Je, ukichukua Vitu hivi katika Ndege pale ikitua tu unakoenda unakuwa Umeiba au Umechukua kile ambacho Umekilipia katika Nauli?

hizo headphone unaondoka nazo ni original?!
Hazina kiwango cha hivyo ndio maana zinakuwa disposable. Jamaa tulitua KIA wakashuka mabeberu ndio tukapelekwa JKIA. Yaani alizizoa zaidi ya 10 na hawakummaind kabisa. Wanazikusanya zinaendwa tupwa tu.
 
Mmh, achana na mambo ya kwenye ndege hayo maana mi ndo kwanza nayasikia leo na huwa sijui hata kunafananaje huko ndani ya mwewe (ndege)

Mi babaangu alilazwa I.C.U Muhimbili.. Kwanzia sabuni, Vikombe, Beseni na vikorokoro vyote walivyokuwa anahudumiwa nazo wodini niliogopa kuvibeba japo nilivilipia, mi nilijua ukinunua vinakuwa mali ya hospitali. :p :p Ushamba mzigo.
 
Kwa kuwa Niko kwenye sekta hii na kupanda ndege mara nyingi ni kuwa hivyo vitu ni lazima uviache hapohapo
Headphones unaitupia kwenye seat ndio maana wanakusanya ili itumike tena na tena
Hata taulo huwa zinafuliwa tena na kutumika
Kwa hiyo kuchukua ni wizi kwani haihesabiki kama mali yako bali ni service tu
 
Unafanya haya mashirika ya safari za ndani ya nchi? Au yale makubwa ya safari za kimataifa?
 
Si umeshaambiwa kuwa wamevilipia katika ile Hela yao ya Nauli au?
Nilikuwa namshangaa aliyesema zinakusanywa na kutumika tena, wakati zile unapewa unatoa kwenye karatasi mwenyewe. Safari ikiisha wanazidispose tu. Labda inategemea na shirika la ndege husika. Kama zile za KLM hata ukichukua sio imara sana hata mziki zinazotoa sio quality nzuri
 
Asikudanganye huyo Mkuu yupo hapo Ubungo Bus Terminal kama Mvizia Wateja ( Wasafiri ) wa safari za kwenda Mikoani na Vijini nchini Tanzania.

Kupanda ndege au kufanya kazi sekta hii iwe supplier wa chochote
Sio sifa za kutafuta bali tunapeana mawili
Umeuliza swali umepata jibu kuwa huo ni wizi that’s all mengine yaache
 
Nilikuwa namshangaa aliyesema zinakusanywa na kutumika tena, wakati zile unapewa unatoa kwenye karatasi mwenyewe. Safari ikiisha wanazidispose tu. Labda inategemea na shirika la ndege husika. Kama zile za KLM hata ukichukua sio imara sana hata mziki zinazotoa sio quality nzuri

Usishangae kwani hizo headphones na vifaa vyote unavyopewa kasoro mswaki na dawa vingine huwa vinakusanywa na vina safishwa na vinakuwa reused tena hiyo ipo kwenye ndege za kimataifa ila kwa nyumbani sijui
 
Mbona Maelezo yako haya yanaonyesha na Wewe ni kama Mimi tu ambaye sijawahi Kupanda Ndege Mkuu? Anayezipanda huwa hana maneno hivi.
 
Nikipanda Ndege ( japo niweke tu wazi sijawahi Kupanda zaidi ya kuziona tu Angani zikipaa ) halafu nikitua kule niendako iwe ni hapa Afrika Kwetu au Mamtoni ( Ulaya ) kisha nikashuka na ile Mito ya Kuegemea iliyoko katika Siti, nikabeba pia na Headphones, Mataulo, Sabuni, Toilet Paper na Vinywaji kadhaa GENTAMYCINE nakuwa ninaiba au nabeba vile ambavyo nimevilipia katika Nauli?
enzi hizo nipo nairobi tulikuwa tunaenda kwenye dampo linaitwa Dandora hapo ndege zote ndo zilikuwa zinaleta uchafu wa siku husika nlikuwa naokota material zimetoka ulaya, arabuni,asia nk. huwa wanatupa
 
Kwahiyo Wewe ni Chokoraa au?
 
Back
Top Bottom