Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?.

Paskali pole.
Instant justice ya DAB ni hulka yake. Hata kama angekuwa na vyeti halisi, nina mashaka kama angebadilika.
Watu wenye hulka kama yake huwa hawasaidiwi na elimu ya vitabuni. Hulka hii katika aiba yao ni matokeo ya malezi na uzoefu wa ubabe unaotokana na maisha alimopotia na kukulia.

DAB amefanya kazi ya ukondakta, house boy, errand boy na mbabe wa kijiwe. Amewahi kukodiwa kutukana, kudhalilisha na hata kupiga. Ukiona haya, uwe na uhakika kuwa hulka ya kupenda kuonekana na ubabe wa kifisadi, haviwezi kubadilishwa na elimu ya vitabuni.

Ikumbukwe licha ya kununua cheti chenye jina la mtu mwingine, DAB alipita darasani kule Moshi na kuhitimu. Lakini ukiona ujenzi wa hoja zake na kiwango cha kutojitambua nafasi yake, unagundua kuwa elimu ya vitabuni haina nafasi katika usugu wa tabia aliyo nayo.

Mahojiano yake na Star TV yameonyesha wazi na kwa kweli kawaaibisha waliopanga naye mkakati wa damage control. Mathalani:
- suala la vyeti limemshinda kulieleza
- suala la kuvamia studio ameishiwa kubwabwaja maneno
- Ameshindwa kuficha chuki yake dhidi ya Nape na Gwajima
- Ameshindwa kujieleza juu ya mwanamke wa shilawadu
- Ameshindwa kueleza ni kwa nini alienda na silaha studio usiku
- Ameshindwa kujieleza kwa nini aligoma kuhojiwa na tume
- Ameendelea kujilinganisha na mawaziri
- Ameshindwa kuficha siri binafsi na za marafiki zake katika masuala ya fedha za michango
- Ametumia majigambo mengi alivyo karibu na Mungu
- kila anayepingana naye anapewa sifa ya kuuza unga
- DSM ni mkoa na mali yake, na wakazi wa Dar ni kama watoto wake!
- Vicarious liability anaitumia vibaya kuhalalisha madhambi yake
- ukitofautiana naye ni sawa na kutofautiana na Mungu
- kwake matokeo ya kazi ni bora kuliko njia za kufikia matokeo hayo

Kimsingi, DAB ni kituko na Paskali unafanya mzaha kumlinganisha na viongozi wasomi.
Yaani kututaka kuchagua kati ya kiongozi asiye na elimu lakini mchapa kazi na mwenye elimu lakini mangi meza. This is an invalid comparison. Si kila Mbashite ni mchapa kazi na si kila msomi ni mangimeza.
DAB hayuko katika makundi hayo mawili.
Mimi nitakuwa sijamuelewa paskali,mbona kama hajamlinganisha na mtu yeyote sana sana amemuona kituko
 
Kiongozi umeelezea vizuri mno mada yako na kwa kuzingatia kwamba umeweka bayana suala la DAB kuwa STD vii na hata jinsi alivyojibu hoja zake zimeshabihiyana na Elimu ya kiwango hicho.

Kumbuka kwamba tuna miaka Mingi toka tupate Uhuru na kipindi hicho wasomi walikua wachache na hilo lilisababisha watu kupambana kutafuta Elimu .Hili umelikiri kwa kusema kwamba ameelezea hoja zake kwa kiwango cha Elimu ya darasa la saba. Kwa sasa tunategemea kuwa kama serikali inatumia kama trillion tatu na kitu kwenye kugaramia Elimu basi tutumia wasomi hao kwenye mambo yetu ili kuongeza tija zaidi kwenye utendaji na uongozi.

Ndio maana imefika sehemu hata Mh.Rais ameamua kuwaondoa waliofoji vyeti kwa kuwa tayari wapo wenye vyeti halali mtaani ambao wanaweza kuchukua nafasi hizo na kufanya vizuri zaidi kwa kutumia Elimu halali na sio zile za kuunga unga.

