Je, tishio la El-nino ni mbinu kututoa DP World!

Je, tishio la El-nino ni mbinu kututoa DP World!

Wabonho tujenge utamaduni wa kusoma au kutafuta habari, tunatia aibu sana, Swala la hizi mvua ziko hadi kwenye Website za FAO na walisha tahadharisha na sio Tanzania tu bali ni East Africa yote.

Tutafute habari
 
View: https://youtu.be/45tUyT29Xx8?si=FiDJLgdgOnGlidgn

Nimewaona hawa wataalamu wa "TMA" kupitia Luninga ya "ITV"habari saa mbili jioni hii. wametoa tahadhali ya mvua kubwa za majanga almaarufu kama El-nino!

Ambazo wanasema zitanyesha kwa wingi sana mwezi huu,na huenda zikavunja madaraja ya reli na miundombinu mingi ya Barabarani na mafuriko nchi nzima.

Ni vema na shukrani ziwaendee.kama itakuwa kweli. Na hii ni mara ya kwanza kwa kitengo hiki kujitokeza na kutoa tahadhali ya janga kubwa kama hili nchini.

Shaka yangu kuu:
Ni kwamba haya masuala ya utabiri wa hali ya hewa, hayatolewi kwa kipande kipande cha ardhi au mipaka ya nchi fulani pekee.

Bali tunaona likiwa ni suala ambalo ni "Global" nikimaanisha ni la kidunia kama "Planet World"

Na tunashuhudia kupitia luninga mbalimbali Duniani zikiwemo maarufu kama CNN, Aljazeera, BBC, France international nk.

Hawa wanaripoti hali ya hewa kwa Dunia nzima na hata tunaona ikionyesha ziwa victoria bahari ya Hindi Dar es Salaam kwa kina kabisa.

Na mara zote imekuwa inatokea kuwa kweli na ninadhani hata hivi vyombo vyetu hapa nchini huwa vina Paste saa ingine kutoka huko.

Sasa basi, hoja yangu na Mashaka yangu ni kwamba haiwezekani vifaa vya Tanzania ambavyo kiuhalisia haviwezi kuzidi vile vya mataifa ya magharibi ambao wanaviona vimbunga na kuwaondoa raia wao maeneo hatarishi.

Kwamba vya kwetu vimeiona El- Nino ya mwezi wa tisa leo?

Ila vile vya nje wanako kopi havijaiona hiyo?

Hii mimi nasema ulu msemo maarufu wa watani zangu wa kichaga.

"NGASHTUKA"
Kuna wahuni wanajaribu kwa kila namna kututoa kwenye mjadala wa DP-WORLD kwa kutaka kututia hofu jamii ili tujisahau kwao wapitishe mambo yao chap, kupitia bunge lijalo kwa kubadili vile vifungu viwili vya dheria ya uwekezaji.
Kwa kuondoa kinga ya "TUNU" za Taifa.

Je, majirani zetu Kenya wao hii haiwahusu?

Au hawana utaalamu kama wetu?

Who cares?
 
Kuwaamini hao TMA hakuna tofauti na kuamini waganga wa kienyeji.
 
MAONO NILIYOYAONA WAKATI NIKISIKIZA VIDEO U-TUBE UNYAKUO TV KUHUSU MAFURIKO YAJAYO MAY.

Nikiwa naendelea kusikiza video, uliopita kama USINGIZI hivi, ghafula nikaona,

Nilikuwa nyumbani, ndani ya nyumba, Hali ya hewa ikiwa tulivu kabisa jua likiwaka.

Cha kushangaza katika maono hayo, nilikuwa ndani ya nyumba, lakini nilikuwa na uwezo wa kuona Kila kitu kilichoendelea nje.

