Je, Tumwombe Zitto Kabwe Afute Kauli Yake?

Je, Tumwombe Zitto Kabwe Afute Kauli Yake?

Sumaku

Member
Joined
Feb 17, 2009
Posts
53
Reaction score
1
Aliyoitoa Kigoma, kuwa 2015 atagombea Urais. Ni kwa tikiti ya CHADEMA? Au yeye hamuoni Dr Slaa?
 
He was joking bse by 2015 umri wake utakauwa haumuruhusu kugombea labda katiba ibadilishwe
 
Sumaku, Hapa Unasi Mtu. sisi ni Watanganyika na sio Wadanganyika tenaaaaaa!!!.
 
Kwani kugombea ni dhambi? Mbona ni jambo jema kabisa?!
 
Kwani tusema Dr. Slaa anashinda uchaguzi huu, ndiyo mwaka 2015 akisema basi ndiyo Zitto asigombee?
Au kama Dr.Slaa ndiyo atake kuendelea kwa awamu ya pili, ndiyo Zitto asijitokeze kupambana naye?
Najuwa chadema wana msimamo wa ki-CCM kuwa bosi hapingwi na ukimpinga "utakufa" lakini je, urais ni milki ya mtu binafsi?
 
Aliyoitoa Kigoma, kuwa 2015 atagombea Urais. Ni kwa tikiti ya CHADEMA? Au yeye hamuoni Dr Slaa?

Tulia.

Zito ana hekima sana.

Ni sehemu ya kampeni.

Ulitaka aseme nini kuonesha kuwa amekomaa kwa wapiga kura wake?
 
Tulia.

Zito ana hekima sana.

Ni sehemu ya kampeni.

Ulitaka aseme nini kuonesha kuwa amekomaa kwa wapiga kura wake?

IT'S ABOUT YOUR SLOGAN''' CCM-chama cha mujahidina''
unataka kutuambia CHADEMA ni kitu gani?? je ni chama cha VITA VYA MSALABA?(CRUSADE?)
USHINDWE NA ULEGEE katika jina la dr slaa
 
Tumalize ya 2010 kwanza..2015 yatafuata..!
Nini haraka..!???
 
Aliyoitoa Kigoma, kuwa 2015 atagombea Urais. Ni kwa tikiti ya CHADEMA? Au yeye hamuoni Dr Slaa?

Hapa nia ni kudivert mada moto za jukwaa...Someni threads zipo nyingi tu zilizoweka sawa jambo hili...search 'zitto' utapata...ni mambo ya kitoto zaidi kuliongelea hili kwa muda huu..Lets concetrate on how shall we quard the votes!
 
it is right for zito to express his intention so long election is a process at the end chadema will nominate the contestant
 
Kauli za zitto usizitilie maanani. Huko nyuma aliwahi kusema yeye ubunge basi lakini yupo ulingoni. Yeye hujiongelea tu
 
Huyu Zitto asituchanganye na kujidanganya. Sidhani kama ni mpinzani wa kweli. Namwona kama ni kinyonga fulani hivi (ana rangi ya CHADEMA at the same time anayo ya CCM). Hii ndio inanifanya niamini kuwa sio kila kingaacho ni dhahabu! Na pia mamwona kama ana uchu wa madaraka au kama ameshalewa hayo aliyonayo na kudhani kila madaraka atakayo atayapata au anastahili.

Unajua tatizo kubwa la mtu anayejiona yuko juu kiuwezo ktk siasa hulewa madaraka, na matokeo yako hufanya vitu bila kufikiria. Embu angalia jinsi alivyolewa madaraka hadi akataka alikimbie jimbo lake la ubunge na kutaka kurukia majimbo mengine. Hivi kweli huyu mtu anafikiri vizuri kweli?

Hivi kweli alipokuwa kwenye jimbo lake anataka atuambie alifanikiwa kutimiza yote yaliyokuwa kwenye plan na objectives/goals zake la mambo aliyopanga kuyafanikisha akiwa mbunge wa jimbo hilo hadi kuamua kukimbilia jimbo lingine? Jibu hapo kwa vyovyote vile ni kuwa hakutimiza yote aliyopanga kwa asilimia mia. Na kama ni hivyo why akimbilie jimbo lingine? Hiyo inaashiria kuwa ni mtu asiye na mipango, vision wala mission ambazo ziko consistent!

Yes ni mpigania haki mzuri! Lakini ambayo hayuko stable na ni mwepesi kulewa na madaraka na kudhani kila kitu anaweza akakifanya kwa mara moja(ubunge wa majimbo kibao na urais ndani ya miaka 5 !).

