Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Kuna mambo mengine ukiyatazama kwa jicho la tatu hakika unabaini kuwa kuna ujanja ujanja na utapeli mwingi kwenye siasa za nchi hii hususan siasa ndani ya vyama vya upinzani.
Tulijinasibu kwa mbwembwe kuu kwamba UKAWA ipo kwa maslahi mapana ya Taifa hili na kuna laghai mmoja ambaye mara zote alikuwa anasema kuwa UKAWA ipo kwa maslahi mapana ya Mama Tanzania. Sote tulishuhudia kuwa wakati wa kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2015, vikao kadhaa vya viongozi wa UKAWA vilikuwa vinafanyika huku wakitoa matamko kadhaa pindi walipoona kuwa mpenyo wao wa kwenda Magogoni unazibwa na CCM. Sisi Bendera fuata upepo tukasema naam sasa ni dhahiri kwamba Upinzani wa Tanzania umekomaa na hakika utawala wa CCM umefika ukingoni.
Baada ya uchaguzi wa Oktoba, hatujashuhudia tena kikao chochote cha viongozi wa UKAWA. Tumachokishuhudia ni kwa CHADEMA kutoa matamko na kujivisha joho la UKAWA kwa upande wa Tanzania Bara. Kule visiwani, CUF imeonekana kusimama kwa miguu yake kwani viongozi wa UKAWA wanaonekana kutokuwa interested na siasa za Zanzibar.
Ni siku nne sasa zimebaki ili uchaguzi wa marudio ufanyike Visiwani. Si Lowasa ambaye anajiita kiongozi Mkuu wa UKAWA aliyediriki kutamka kwa kinywa chake kuhamasisha viongozi wenzake kuungana kuisaidia CUF Zanzibar. CUF wamebaki yatima baada ya mama yao UKAWA kuacha misingi yake na kugeukia UKAHABA wa kisiasa. Ndipo ninapojiuliza, je UKAWA ilikuwa ni kwa maslahi ya CHADEMA na Tanzania Bara tu na si kwa CUF na Zanzibar?