Niliona na kusikia upepo mkalia ukivuma Kwa Kasi Kutokea mashariki, nilidhani ni dalili ya mvua ya kawaida,

Kufumba na kufumbua, nami nikaona mbinguni juu ,duara jeusi lenye kuzunguka mithili ya sahani flat, palikuwa na maji yakizunguka Kwa Kasi katika duara Hilo, maji hayo hayakudondoka hata tone chini ardhini,

Wakati nikiendelea kutizama duara lile likizunguka, ndipo nikaona umetokea mfuniko uliokuwa umeziba maji Yale ,RANGI ya mfuniko ilikuwa bilauli ukifunguka na kumimina maji Yale ardhini tulipokuwepo na Kisha kujifunga.

Baada ya kuona tukio lile, nilihisi hatari inakuja, sasa kitendo Cha Mimi kutaka kuwambia wenzangu ndani ya nyumba kwamba tutoke na kuchukua zana za kutuepusha na hatari, ghafula nilijiona nikielea juu ya maji sikuona mtu mwingine yeyote, hapakuwa na nyumba Wala mti, au mlima ulioonekana. Vyote vilikuwa ndani ya maji.

Mwisho wa maono!!

Cc: 7seven

Tresor Mandala
 
Mtoa mada umewaonea sana TMA. Mimi ni mdau wa Climate Change. Taarifa hii TMA walianza kuliongelea mwezi wa Tano. Na kuongelea tena tarehe 4June wakisema wanaendelea kufuatilia Hali hiyo kufuatia mgandamizo wa hali ya upepo bahatini na wakaahidi kuelezea kwa kina Mwezi August. Tuwaache wafanye kazi yao kwa Sasa wana mitambo ya kisasa sana Jiwe aliwanunulia.
 
MAONO NILIYOYAONA WAKATI NIKISIKIZA VIDEO U-TUBE UNYAKUO TV KUHUSU MAFURIKO YAJAYO MAY.

Nikiwa naendelea kusikiza video, uliopita kama USINGIZI hivi, ghafula nikaona,

Nilikuwa nyumbani, ndani ya nyumba, Hali ya hewa ikiwa tulivu kabisa jua likiwaka.

Cha kushangaza katika maono hayo, nilikuwa ndani ya nyumba, lakini nilikuwa na uwezo wa kuona Kila kitu kilichoendelea nje.

Niliona na kusikia upepo mkalia ukivuma Kwa Kasi Kutokea mashariki, nilidhani ni dalili ya mvua ya kawaida,

Kufumba na kufumbua, nami nikaona mbinguni juu ,duara jeusi lenye kuzunguka mithili ya sahani flat, palikuwa na maji yakizunguka Kwa Kasi katika duara Hilo, maji hayo hayakudondoka hata tone chini ardhini,

Wakati nikiendelea kutizama duara lile likizunguka, ndipo nikaona umetokea mfuniko uliokuwa umeziba maji Yale ,RANGI ya mfuniko ilikuwa bilauli ukifunguka na kumimina maji Yale ardhini tulipokuwepo na Kisha kujifunga.

Baada ya kuona tukio lile, nilihisi hatari inakuja, sasa kitendo Cha Mimi kutaka kuwambia wenzangu ndani ya nyumba kwamba tutoke na kuchukua zana za kutuepusha na hatari, ghafula nilijiona nikielea juu ya maji sikuona mtu mwingine yeyote, hapakuwa na nyumba Wala mti, au mlima ulioonekana. Vyote vilikuwa ndani ya maji.

Mwisho wa maono!!
Mkuu

Hii itakua KWA Tanzania nzima au KWA dar tu!!?
 
Mkuu

Hii itakua KWA Tanzania nzima au KWA dar tu!!?
Bandari salama ndo inasoma hatari kubwa, ingawa matatizo hayo yatakuwa Mahali Mahali.

Mungu kutuonyesha haya, anataka tuombe, wote Kwa pamoja tukusanyike na kulia kuomba TOBA Ili atuepushe.

Watu na viongozi wanauona ujumbe lakini wanapuuza, wanausubiri yakitokea ndo wastuke,

Hapo bandari salama kama ikitokea inavyoonekana ktk Roho, mji hautakuwepo tena!!!
 
Back
Top Bottom