Hii inaashiria ni sign ya immaturity, tena gross immaturity! Na pia inanitia wasiwasi mbona anakimbilia vyeo na kuwa uchu wa madaraka kwa haraka sana?

Haf mbona ndugu Zitto ghafla amekuwa na maisha bora kuliko yale aliyokuwa nayo muda mfupi uliopita? Hali ya maisha yake imekuwa nzuri sana ghafla katika kipindi kifupi alichokaa bungeni! Hakika amefaidika na siasa kwa haraka sana kuliko wananchi anaowawakilisha na kuwatetea!

Ningependa atufafanulie utajiri wake WA GHAFLA (nauita utajiri, ikiwa ni "relative term" uki compare na Watanzania wengi hali yao ilivyo na pia na hali ya Wabunge wenzake walioanza nae ubunge). Au umetoka wapi? Nahofia mbunge wetu anayependa kutetea wanyonge asije akawa amewekwa kapuni na mafisadi wa CCM kama akina Rostam!

Ingependeza basi kama mheshimiwa Zitto angenifafanulia madukuduku yangu. Kwanini amekuwa na hali nzuri sana ghafla! Asije kuwa na speed kama ya mh. Lowassa!

Dr Slaa hoyeeeeeh!
 
Kwa kweli jamii forums ina mambo. Hivi karibuni tu wengi wenu mlikuwa mkilaumu utaratibu wa watu kuzuiwa kutangaza nia kwa wakati unaotosheleza watu kuwajua zaidi. Wengi mliwahi kudai kuwa mgombea urais ajlikane mapema ili mumchunguze vya kutosha. Anatokea mtu anawataarifu miaka mitano kabla tayari amekuwa amefanya dhambi.....Kazi kweli kweli
 
Ndugu yangu Omary kutangaza urais sio dhambi. Ni vema na haki. Lakini ukumbuke kama una peculiarities na some doubts surrounding you, usitegemee watu wakae kimya na wakupokee kwa mikono miwili na kukupigia vigelegele eti kwa kuwa wewe ni shujaa kwani umewahi miaka mitano kabla kutangaza nia. Ni vizuri sana mh. Zitto alivyotangaza nia ya urais mapema kwani anatimiza demokrsia na haki yake ya msingi ya kugombea urais kama ametimiza vigezo vyote.

Lakini ndugu yangu Omary nini lengo la kutangaza nia mapema?

Simply, ni kukuwezesha watu wakufahamu vizuri, mazuri yako (na mabaya yako) ili watu wapime na wenyewe waweze kuchuja na pumba na mchele then wa decide kukupa dhamana kubwa ya kuwalinda, kutetea, kuwatumikia na mwisho kuwaletea maisha bora zaidi ya yale uliyowakuta nayo!

Ndugu yangu unapochambuliwa ukae ukijua unapitishwa kwenye microscope kali kabisa na watu wanaku screen na kuku probe mpaka wajiridhishe kuwa unafaa. Hapo ndipo mtu unapochambuliwa na kuwa exposed kwa mazuri na mabaya yako! Yaani hapo ndipo unapovuliwa nguo kisiasa ili kuonekana usafi au uchafu wako.

Kama una mabaya ni lazima yasemwe, na kama kuna doubts ni lazima ziwe cleared. Na kama unasifa pia usifiwe. Ndugu yangu hiyo ni very painful process, kwani utapata kila aina ya dhoruba na hata kusingiziwa kunakuwepo. Lakini kama uko clean, then atleast unaweza ukatembea kifua mbele kama Dr Slaa bila wasiwasi, ingawa pia unaweza ukazushiwa mambo mabaya! Lakini mwisho wa siku wananchi ndio wanaamua uwepo au usiwepo. Lakini pia kura zako zinawezaibiwa au ukachezewa kila aina ya rafu za kisiasa.

Ndugu yangu hiyo ndiyo hali halisi, na ndio mchezo unaoitwa siasa! Cha maana kuwa strong, vumilia na pambana! TURIDHISHE, tu CONVINCE.

Sisi wananchi ni tunayo haki ya kujiridhisha na kutoa maoni na madukuduku yetu, lengo likiwa ni kuboresha na ni demokrasia.

Hivyo ndugu yangu naomba utofautishe kutangaza nia mapema na kuwa screened. Ni kweli kabisa hiyo process ya kuwa screened ni ngumu na ni kazi kwelikweli kama ulivyosema! Cheche lazima ziwepo!! kUONGEA NA KUTOA MAONI NA MADUKUDUKU NITAFANYA BILA KUSITA ILI NISIJEJILAUMU BADAE BALI NIPATE MTU ATAKEYENIONGOZA KATIKA MAISHA BORA!
 
Back
Top Bottom