Je, ujauzito ni hatari kuliko UKIMWI?

Jeune Kims

Member
Sep 8, 2021
5
0
Ni kweli kwasababu ya utandawazi, mambo yanabadilika. Namna za kuishi pia zinabadilika, mapokeo nayo kutoka kizazi hadi kizazi yanabadilika. Je hekima imesafiri? Au amepotea njia? Au maarifa ya utandawazi yamebadilisha maana ya hekima?

Je ni kweli kwa kizazi hiki mimba imekua ni ugonjwa hatari kuliko UKIMWI? au magonjwa mengine ya zinaa?

Nimebahatika kukutana na vijana wengi na tunapozungumzia swala la mahusiano wengi huonekana kuogopa kumpa mwanamke au kupata mimba. Lakini hayupo anaeogopa kupata magonjwa ya zinaa.

UKIMWI upo, Kisonono upo, kubwa zaidi tunalalamika fungus na uti haziishi lakini umejipanga je kukwepa magonjwa ya ngono? Je hakuna namna ya kujikinga na haya magonjwa? Kama ipo kwanini tunaipuuzia? Au sauti za wanaharakati wa maswala la afya hazitoshi? Basi sauti yangu iwafikie afya ya uzazi (reproductive health) sio swala la kupuuzia. Jitunze wewe ili uweze kutunza ndoto na malengo yako pia.
 
Back
Top Bottom