Je, Tutafika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Tutafika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkereketwa_Huyu, May 19, 2012.

 1. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280
  Jana ilitimu siku ya sita (6) mimi na jamaa yangu toka Arusha tukihangaishwa na watu wa mali asili. Jamaa yangu kaja hapa Dar kusajili kampuni yake ya utalii, na kule Arusha aliambiwa nani wa kumuona kipindi akifika hapa Dar. Alipofika hapa, nikampeleka kwenye idara alizotakiwa kwenda kama vile TRA, na sehemu nyingine nyingi tu pamoja na wizarani kwenyewe.

  Cha kushangaza kila sehemu tuliyokwenda tunaambiwa nenda kamwone fulani yeye ndiye anayehusika na hivyo vitu. Utakwenda kumwona huyo mtu atakuambia hapana, si mimi mwenyewe anayeshughulika na hivyo vitu yuko ghorofa fulani, yaani ni usumbufu usio na sababu.

  Huyu jamaa yangu anafungua kampuni ya kitalii na ana watalii zaidi ya 300 waliojiandikisha kuja TZ anytime akipata hicho kibali, na hao watalii watakuja TZ na kuingizia taifa faida, eventually na yeye jamaa yangu ataajiri watu na watu hao hao watapata kipato na kutunza familia zao hatimaye mzunguko wa pesa utaongezeka.

  Swali, inakuwaje serikali inafungia macho masuala ya maendeleo kama haya? Nimegundua kimoja jana kwamba pale mali asili kuna ubadhilifu sana, au ndiyo tuseme kuwa wale watu wa pale wengi wamefuji vyeti vyao maana hawajui wanafanya nini pale kwa sababu kila mmoja anamuhusisha mwenzake kuwa suala hili anashughulikia fulani na hili fulani, je huyo anayekuambia suala hili anashughulikia fulani yeye anafanya nini pale?

  Na hii siyo mali asili tu, hata pale TRA tumeyaona haya juzi, nobody knows anything ama wako tu pale kwa sababu mjomba yake ni boss. Rais Kikwete, tafadhali nyonga hawa vimeo kwani wanatuangushia taifa letu changa. Kumbuka Mh. rais, hatutafika popote kama taifa letu litakuwa linaongozwa na vimeo kwenye sekta nyeti.

  Jamaa yangu karudi Arusha bila mafanikio bali na masikitiko ya ubabaishaji ya idara zetu nyeti. Utalii Kenya na South Africa umeendelea kwa sababu people there follow orders ila hapa TZ we don't kisha tunalalamika wakati sumu ni sisi wenyewe. Sie TZ ndiyo inabidi tuwe juu zaidi ya hawa watu kutokana na kuwa na vivutio vizuri zaidi ila tumelala ukitaka kuamka unarudishwa tena kulala kulikoni? Je, tutafika kweli?
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  mtaji huo hauwezi kutufikisha popote penye maana
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada ananifurahisha anaposena "RAIS KIKWETE NYONGA HAWA WATU", mtoa mada hujui ulinenalo.
   
 4. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280

  Nasema inabidi vimeo wanyongwe kwa sababu wamelidanganya taifa na kutuingizia hasara. Fika TRA na mali asili uone uozo uliopo pale. Au mwenzetu nawe ni mmoja wa vimeo? Pole kama nimekugusa lakini bora ukweli uwekwe bayana kulikoni kuficha ujinga.
   
Loading...