Je Uko Huru?? Jitathmini.....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,802
Reaction score
43,205
Habari za siku ya jumapili wapendwa,

Nahisi maelezo yatakuwa marefu ila najitahidi kuyafupisha. Nimekuwa nikijitathmini na kulinganisha na uhalisia wa maisha.... nikagundua vingi tuu kuhusu uhuru wa mwanadamu hata mimi Kasie.

Tangu ulipozaliwa hadi una miaka 18 (kwa waliolelewa chini ya wazazi au walezi ) hapo hawakuwa huru kwa maana ya kuwa unafanya kile anachopenda na kusema mzazi au mlezi hata kama anakosea au si sawa au hukipendi. Hii inaanzia kwenye kuchaguliwa nguo za kuvaa chakula gani ule asubuhi mchana na jioni, uende wapi na wapi kutembea au kupumzika, likizo ufanye nini, hata marafiki saa ingine mzazi au mlezi aliingialia kati. Kiufupi unakuwa huna uhuru wa kufanya unachopenda au unachotamani.

Kwa sie waafrika baada ya miaka 18 ni wachache sana wanapata uhuru wa kufanya yao kuishi wanavotaka wao kwasababu bado wanakuwa wanaomtegemea mzazi kwa kiasi kikubwa. Inapofikia unaanza kazi kuna baadhi huapata uhuru wa maisha yao kwa kuishi watakavyo na wapendanao japo kuna baadhi huendelea kuwa watumwa wa familia au kutokuwa huru kwa kufanya na kutenda wasemacho wazazi na familia aliyokuwa nayo sisemi kuwa hivi ni vibaya hapana. Hapa naongelea je uko huru?

Au kuwa huru ni nini? Naomba mtu anisaidie kuelezea maana ya kuwa huru...

Hapohapo kuna baadhi akishapata kazi anaoa au anaolewa hapa anaanza kuishi kwa matakwa ya mpenzi wake na akishapata watoto anaishi kwa matakwa ya watoto wakwe wifi shemeji n.k. jiulize tena uko huru? Sisemi uache familia yako?

Ni hivi, kama katika maisha yako umefanikiwa kufanya matakwa ya wazazi huku ukapata wasaa wa kufanya matakwa yako basi ulikuwa huru. Hapa yaweza kuwa unapenda bustani au kufuga na uliweza kufanya haya chini ya himaya ya wazazi basi ulikuwa huru kwa kiasi. Kama umefanikiwa kuwa na maisha yako unajitegemea mwenyewe na bado unatimiza matakwa yako binafsi na unatimiza matakwa ya wazazi au walezi wako na mpenzi wako mke au mume na watoto basi uko huru.

Ukiona hadi leo unaishi maisha yako na familia au hata kama huna familia na hujafanikiwa kufanya au kutimiza matakwa yako binafsi kama kujiendeleza kieleimu kufuga au kupima kisasa kama unapenda hivyo basi ujue hauko huru. (uhuru bunafsi)

Na ukiona hata ukitaka kwenda short call ni hadi upate ruhusa au ushauri wa mtu ujue wewe ndo uko gerezani kabisa.

Poleni kwa kuwachosha na maelezo mengii. Kwa waliolelewa mtanisaidia kuwaelewesha wengine tafadhali.

Muwe huru kuchangia na mchango wako utaonesha kama uko huru au laah. Watch out hehehehee.

Jumapili njema.

Kasie Mahaba bin Nyonda-ake Mtufudenge.

UPDATE:


Mkiwa mnaendelea kutafakari na kuchangia burudikeni na jiwimbo hilo la Lucky Dube...

Again Kasie Mahaba, Mahabat wake mtu....
 
mie pia siko huru! maana sina njaa lakini nipo jikon napika ili familia ile... sijui nasaidiwaje hapo! [HASHTAG]#naanzishaMaandamano[/HASHTAG]
 
utakuwaje huru sasa? we are controlled by power from outside kwa hiyo kama mimi nimeletwa kwa kusudi la Mungu hapa duniani nitaishi kwa mapenzi yake na nisipotimiza aliniambia sitoingia katika ufalme wake naweza kusema kuwa huru kabisa kabisa hiyo kitu hakuna na haipo na haitokuwepo
 
Hakuna msamiati wa uhuru katika maisha,tusidanganyane.
Kuna sheria za nchi,dini,moral ethics,utumishi sijui nk mavazi daima zinachukua uhuru wetu. Mfano mimi napenda sana kutovaa nguo kabisa lakini nathubutuje? Uchumi pia unalimit uhuru wetu,sipendi kabisa kuendesha vitz lakini uwezo umekomea hapo,sipendi kuishi uswazi ila hali sasa! Kwa hiyo dunia haitoi huo uhuru tunaousema,kwangu mimi ni imaginary tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh hakuna uhuru usio na mipaka
Unaweza kuwa na uhuru wa jambo moja au mawili ila sio yooote maishani maana hapo utagusa maisha ya wengine wasiwe nao huru
Kwahiyo upo Ila kiasi sio asilimia
maishani
 
Maisha ni mipaka .Huwezi kwenda hovyo hovyo tu kwa kisingizio cha uhuru.
Mipaka inaanza kwa sheria za kiroho.
Sheria za nchi .
Taratibu za ndoa zinakufanya uwe kwenye mipaka.
Sheria za ofisini zinakufanya uwe ndani ya mipaka.
Labda uhamue tu kwa utashi wako uchupe mipaka ndio utakuwa huru.
 
Haiwezekani kuwa huru kabisa.
Hata uhuru tunaohisi tunao ni kujiliwaza tu.

Kwa mfano mtu hudhani akijitegemea bila mpenzi, mbali na wazazi na bila watoto basi yuko huru anasahau kwamba bado unatawaliwa na sheria za kazini kwenu kwa hiyo kuna mambo huweZi fanya.

Hata kama huna kazi umejiajiri bado miongozo ya kijasiriamali na kanuni za fedha zitakunyima uhuru fulani.

Hata ukiwa huna hayo yote bado unabamwa na kanuni za kiimani(labda dini) au kanuni za kimazingira na kisayansi mf huwezi kuwa huru kukimbia kwa kasi ya mwanga, huwezi kupaa hata kama ungetamani.
 
Hiii anzishia thread yake
 
Huwezi kuwa huru hadi ukawa huru, kila ukiona upo huru lazima kuna pingamizi la huo uhuru wako. I'd like to bang as many pretty chicks out there but uhuru huo sina due to morals za kidini, I'd like to drive the most expensive car out there but financial constraints won't let me.

Ndio maana hata mkulu akasema you've got freedom but not to that extent.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…