Je, ujauzito upo au haupo hapa?

Je, ujauzito upo au haupo hapa?

yope

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
368
Reaction score
697
Wakuu kama kichwa kinavyojieleza yapi ni majibu sahihi ya hiki kipimo cha UPT , Kwa sababu naona mstari mmoja umekolea na mwingine ni hafifu kidogo.

IMG_20211010_072128_3.jpg
 
Wakuu kama kichwa kinavyojieleza yapi ni majibu sahihi ya hiki kipimo cha UPT , Kwa sababu naona mstari mmoja umekolea na mwingine ni hafifu kidogo.View attachment 1969928

1: Cha kwanza ni kujua karatasi yako ya kitendea kazi imeelekeza usome majibu ndani ya muda gani? Kama nakumbuka vyema ni ndani ya dakika 20. (Naomba urejee kwenye karatasi ya maelekezo).

Je, picha imepigwa baada ya muda gani?

Kama ni ndani ya muda tajwa basi ni mjamzito.

Kama ni nje ya muda tajwa basi kuna walakini. Irudiwe

2: Mkojo ni wa nani?
Maana kuna matatizo kwa akina baba pia huweza kuleta majibu kama hayo (hivyo ni muhimu kusema mkojo ulitokana na nani?)
 
Back
Top Bottom