Je tatizo la BP linaweza sababisha figo kufeli?

ubwindo

Member
Jul 23, 2017
43
29
Habari zenu wote...
Niende direct kwenye mada kuna mtu namfahamu amepat shida ya figo, imepelelekea mpaka kua anasafishwa kila wiki hospitali.
Kinachonifanya niulize humu ni sababu aliyonipa ya kupata tatizo lake kuwa ni baada ya presha kupanda.
Je ni kuna ukweli hapo?
Nawasilisha.
 
Uhusiano upo...

Mtu anapokuwa na pressure iliyopanda maana yake ni kwamba mishipa ya damu imekuwa myembamba,(vasoconstriction). Hii husababisha damu kutofika vizuri au ya kutosha kwenye viungo muhimu ikiwemo figo,ubongo na ini.
Figo inapokosa damu ya kutosha maana yake haipati oxygen vizuri na seli za figo hufa kwa kukosa oxygen. Hii hufanya figo kufa na kutofanya kazi vizuri.

Pia mishipa inapokuwa myembamba ni rahisi kwa damu kuganga kwenye mishipa na damu kushindwa kupita kabisa. Mfn wale wanaopata stroke kwa sabb ya presha kupanda ni kwa sababu presha imesababisha damu kutofika kabsa kwenye ubongo au mishipa kupasuka kwenye ubongo. Hii pia inaweza sababisha damu isifike kabisa kwenye figo kupelekea figo kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi.

Kifupi huo ndo uhusiano.
Naweza rekebishwa kama nimekosea pia.
 
GoPPiii asante, nimepata mwanga
 
Back
Top Bottom