Mayalla unaelewa umuhimu Wa Elimu labda tu unajitoa ufahamu .Twende taratibu utakua na watoto wanaosoma Shule tena nzuri tu kwa nini usiwaache wakae mtaani ili wajifunze uchapaji Kazi badala yake wlumewapeleka Shule za maana waelimike waweze kutumia Elimu hiyo kwa maisha yao na vizazi vijavyo.

Tutakua wanafiki Wa kiwango cha standard Gage iwapo tutakua tunabeza nguvu ya Elimu katika maswala yanayoonekana wazi kwamba kuna mkwamo Wa moja kwa moja kwa kuwa tu Elimu imekosekana.

Ikumbukwe kwamba suala la DAB sio suala la kutokua na Elimu Bali ni kuwa na kashfa ya kufoji cheti na kuwa kiongozi ambaye anajipambanua kwamba ameapa kwa katiba na ataitumikia ili hali ameshavunja katiba hiyo kama ni kweli amefoji vyeti na hapa ndio waelewa na tusiokua na punje ya ubafiki tunapohoji uhalali wake kusimamia kanuni ,taratibu na sheria za Nchi wakati naye ni mtuhumiwa .

Nilitegemea angeanza na kuondoa tuhuma ya vyeti kwanza ndio aendelee kuzungumzia mambo mengine . "Hatutegemei kupata upendo kwa mtoto ambaye amekulia mtaani maana hatakua na upendo kwani hakupewa upendo huo" vivyo hivyo hatutegemei MTU anayetuhumiwa kuwa amevunja sheria kwamba ataweza kusimamia sheria ipasavyo hata kidogo .

Ni katika muktadha huu ndio tunajikuta tumekua na mijadala ya kujadili watu badala ya kujadiki mambo ya msingi ya kitaifa .Hapa tunapotea maana Nchi yenye watu M50 tunakua na mtuhumiwa Wa kufoji vyeti ndio kiongozi wetu ni aibu Kubwa sio kwamba ni kitu cha kuzungumzia taratibu hapana "ni aibu Kubwa" ni sawa na suala la kukuta wafanyakazi waliofoji vyeti zaidi ya elfu kumi .Hili linaonyesha ni jinsi gani kuna uozo kwenye Taifa ni mambo ya aibu tupu.

Jiulize hawa waliingiaje , Na kama kuna wengine kama DAB tunawaacha tumemaliza tatizo au tunaendeleza tatizo?

Wakati tunajibu maswali magumu kwa majibu mepesi tunasema wanahitaji kujua kusoma na kuanzika tu yaani KK mbili tu ili hali watoto wetu Wa darasa la tatu tunawapima kwa Kkk yaani Kusoma, kuandika na kuhesabu usishangae kwamba hata kuhamasisha watoto wetu wajibidishe kusoma itakua ngumu kwani hii Elimu tunayoitoa hatuithamini badala yake tunaibeza tu.

Bila kutumia Elimu ya secondary utaelewa tu kwamba Nchi inaendeshwa kwa kanunu ,taratibu na sheria tulizojiwekea na wala sio matamko .Hivyo basi kiongozi wetu wanapaswa sio tu kuzifuata hizo zote Bali pia kuzisimamia na kama wao ndio watakua mstari Wa mbele kuzivunja basi tegemea matatizo makubwa kwenye jamii tunamoishi.

Kila muda una mambo yake na hutoa hukumu zake miaka kumi baada ya Uhuru tungehitaji viongozi mwenye KK tu na ilichukuliwa kama maendeleo makubwa ila kwa sasa tunahitaji zaidi ya hapo kwenye Kk hizo mbilia au tuongeze na ile ya tatu .
Bado tungehitaji tuwe na watu wenye upeo zaidi ya kina DAB kwenye taasisi zetu hizo nyeti na ndio maana utaona kuna mambo mengi yasiyoeleweka yanatokea na hata MTU akipewa nafasi ya kuzungumzia na kueleza ni kwa nini amefanya hayo mf.kuvamia Clouds redio hawezi kutoa sababu za kueleweka.

