Je, trafiki anaruhusiwa kukunyang'anya leseni?

Je, trafiki anaruhusiwa kukunyang'anya leseni?

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
6.JPG

Kumekuwepo na sintofahamu nyingi kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya usafiri. Sintofahamu hii imekuwa ikiletwa na baadhi ya mambo ambayo hayaeleweki sawasawa katika suala zima la usalama barabarani na sheria zake. Wadau wa barabarani wamekuwa wakilaumiana, madereva wakiwalaumu askari wa barabarani kwa uonevu huku askari wa barabarani wakiwalaumu madereva kwa ukorofi na ukosefu wa utii wa sheria bila shuruti. Lakini swali hapa ni kwanini iwepo mivutano na hali kuna sheria. Sheria inasemaje kwa kila jambo ambalo wadau hawa wanatofautiana?.

1.UBABE WA ASKARI WA BARABARANI.
Baadhi ya askari wa barabarani wamekuwa ni wababe sana. Wanahoji mambo ambayo si wajibu wao kuyahoji na hawataki dereva aulize lolote kuhusu kuhoji kwao mambo hayo. Wanataka kila wanachosema dereva atii hata kama anaona hakipo kwa mujibu wa sheria. Matokeo yake mtu anaandikiwa faini za makosa mengi ilimradi tu kumkomoa. Askari wengine wamefikia hatua ya kuwapiga madereva vibao. Binafsi nimewahi kushuhudia askari wa usalama barabarani akimnasa kibao dereva wa daladala. Ni ubabe uliovuka mipaka na hakika ni uvunjaji wa sheria uliopitiliza.

2. JE TRAFIKI ANARUHUSIWA KUMNYANGANYA DEREVA LESENI.
Masuala ya usalama barabarani yanaainishwa ndani ya Sheria ya Usalama barabarani ( TheRoad Traffic Act) ambayo ndio hueleza wajibu na haki za kila mdau na mtumiaji wa barabara. Katika sheria hii hakuna pahala pameandikwa kuwa trafiki achukue leseni ya dereva kwa kuwa dereva ametenda kosa fulani. Maana fupi ya hili ni kuwa trafiki haruhusiwi kuchukua leseni ya dereva. Anachoweza kufanya trafiki ni kile kilichoainishwa na kifungu cha 17 cha sheria hiyo ya usalama barabarani.

Kifungu hicho kinampa trafiki mamlaka ya kukagua na kujiridhisha na uhalali wa leseni ya dereva. Hakisemi aichukue. Kinasema aikague basi. Kukagua na kuchukua ni mambo mawili tofauti.
Kama hivyo ndivyo basi yafaa kueleweka kuwa kitendo cha askari kumsimamisha dereva na kisha kumpokonya leseni yake ni kinyume cha sheria.Dereva anao wajibu wa kulinda haki hii kwa kulikataa hili na kuhakikisha trafiki hamfanyii kitendo hiki. Kumbuka kuwa wakati askari wa barabarani akitekeleza wajibu wake wa kisheria na wewe dereva unayo haki ya kutetea haki zako za kisheria. Hakuna aliye juu ya mwingine kwani anatekeleza wajibu nawe unalinda haki.

3. SAID MWEMA AKATAZA KUNYANGANYWA LESENI.
Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu ndugu Saidi Mwema aliwahi kuandika kukemea hatua ya madereva kunyanganywa leseni. Katika kijarida alichokiita UMESIMAMISHWA NA POLISI UKIWA UNAENDESHA ?, ZIJUE HAKI NA WAJIBU WAKO, ndugu mwema ameandika akisema kuwa ofisa wa polisi hana haki ya kuchukua leseni ya dereva.

4. HAIRUHUSIWI KUBANDUA BIMA/ AU KIBANDIKO( STICKERS) KINGINE CHOCHOTE.
Wakati mwingine askari wa barabarani huamua kubandua bima au vibandiko vingine ( stickers) kwa lengo la kumfanya dereva amfuate au malengo mengine yoyote. Hili nalo ni kosa kwakuwa haliainishwi popote katika sheria. Jambo ambalo halikuruhusiwa na sheria kulitenda kwake ni kosa. Ieleweke kuwa askari wa barabarani haruhusiwi kubandua stika yoyote katika gari lako wala kuichukua.

5. UKIONEWA NA ASKARI WA BARABARANI CHUKUA HATUA HIZI.
Ili uweze kumchukulia hatua vizuri askari ni vema ukijua jina lake, cheo chake, na kituo anachotokea. Katika kuyajua haya ni lazima watu wajue kuwa ni haki yako kumuuliza askari taarifa hizi. Sio dhambi wala kosa ila ni haki kumuuliza askari taarifa hizi. Na kwa askari ni wajibu kukueleza taarifa hizi. Haijalishi mmeshatofautiana wala nini isipokuwa ni wajibu akupe taarifa hizi. Lakini ushauri ni kuwa ni vema zaidi askari anapokusimamisha tu kabla ya kujadili lolote kumuuliza au kumuomba ajitambulishe ili hata mkishatofautiana mbeleni iwe rahisi kwako kuchukua hatua.

