Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,986
- 168,508
Katika pita pita zangu leo, nilikumbana na majarida mbalimbali yaliyokuwa yakiongelea juu ya umuhimu wa kumsomea mtoto kitabu kila siku kwa dakika 20 tuu. mhhhhh! well, mi najua kusoma leo infact napenda kweli kusoma vitabu lakini sikumbuki kama nilishawahi kusomewa kitabu chochote na wazazi wangu LOL. Nisieleweke vibaya, wazazi wengi hufanyia watoto wao mambo mengi ili kuendelea kimaisha, sio lazima iwe kusomewa kitabu tuu. Well, labda kwasababu nilikulia vichochoroni LOL ila seriously, sijawahi kusikia mtoto yoyote wakiswahili akijisifu hata siku moja kwamba alisomewa vitabu na wazazi wake akiwa mdogo LOL not like its a big deal or anything. Well, basi, tafiti nyingi zimekuwa zikisisitiza wazazi umuhimu wa wazazi kusomea mtoto/watoto wao kitabu/vitabu toka wakiwa na umri wa miezi mitatu na kuendelea.
Nadhani kwa akina mama na baba wa kizazi kimpya hili jambo linabidi liwe "PRIORITY" katika familia na katika kukuza watoto wetu.
Tena sikuhizi kwajinsi watu wanavyopenda maendeleo makubwa haswa katika kuwapatia watoto elimu haina budi kuanza hiyo elimu kutokea nyumbani kwa kusomea watoto wetu vitabu.
Tafiti zinaonyesha kwamba; mtoto anayejua kusoma mapema haswa angali katika umri mdogo hata mafanikio yake katika kazi za kishule/kimasomo huwa nzuri. Pia kusoma vitabu ama kumsomea mtoto kitabu humsaidia mtoto kupanua upeo wake wa kufikiri (imagination) na hata kuweza kumsaidia kufungua milango ya kila aina katika hii dunia (speaking of empowering a child katika kukuza vipaji vyake). Hata hivyo, kumsomea mtoto kitabu ama vitabu ni njia moja wapo inayoweza kumsaidia mtoto kuweza kuongea na kuzielezea hisia zake kutokana na ukaribu unajijenga kati ya mzazi na mtoto wakati wanaposoma kitabu/vitabu pamoja.
Well, inaeleweka kwamba maisha ni mchaka mchaka, uwe Tanzania ambapo unaweza kuafford wasaidizi wa ndani na nje ya njumba ama uwe nchi za nnje ambapo huwezi kuafford wasaidizi. Kitu cha kuzingatia ni kuspare kamuda kadogo ili kuweza kuspend time na mtoto/watoto wako. Tafiti zinaonyesha kwamba, Dakika ishirini tuu za kukaa karibu na kumsomea mtoto wako kitabu husaidia mzazi/wazazi; kubond/kuwa na uhusiano wa karibu na mtoto/watoto wao emotionally na haswa kujenga urafiki wa karibu sana. Hivyo visingizio vya nimechoka mara sijui nini inabidi vife LOL.
Anyways, je utaanzaje ama utafanyaje ili kuhakikisha unasoma kitabu/vitabu na watoto wako? Au utafanyaje ili kusoma na mtoto/watoto wako iwe ni Priority ya kwanza katika Familia yako? Well...,Kwanza kabisa cha kufanya ni KUZIMA TV na MACOMPUTA yaliyoko ndani ya nyumba. Hizi ni destruction kubwa kwa watoto na wazazi. Pia tafiti zinaonyesha ijapokuwa kuna vitu kadhaa mtoto anaweza kujifunza kupitia TELEVISION, kideo husababisha watoto kuwa na short attention span.
Hivyo basi, cha kufanya ili kuweza kutekeleza project hii ya kumsomea mtoto wako kila siku kwa dakika ISHIRINI (20) tuu, inabidi uset mda wa watoto wanapoweza kuangalia TV na isiwe zaidi ya lisaa limoja kwa siku. Pia vipindi wanavyoangalia viwe zaidi ni vya kuwaelemisha na kusaidia kukuza akili zao. (Hint hint...sio music videos na reality shows).
Cha pili, watoto wanajifunza kwa kufuata mfano wa wazazi/wakubwa. Hivyo basi, hata wewe kama mzazi inabidi upunguze muda wako wa kuangalia TV na badala yake uchukue hata gazeti ama kitabu chochote usome kama njia moja wapo ya mapunziko (kupumzisha akili). Hakikisha nyumba yako imezungukwa na vitabu. Hii itamsaidia mtoto kujua kwamba kusoma ni muhimu. Pia ikiwezekana, pitia maktaba/library na tafuta vitabu vitakavyo mvutia mtoto kusoma i.e. watoto wengi wanapenda vitabu vyenye picha kwasababu vinawasaidia kufuatilia stori vizuri na kuimagine. Ama muulize mtoto wako ni vitabu gani anapendelea kuangalia. Kumbuka kutomlazimisha mtoto kusoma kitabu though, ndo maana kama hukuanza toka mtoto akiwa na miezi midogo basi inabidi uende nae taratibu huku akikuwa. Hutaki mtoto aone kama ni kazi kusoma kitabu bali unataka aone ni enjoyment kusoma kitabu.Pia kitu kingine kinachosaidia mzazi anapomsomea ama anaposoma kitabu na mtoto wake ni kwamba, mzazi anaweza kugundua mapema dalili zozote za kama mtoto wake anatatizo la kusoma ama kuandika na hivyo kuweza kumsaidia mtoto mapema kabla hajaenda shule na kuanza kupata tabu na kuogopa kuchekwa na wenzake. Then mzazi anashangaa ahhh mtoto huyu hapendi shule ama hapendi kusoma....well, je ULIMFUNDISHA ama KUMSAIDIA KUSOMA WAKATI ANGALI MDOGO????
NIJUKUMU LA KILA MZAZI KUHAKIKISHA KWAMBA HASUBIRI MWALIMU SHULENI NDO AKAWA MFANO NA TEGEMEO LA ELIMU NZURI KWA MTOTO WAKE!





