“Kuanzia sasa hivi mara moja, Jeshi la Wanamaji la Marekani — lililo bora zaidi duniani — litaanza mchakato wa kuzuia (blockade) meli zote zinazojaribu kuingia au kutoka katika Mlango wa Bahari wa Hormuz,” aliandika Rais wa Marekani Donald Trump kwenye Truth Social.
Nikimnukuu:
“Kwa hiyo, kama mnavyoona, mkutano ulienda vizuri, mambo mengi yalikubaliwa, lakini jambo muhimu zaidi — suala la nyuklia — halikukubaliwa.
Kuanzia sasa mara moja, Jeshi la Wanamaji la Marekani, lililo bora zaidi duniani, litaanza mchakato wa kuzuia (blockade) meli zote zinazojaribu kuingia au kutoka katika Mlango wa Bahari wa Hormuz.
Wakati fulani, tutafikia hali ya ‘kila mtu anaweza kuingia, kila mtu anaweza kutoka,’ lakini Iran haijaruhusu hilo kwa kudai tu kwamba ‘huenda kuna bomu la baharini mahali fulani,’ jambo ambalo hakuna anayelijua isipokuwa wao.
Hii ni unyang’anyi wa kimataifa, na viongozi wa nchi, hasa wa Marekani, hawatakubali kunyanyaswa.
Nimeagiza pia jeshi letu la wanamaji kufuatilia na kuzuia kila meli katika maji ya kimataifa ambayo imelipa tozo kwa Iran. Hakuna atakayelipa tozo haramu atakayekuwa salama baharini.
Pia tutaanza kuharibu mabomu ya baharini ambayo Iran imeweka katika njia hiyo.
Muirani yeyote atakayefyatua risasi dhidi yetu au dhidi ya meli za kiraia atakabiliwa na nguvu kali sana.
Iran inajua, kuliko mtu yeyote, namna ya kumaliza hali hii ambayo tayari imeiharibu nchi yao. Jeshi lao la majini halipo, jeshi la anga halipo, ulinzi wa anga na rada zao hazina maana, na viongozi wao wengi wamekufa kutokana na azma yao ya nyuklia.
Zuio hili (blockade) litaanza muda si mrefu. Nchi nyingine pia zitahusika.
Iran haitaruhusiwa kufaidika na kitendo hiki kisicho halali cha unyang’anyi. Wanataka pesa, na zaidi wanataka nyuklia.
Zaidi ya hayo, wakati ufaao utakapofika, sisi tuko tayari kabisa kijeshi, na jeshi letu litakamilisha kilichobaki dhidi ya Iran.”