Angalia mikutano yake na mambo anayoongea huko haelewi kwamba yeye ni mmoja Wa hao anaowaongoza yeye anaona yupo pembeni ndio maana kauli za kuwachapa wafanyakazi Wa ardhi kitu ambacho hakipo kisheria yeye amekizungumza .
Ndio maana aliweza kuwaharasi wafanyakazi wake mwenyewe Wa Mkoa wake mbele ya waandishi kwa kuwaita machizi hii yote inaonesha kuna shida sehemu .

Ingekua ni kocha basi wangemsusia ili afukuzwe ,wangeacha tumu ifungwe tena magoli mengi tu na hapo ndipo mmiliki au wamiliki wangeamua kumlinda yeye au masilahi ya timu na kuamua kumtimulia mbali au kubadili kikosi. Katika haki yetu kwa kuwa huwezi kubadili kikosi unaweza kuamua kumuacha kwa muda mrefu huku timu ikiambulia kipigo na aibu . lakini timu ikinunuliwa na mmiliki mwingine basi atamuondoa tu hamna jinsi .

Tunapoongelea suala la utendaji pia tunatakiwa kuangalia tija ya utendaji huo na tija hiyo kwa kiwango gani ?

Isijekuwa ni utendaji ambao bado hauna tija yoyote kwa mustakabali Wa eneo husika . utendaji huo unafuata taratibu ,kanuni na sheria tulizojiwekea?

Unapowauliza wafanyakazi wako walete Vyeti na kuvikagua je wewe unavyo au ukiulizwa unang'ata meno ?

Je unafikiria tukiwa na viongozi ambao wanajua tu kk haitaleta shida kwa Nchi maana viongozi ndio wanaosimamia mambo yote hivyo italeta mwanya kwa watendaji wasio na maadili kufanya udanganyifu kirahisi kama kuendelea kuajiri wasio na vyeti ,ndugu ,ukabila na mengine yalioko nje ya utaratibu .

Wakati Wa mwalimu maadui walitangazwa kuwa ni watatu Ujinga ,maradhi na umasikini sijui Leo ni nani amekuambia kwamba ujinga umeondolewa kwenye kundi la maadui zetu ?
 
Dunia ya leo uongozi siyo kipawa tena ni professional. Na professional inahitaji mtu aliyeelimika. Dunia ya leo elimu ya juu ni muhimu kwenye uongozi. Ndiyo maana anafanya mambo ya ajabu na kupoteza muda kufuatilia mambo yasiyo ya msingi. Yaani kwenye information age unaquestion umuhimu wa wa elimu kwa viongozi? KKwani hatuwezi pata kiongozi mwenye vyeti na mchapa kazi!
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali. Kufuatia mahojiano ya jana ya Daudi Albert Bashite, kwenye Star TV, imethibitishwa pasi shaka kuwa ni kweli Daudi Bashite hana vyeti vya elimu zaidi ya cheti cha darasa la saba tuu ndicho chenye jina lake la Daudi Albert Bashite alilopewa na wazazi wake pale alipozaliwa Kolomije na kusoma Shule ya Msingi ya Kolomije.

Mahojiano hayo yamezua mjadala mkali huku kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakisema ametia aibu.

Hili ni bandiko la swali, Jee sisi Watanzania tunataka Viongozi wa aina gani? . Wajinga wenye zero,na wasio na vyeti lakini ni wachapa kazi na wana deliver, au wasomi wenye macheti hadi ma Ph.D lakini ni Mangi Meza, hukaa ofisini tuu na makabrasha lundo, lakini kwenye delivery ni zero?.

kuna hoja nimesoma mahali kuwa eti Bashite ametia aibu kukwepa kuzungumzia elimu yake, vyeti vyake, kufoji vyeti na kulikana jina lake la Daudi Albert Bashite.

