Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,826
- 730,258
Kwasababu maisha na jinsi ya kuishi vina maelezo mengi kulingana na mtoa jibu upeo wake elimu yake historia yake mahusiano yake asili yake imani yake na hata jinsia yake.Mtu wa dini atakujibu kwa muktadha wa kidini na kiroho!
Mwana philosophia atakujibu kiundani na hata anaweza kukuchanganya, mwanasiasa atakujibu kiitikadi tajiri tabibu mwalimu mfanyakazi mfanyabiashara nk wote watakujibu kutokana na uzoefu na uhalisia wa fani zao Jaribu kujiuliza hapo ulipo unaishije? Kisha linganisha jibu lako na fani yako uone mfanano wa ajabu.