Kiutaratibu inatakiwa askari ajitambulishe kwako bila wewe kumuuliza na kabla ya kuzungumza lolote lakini kwakuwa hawafanyi hivyo ndio maana wewe unalazimika kumuuliza. Baada ya kupata taarifa hizo peleka malalamiko yako kwa mkuu wa kituo anachotokea halafu fuatilia.

Atachukuliwa hatua wala huna haja ya kulihofi hilo. Jeshi la polisi ni sehemu ambako nidhamu inazingatiwa kuliko pahali pengine popote hivyo unapomripoti askari ni lazima ashughulikiwe.

Kwa taarifa yako askari wanaogopa sana kuripotiwa kwa wakubwa zao kuliko watumishi wengine wowote wa umma unaowajua, hili nakupa. Na askari yoyote mwenye kujitambua akijua unalenga kumripoti ni lazima akubali myamalize. Basi usiishie kulalamika kwani kulalamika hakusaidii chukua hatua ili iwe funzo kwa wengine kesho na mbeleni.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
 
Askari yupi wa usalama barabarani anaruhusiwa kukagua hati ya kuendeshea gari? (Maana ya cheo gani.)
 
Siku hizi nimegundua kitu. Nikibambikiwa noti feki ya elfu kumi au tano siitupi. Akinisimamisha trafiki wala sipendi maongezi, baada ya salaam tu namwambia MKUU BAMBA HII UKAPATE SUPU upige kazi vizuri.

Hawanaga muda wa kukagua kama hela ni feki au halal.
 
Asante kwa kutujuza, mamlaka aliyonayo askari kukaguwa leseni yako ndio chanzo cha kunyang'anya hiyo leseni, sababu hukataa kuirudisha hiyo leseni. ..kwa wale wanaojiweza na wanachukia mlungula huziacha hizo leseni na kwenda kuchukua lost report na kupata leseni nyingine. Hawa polisi wa barabarani wana leseni nyingi majumbani mwao na sijui wanajisikiaje. ..??? Nyie mapolisi mnaosoma JF kwanini mnafikiri kuwa polisi ni siraha ya kunyanyasa watu?? Ugumu wa maisha yenu msihamishie kwa raia... nawapenda lakini nawachukia kwa vitendo vyenu vya uonevu. .
 
Asante kutuelimisha mm walichukua license yangu nikaawachia nikaenda kuchukua nyingine
 
@i @i @i @i @i yyyyyap wazma za s..................................la@aa
 
Siku Hizi hadi Hawa Askari wanaovaa GWANDA za kijani FFU Tena ana SILAHA wanagua VIBALI na LESENI
 
Hawa wanasheria wa mitaan hawa muwe makin nao.

Trafic anaweza kukunyang'anya lesen yako endapo itapatikana na makosa mfano, lesen yako imeisha mda wake, lesen yako inaonesha class tofauti na gari unayoendesha, umetumia lugha chafu au umemzuia kufanya kaz yake na huyo trafic kupitia
vihicle inspetor anauwezo wa kukufungia lesen yako isifanye kaz tena..

Sasa unavyojitutumua mbele ya askar hakikisha unaijua vyema sheria na uwe unatambua ya kuwa huyo askar ana makosa kweli.

Wengi nmeona wanajitutumua kwa kuwa wamefundishwa na bush lawyer baadae wanajikuta wanaingia kwenye makosa ya kujitakia..
 
Siku hizi nimegundua kitu. Nikibambikiwa noti feki ya elfu kumi au tano siitupi. Akinisimamisha trafiki wala sipendi maongezi, baada ya salaam tu namwambia MKUU BAMBA HII UKAPATE SUPU upige kazi vizuri.

Hawanaga muda wa kukagua kama hela ni feki au halal.

Hahaha nakumbuka nikipita Iringa nakuja dar trafic mmoja kanidaka mim nilikuwa na haraka nikapiga mfukoni nikatoka huko na jero nikaikunja nikampa yeye kwa kujificha kaitupia mfukoni! kuja kupita tena pale kaniona kabaki kucheka
 
Kati ya vitu vinanikwaza kwa trafic ni kung'ang'ania leseni au kadi ya gari.
Inakera sana.
 
Askari yupi wa usalama barabarani anaruhusiwa kukagua hati ya kuendeshea gari? (Maana ya cheo gani.)

Ni askari POLISI yeyote aliyekula kiapo bila kujalo cheo na wala so lazima awe trafiki.
 
