Je, tokea lini unit moja ya LUKU imefika 700/=??

Je, tokea lini unit moja ya LUKU imefika 700/=??

Kuwa mpole mkuu jamaa sasa hivi wanafukua makaburi hatari. Ilo deni unawezakuta Lina miaka hata mitano ila sasa ndo wameamua kuanza kukata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF?

Katika hali ya kushangaza leo tumeongeza umeme wa 20,000/= kwa kutumia tigo pesa, nashangaa tumepewa units 28.1 ambazo ni sawa na 711 Tsh per unit!!

Je ni kwamba unit moja imefika 711Tsh??

Tokea lini hii bei imeanza?? Au ni wapi tumekosea??
kwani kawaida Unit 1 ni Tsh ngapi?
 
Nenda jukwaa LA tenesco hapa kuna ubuyu tyu

acha uongo
 
Nilipo ni ngumu kuwapata TANESCO mkuu! Wako mbali!!
Sasa hapa hutopata jibu bali utagewa viashiria na visababishi vya hilo tatizo lako lakini jibu sahihi nenda tanesco na meter namba yako mhasibu atakudirect sehemu husika watakufungulia mtiririko wa mita yako mpaka ulipofikia sasa hivi utaona kila kitu na hautakua na swali tena. Labda nikudokezee jambo moja kuna wakati kuna mambo yanafanyika may be bila kujua au kwa uzembe wa baadhi ya watu kati ya mtumia umeme na muuza umeme yaani tanesco. Kama mliwahi tumia meter zile za zamani alafu bahati mbaya kulikua na deni kumbuka kule unaweza kuwa na deni na bado ukala umeme kama kawa, sasa wanapokuja kukubadirishia kukuwekea luku hawakuambii chochote na wakati wanakuwekea luku unaweza kuanza kutumia luku yako kma kawaida na ukanunua umeme vizuri tu ata miezi sita ikapita baadae sana ndio wanaliingiza lile deni lako kwenye luku yako bila ata kukutaarifu wewe utashangaa unatoa elfu 10 unapata umeme wenye gharama sawa na elfu tano yaani ukitoa elfu 10 wanakata nusu ya hela uliyotoa inalipia deni alafu nusu iliyobaki ndio unapewa umeme na hii wanaiset automatically haikwepeki popote utakaponunua umeme itakata tu, hiyo ni kesi moja kesi nyingine unakuta wakati wa kubadirishiwa mita ya kawaida kwenda luku mteja anaambiwa kuwa kuna deni sasa either anaona deni.ni kubwa anatafuta njia ya ujanja ujanja kutaka afutiwe lile deni ndipo anapokutaka na baadhi ya workers wasio waaminifu na kumlia pesa na kumuhaidi kulifuta lile deni kumbe mteja smasiki ya Mungu bila kujua kuwa lile deni halifutiki kizembe hivyo maana limeshafanyiwa auditing anachofanya yule jamaa ni kukucheleweshea muda wa kulipa tu hilo deni na mwisho wa siku utashangaa unaingizwa katika wadaiwa sugu hivyo hakuna haja ya kupewa taarifa badala yake wanakuingizia katikamita yako mpya ambayo ni luku yako. Fika tanesco au kesho piga simu watakuangalizia ila wakati unapiga simu uwe na mita namba yako karibu
 
unaingizwa katika wadaiwa sugu hivyo hakuna haja ya kupewa taarifa badala yake wanakuingizia katikamita yako mpya ambayo ni luku yako. Fika tanesco au kesho piga simu watakuangalizia ila wakati unapiga simu uwe na mita namba yako karibu
Nimekuelewa sana mkuu!!
 
Back
Top Bottom