Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,292
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali. Kufuatia mahojiano ya jana, kwenye Star TV, imethibitishwa pasi shaka kuwa ni kweli muhojiwa hana vyeti vya elimu zaidi ya cheti cha darasa la saba tuu ndicho chenye jina lake alilopewa na wazazi wake pale alipozaliwa kijijini Kolomije na kuandikishwa Shule ya Msingi ya Kolomije.
Mahojiano hayo yamezua mjadala mkali huku kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakisema ametia aibu.
Hili ni bandiko la swali, Jee sisi Watanzania tunataka Viongozi wa aina gani? . Wajinga wenye zero,na wasio na vyeti lakini ni wachapa kazi na wana deliver, au wasomi wenye macheti hadi ma Ph.D lakini ni Mangi Meza, hukaa ofisini tuu na makabrasha lundo, lakini kwenye delivery ni zero?.
kuna hoja nimesoma mahali kuwa eti muhojiwa ametia aibu kukwepa kuzungumzia elimu yake, vyeti vyake, kufoji vyeti na kulikana jina lake halisi, na badala yake kukumbatia jina la wizi.
Jee ni kweli muhojiwa ametia aibu?. Jee ameaibisha mamlaka yake ya uteuzi?, kipi muhimu kwa muhojiwa kati ya macheti au uchapakazi wake unaodeliver? .
Jibu ni a big No. Muhojiwa hajajiaibisha wala hajaiaibisha mamlaka yake ya uteuzi, kwa sababu amejieleza vizuri kabisa kwa kiwango cha elimu yake ya darasa la saba.
Huyu mtu elimu yake ni darasa la saba, hivyo ameongea kama darasa la saba na kiukweli amejieleza vizuri. Mimi nimeridhika. Amefunika na ndie shujaa wa kipindi hicho. Thamani yake ni uchapakazi wake na sio macheti!.
Ili mteuliwa amuaibishe mteule, only if kauli, maneno na matendo ya mteuliwa, yatamuaibisha mteule na ndipo mteule huchukua hatua kuondoa aibu hiyo kama alivyofanya kwa Mhe. Kitwanga.
Lakini mteuliwa hata akifanya vitendo vya ajabu kiasi gani, au vya aibu kiasi gani, kama mteule hajaona aibu kwa vitendo hivyo, then, mteuliwa huyo anakuwa hajajiaibisha wala hajamuaibisha mteule wake kwa sababu hiyo aibu haipo.
Ili mtu kujisikia umeaibika, hatua ya kwanza ni lazima kwanza hiyo aibu yenyewe iwepo ndipo mtu ujisikie aibu. Lakini ikitokea hiyo aibu yenyewe haipo, mtu huyo hawezi kabisa kujisikia aibu. Yaani hana haya!.
Hivyo mhojiwa, hajajiaibisha wala hajamuaibisha yoyote kwa sababu huyo wa kuibishwa, hata aibu yenyewe hana!, ndio maana mpaka leo, mpaka kesho na mpaka keshokutwa mchapakazi huyu anaendelea kuchapa kazi, licha ya kuwa hana vyeti, hana aibu na hana haya! na wanao aibika sasa ni wale wanaodhani anaaibisha!.
Aibu ni kama kutumia akili au kutumia hekima na busara.
Ili mtu kutumia akili, jambo la kwanza ni lazima hiyo akili yenyewe iwepo!. Ikiisha kuwepo ndipo itaweza kutumika. Inapotokea hata hiyo akili yenyewe ya kutumika haipo, hawezi kumwambia mtu kuwa hakutumia akili as if akili hiyo ipo na mtu anayo lakini hakuitumia, ikitokea mtu huyo, akili hiyo hana kabisa, japo ni mchapa kazi hodari lakini kichwani ni mtupu kabisa, hana aibu kwa utupu wake kichwani, hana vyeti, ila ni hodari na mchapakazi, na mamlaka yake ya uteuzi haiuoni huo utupu wake, unaouona wewe, then ujue hicho ndio kiwango cha mamlaka hiyo uteuzi, ambayo kama hata bila ya vyeti au kwa kufoji vyeti na kufoji jina, lakini imeridhika naye, kwa bidii yake, kwa kujituma kwake, kwa uchapakazi wake, who are you kuhoji vyeti vya mchapakazi huyu?!.
Vivyo hivyo katika matumizi ya hekima na busara, ili hekima na busara itumike, ni lazima kwanza hiyo hekima na busara iwepo. Kama hekima na busara haipo kabisa ndani kichwa cha mtumiaji, ukimtegemea kutumia hekima na busara, ni kumuonea bure!. Hiyo hekima na busara ya kutumika itoke wapi wakati haipo kabisa?!.
Natoa wito kwa sisi wana JF, tuwaache wachapa kazi wachape kazi, hii ni awamu ya hapa kazi tuu, sio hapa cheti cha elimu au hapa hekima na busara, hapa ni kazi tuu!.
Wenye aibu zenu kaeni nazo hizo aibu zenu, wenye vyeti vyenu kaeni navyo hivyo vyeti vyenu, wenye akili zenu, kaeni nazo hizo akili zenu na ma vyeti yenu ya elimu zenu, na busara zenu kaeni nazo wenyewe; sisi tunataka kazi tuu na wachapakazi tuu wanaodeliver , hata kama hawana vyeti, hawana akili, hawana aibu, hawana haya kudanganya majina na kutumia vyeti vya kughushi, na hawana hekima na busara za kufunga mabakuli yao, as long as ni wachapakazi, wataendelea kuwepo na kulindwa kwa nguvu zote hata kwa kuwatumia makirikiri kwa sababu, thamani yao ni uchapakazi wao tuu, na sio vyeti au majina ya wizi wanayotumia!.
Jiji la Dar es Salaam ni cosmopolitan city, the majority ni watu wa kawaida sio the elites. The elites wana occupy only a small fraction of the city, Town centre, Seaview, Upanga, Oysterbay, Masaki, Mikocheni na Mbezi, huko ndiko kwa the elites wanaohitaji vyeti, the rest ni kwa watu wa kawaida, the working class na Uswazi kwa Waswazi ambao hawahitaji viongozi wenye macheti. Wao wanachohitaji ni viongozi wanao delivers. Paul Makonda delivers na ameweza kwasababu anafanana nao!. Mtu mwingine aliyeliweza Jiji la Dar es Salaam ni Yusuf Makamba, katafuteni elimu yake na vyeti vyake ndipo mtanielewa!.
Namalizia kwa Hili swali
la msingi la bandiko hili, Jee sisi Watanzania tunataka Viongozi wa aina gani? . Viongozi Wajinga wasio na vyeti au waliofeli kwa kupata zero darasani, lakini kwenye utendaji, ni wachapa kazi hodari na wana uwezo mkubwa ku deliver, au tunataka viongozi wasomi wenye macheti makubwa hadi ma Ph.D lakini ni akina, Mangi Meza, kazi yao ni kukaa tuu ofisini na lundo la makabrasha, lakini kwenye delivery, uwezo wao ni zero kabisa?.
Jumanne Njema.
Paskali.