Askari kuzaba makifi madereva;

Hii ilitokea Tabora. Trafiki mmoja pale stendi ya mabasi ana tabia hiyo. Siku moja akamkamata jamaa anaendesha pikipiki hana helmet. Alifika sstendi akaipaki baadaye askari huyo akamfuata. Katika kujibizana askari akataka kumnasa kibao jamaa akaudaka mkono. Palichimbika! Kumbe jamaa ni JWTZ Mirambo barracks......Askari traffic huyo alipigwa ikabidi waite askari kama 20 kutoka kituo kikuu cha polisi Tabora. Askari hao walishindwa kumkalisha chini ndani ya karandiklnga. Alikwenda amesimama mpaka kituoni. Mimi siwapendi kabisa polisi na nina sababu!
 
Hawa wanasheria wa mitaan hawa muwe makin nao.

Trafic anaweza kukunyang'anya lesen yako endapo itapatikana na makosa mfano, lesen yako imeisha mda wake, lesen yako inaonesha class tofauti na gari unayoendesha, umetumia lugha chafu au umemzuia kufanya kaz yake na huyo trafic kupitia
vihicle inspetor anauwezo wa kukufungia lesen yako isifanye kaz tena..

Sasa unavyojitutumua mbele ya askar hakikisha unaijua vyema sheria na uwe unatambua ya kuwa huyo askar ana makosa kweli.

Wengi nmeona wanajitutumua kwa kuwa wamefundishwa na bush lawyer baadae wanajikuta wanaingia kwenye makosa ya kujitakia..

Vizuri kama utatuwekea vifurngu vya kisheria vinavyomwelekeza askari polisi kunyang'anya driving licence. Ninachofahamu kama kitu ni feki kuna sababu ambazo zinaweza kumfanya polisi kuchukua kitu faki au cha wizi
kama kielelezo katika kesi atakayofungua mahakamani. Kimsingi bado hatujaona sheria inayomruhusu polisi kunyanyanga document kwa sababu ya kosa la usafriri barabarani vinginevyo ni faki, wizi nk.

Kimsingi ujue kuwa driving license ni kitambulisho rasmi cha serikali, hivyo kunyang'anya ni kosa la kumnyima kitambulisho chake halali.
 
Hawa wanasheria wa mitaan hawa muwe makin nao.

Trafic anaweza kukunyang'anya lesen yako endapo itapatikana na makosa mfano, lesen yako imeisha mda wake, lesen yako inaonesha class tofauti na gari unayoendesha, umetumia lugha chafu au umemzuia kufanya kaz yake na huyo trafic kupitia
vihicle inspetor anauwezo wa kukufungia lesen yako isifanye kaz tena..

Sasa unavyojitutumua mbele ya askar hakikisha unaijua vyema sheria na uwe unatambua ya kuwa huyo askar ana makosa kweli.

Wengi nmeona wanajitutumua kwa kuwa wamefundishwa na bush lawyer baadae wanajikuta wanaingia kwenye makosa ya kujitakia..
Jifunze, usisubiri uambiwe cha kufanya. Kukariri ni ujinga c kujua.
 
Traffic ni gari, askari wa magari anaitwa traffic police. Traffic jam ni msongamano wa magari.

#TeamUkawa
 
Asante kwa kutujuza, mamlaka aliyonayo askari kukaguwa leseni yako ndio chanzo cha kunyang'anya hiyo leseni, sababu hukataa kuirudisha hiyo leseni. ..kwa wale wanaojiweza na wanachukia mlungula huziacha hizo leseni na kwenda kuchukua lost report na kupata leseni nyingine. Hawa polisi wa barabarani wana leseni nyingi majumbani mwao na sijui wanajisikiaje. ..??? Nyie mapolisi mnaosoma JF kwanini mnafikiri kuwa polisi ni siraha ya kunyanyasa watu?? Ugumu wa maisha yenu msihamishie kwa raia... nawapenda lakini nawachukia kwa vitendo vyenu vya uonevu. .
Tatzo la pols tz,ni akikumata umekua ATM
 
Mi kuna mmoja alinidaka nkampa buku 5 akakataa, nilikuwa na US$ kwenye wallet nkamwambia chukua hii bas akaichukua haraka kumbe ilikuwa ni US $1😆😆😆😆
 
Siku hizi nimegundua kitu. Nikibambikiwa noti feki ya elfu kumi au tano siitupi. Akinisimamisha trafiki wala sipendi maongezi, baada ya salaam tu namwambia MKUU BAMBA HII UKAPATE SUPU upige kazi vizuri.

Hawanaga muda wa kukagua kama hela ni feki au halal.

Aisee ubarikiwe sana mkuu umenipa maujanja
 
Back
Top Bottom