The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,100
- 13,698
Pamoja na uzee wangu, wanangu, nina swali dogo. Je umewahi kumpenda mtu, ukamsifu, ukamtukuza, ukajikomba hata kujidhalilisha halafu ukamchukia? Nauliza hivi kutokana na ninayoshuhudia kuhusu wapendwa wanene wetu. Wanasifiwa hata pale wanapopaswa kulaumiwa.Wanadanganywa hadi wanadanganyika. Je tufanye nini kuwasaidia wazinduke usingizini? Nani alijua kuwa January Makamba na Nape Nnauye wangemsengenya na kumkandia marehemu Magufuli? Je walimpenda hadi wakamchukia?