Jee ni kweli Bashite ametia aibu?. Jee ameaibisha mamlaka yake ya uteuzi?, kipi muhimu kwa Bashite ni macheti au uchapakazi wake? .

Jibu ni no. Bashite hajajiaibisha wala hajaiaibisha mamlaka yake ya uteuzi, kwa sababu amejieleza vizuri kabisa kwa kiwango cha elimu yake ya darasa la saba.

Huyu mtu elimu yake ni darasa la saba, hivyo ameongea kama darasa la saba na kiukweli amejieleza vizuri. Mimi nimeridhika. Amefunika na ndie shujaa wa kipindi hicho. Thamani ya Bashite ni uchapakazi wake na sio macheti!.

Ili mteuliwa amuaibishe mteule, only if kauli, maneno na matendo ya mteuliwa, yatamuaibisha mteule na ndipo mteule huchukua hatua kuondoa aibu hiyo kama alivyofanya kwa Mhe. Kitwanga.

Lakini mteuliwa hata akifanya vitendo vya ajabu kiasi gani, au vya aibu kiasi gani, kama mteule hajaona aibu kwa vitendo hivyo, then, mteuliwa huyo anakuwa hajajiaibisha wala hajamuaibisha mteule wake kwa sababu ili mtu kujisikia umeaibika, hatua ya kwanza ni lazima kwanza hiyo aibu iwepo ndipo mtu ujisikie aibu. Lakini ikitokea hiyo aibu haipo, mtu hawezi kujisikia aibu.

Hivyo Daudi Bashite hajajiaibisha wala hajamuaibisha yoyote kwa sababu huyo wa kuibishika hata aibu yenyewe hana, ndio maana mpaka leo, mpaka kesho na mpaka keshokutwa mchapakazi Daudi Bashite anaendelea kuchapa kazi, na wanao aibika ni wanaodhani anaaibisha.

Aibu ni kama kutumia akili au kutumia busara.

Ili mtu kutumia akili, jambo la kwanza ni hiyo akili kwanza iwepo. Ikiisha kuwepo ndipo itaweza kutumika. Inapotokea hata hiyo akili ya kutumika haipo, hawezi kumwambia mtu kuwa hakutumia akili as if akili hiyo ipo na mtu anayo lakini hakuitumia, ikitokea mtu akili hiyo hana kabisa, yaani ni mchapa kazi hodari lakini kichwani ni mtupu kabisa, lakini mamlaka yake ya uteuzi haiuoni huo utupu unaouona wewe, then ujue hicho ndio kiwango cha mamlaka hiyo na imeridhika naye, who are you kuhoji akili za mchapakazi huyo?.

Vivyo hivyo katika matumizi ya busara, ili busara itumike, lazima kwanza hiyo busara iwepo. Kama busara haipo kabisa ndani kichwa cha mtumiaji, ukimtegemea kutumia busara, hiyo busara ya kutumika itoke wapi?.

Natoa wito, tuwaache wachapa kazi wachape kazi, hii ni awamu ya hapa kazi tuu, sio hapa elimu au hapa busara, ni hapa kazi tuu.

Wenye aibu zenu kaeni nazo hizo aibu zenu, wenye akili zenu, kaeni nazo hizo akili zenu na ma vyeti yenu ya elimu zenu, na busara zenu kaeni nazo wenyewe; sisi tunataka kazi tuu na wachapakazi tuu, hata kama hawana vyeti, hawana akili, hawana busara na hawana aibu, thamani yao ni uchapakazi wao tuu.

Namaluzia kwa Hili swali
ili ni bandiko la swali, Jee sisi Watanzania tunataka Viongozi wa aina gani? . Wajinga wenye zero,na wasio na vyeti lakini ni wachapa kazi na wana deliver, au wasomi wenye macheti hadi ma Ph.D lakini ni Mangi Meza, hukaa ofisini tuu na makabrasha lundo, lakini kwenye delivery ni zero?

