Salvatory Mkami
Senior Member
- Apr 17, 2013
- 146
- 244
Mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya ni ya muda tu au ni endelevu?!
Mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya ni kwa jiji la Dar es salaam pekee au ni nchi nzima na dunia kwa ujumla?!
Je, ni kweli "Vijana wanaangamia kwa matumizi ya madawa ya kulevya"?!
Hivi nani ambaye hajui madhara ya madawa ya kulevya?!
Hivi kuna mtu amelazimishwa kutumia madawa ya kulevya?!
Hivi kama Serikali kupitia vyombo husika vitayadhibiti ipaswavyo madawa ya kulevya kuingia nchini na kutopatikana hao vijana watayapata wapi madawa hayo na kuangamia katika mazingira gani?!
Kama mbinu na njia za kuingiza madawa hayo nchini zinajulikana kwanini hayadhibitiwi?! Je, tumejipanga vipi kuyadhibiti?!
Bajeti ya mapambano dhidi ya vita ya madawa ya kulevya ipo au haipo?! Kama ipo ni kiasi gani?! Kama haipo Je, mapambano yanaendeshwa kwa bajeti/gharama zipi?!
Tuna mpango gani na wale ambao tayari ni waathirika wa madawa ya kulevya?! Au labda waachwe tu wazagae mitaani kama ambavyo wamezagaa katika baadhi ya maeneo wakiendelea na matumizi ya madawa hayo kwasababu wameshaathirika?! Au labda wafikishwe kwenye Vyombo vya sheria na kufungwa gerezani?!
©S. Mkami