kufanya uchunguzi wa kutosha kwani utaanguka mara moja na kupoteza pesa zako zote.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri,naamini ukifanyiwa kazi itakuwa tiba tosha ki psychology.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa wale ambao umri haujakaribia machweo ni wakati mzuri wa kufufua kipaji chako na kukifanyia kazi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom