Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Katika miaka ya hivi karibuni, kuna mambo mengi sana yamefanyika nchini Tanzania ambayo yamerudisha nyuma sana juhudi za kujenga jamii iliyostaarabika, inayojiheshimu na inayoheshimika.
Leo sitamnyooshea kidole yoyote kwa lawama hizi ila naomba nigusie tu madhara ya kuwa ‘a pariah state’.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia:
“A pariah state (also called an international pariah or a global pariah) is a nation considered to be an outcast in the international community. A pariah state may face international isolation, sanctions or even an invasion by nations who find its policies, actions, or its very existence unacceptable.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa “a pariah state ni taifa ambalo Jumuia ya Kimataifa imeliona kuwa halina hadhi au sifa za kuwa katika Jumuia hiyo. Na taifa hilo kama lisipojirekebisha huwa linaenda kutengwa, kuwekewa vikwazo, na hata kuvamiwa. Katika macho ya dunia, sera, matendo na hata uwepo wa taifa la namna hiyo ni vitu ambavyo havikubaliki”.
Kiufupi kuwa a pariah state, au an outcast siyo jambo zuri. Linakunyima vingi. Ndiyo, utabaki na uhuru wako wa kujifungia ndani na kujiamulia mambo yako wakati wenzako wanajumuika na kufurahi pamoja. Kuwa an outcast siyo jambo zuri kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa taifa.
Kwenye issue ya corona, Tanzania tuliona tuangalie kwanza maslahi ya taifa na tukaweka pembeni jukumu letu kama sehemu ya Jumuia ya Kimataifa.
Kutoa takwimu na taarifa rasmi na za uhakika za mambo kama maambukizi ya milipuko, ni moja ya majukumu yetu. Taarifa hizi zinasaidia dunia na wataalamu kujua mwenendo wa maambukizi na ndiyo msingi wa jinsi Jumuiya ya Kimataifa inatumia kujua wapi pa kusaidia. Fikiria kila taifa lingesema, sisi hatupimi na hatutoi taarifa zozote, leo dunia ingekuwa kwenye hali gani?
Tunatumia takwimu za wengine kuwazodoa kuwa wao corona imewapiga kweli kweli ila sisi takwimu zetu hatutaki kuzitoa.
Tunapowaza kuwa a pariah state, embu tuangalie taifa kama Eritrea limefaidika vipi kwa hali hiyo na ni hasara gani wamepata. Na hapo hata sijazungumzia mambo ya haki za binadamu na utawala wa sheria.
Naomba tujitafakari, nadhani kuna njia bora zaidi kuliko hizi tunazochukua.
NYONGEZA:
Sijui tafsiri rasmi ya kiswahili ya ‘a pariah state’ ila ukiniuliza mimi nitasema ni ‘taifa la kihuni’.