Jumanne Njema.

Paskali.

Kama elimu si kigezo cha bashite kuteuliwa Bali utendaji wake basi watu wa aina hiyo wako wengi,wako wakulima wengi vijijini wenye weledi mkubwa kuliko bashite nao wafikiriwe ktk teuzi,NA mwelekeo wa serikali hii ya maprofesa Na ma dokta ni kuiangusha nchi kwa sababu u prof Na u dokta wao hauna tija kwa taifa Bali kuendeleza umangi meza,stupid notion
 
Kama hii makala siyo ya kugushi, Paschal umeteleza . Ujue,
1. Kabla ya Uhuru,wakoloni ndo walitumia mfumo wa kuweka viongozi wasio na elimu,bali wanaowatii,wanaojipendekeza kwao ila wanakandamiza waafrika wenzao waliotaka kuleta mageuzi ya uhuru.
2. Baada ya uhuru, Mwl, Nyerere alifuta hayo. Aliimarisha elimu kuanzia msingi hadi chuo kikuu. Lengo, apate wasomi watambuzi ,washike madaraka,waongoze wenzao,maendeleo yapige hatua. Ndiyo maana hadi leo,tunasisitiza na kutenga bajeti kubwa kuendeleza elimu ili kuongeza "utambuzi".
3. Pascal,siamini kama wewe ungekuwa unajua tu "kusoma na kuandika" ungeweza hata kuandika article kama hii.
4. Kama juhudi tu ndo kigezo cha uongozi,basi "juhudi "na maarifa" ni kigezo bora zaidi cha uongozi.
 
Kama elimu si kigezo cha bashite kuteuliwa Bali utendaji wake basi watu wa aina hiyo wako wengi,wako wakulima wengi vijijini wenye weledi mkubwa kuliko bashite nao wafikiriwe ktk teuzi,NA mwelekeo wa serikali hii ya maprofesa Na ma dokta ni kuiangusha nchi kwa sababu u prof Na u dokta wao hauna tija kwa taifa Bali kuendeleza umangi meza,stupid notion
Majanga yapo kwenye (Elimu, Sheria, Habari, Hazina, Ujenzi na Bungeni)
 
Uongozi ni hekima, unawezakuwa umesoma ukikosa hekima hustshili kuwa Kiongozi. Kumbuka kutokuwa na hekima utakuwa Kiongozi matukio kwani kiongozi lazima afanye jambo kwa kutafakari kabla ya kutenda au kutoa maamuzi yoyote yale
 
Kama huwa namwelewa Pascal anachoandika kuhusu DAB ni kejeli na dhihaka. Ukijikumbusha fasihi hii huwezi mshambulia Mayalla labda kama utaendeleza mjadala kwa kejeli pia. Swali alilouliza na mifano aliyotoa ni ushahidi tosha wa sifa za makundi mawili ya viongozi wengi tulionao.
Paskali pole.
Instant justice ya DAB ni hulka yake. Hata kama angekuwa na vyeti halisi, nina mashaka kama angebadilika.
Watu wenye hulka kama yake huwa hawasaidiwi na elimu ya vitabuni. Hulka hii katika aiba yao ni matokeo ya malezi na uzoefu wa ubabe unaotokana na maisha alimopotia na kukulia.

DAB amefanya kazi ya ukondakta, house boy, errand boy na mbabe wa kijiwe. Amewahi kukodiwa kutukana, kudhalilisha na hata kupiga. Ukiona haya, uwe na uhakika kuwa hulka ya kupenda kuonekana na ubabe wa kifisadi, haviwezi kubadilishwa na elimu ya vitabuni.

Ikumbukwe licha ya kununua cheti chenye jina la mtu mwingine, DAB alipita darasani kule Moshi na kuhitimu. Lakini ukiona ujenzi wa hoja zake na kiwango cha kutojitambua nafasi yake, unagundua kuwa elimu ya vitabuni haina nafasi katika usugu wa tabia aliyo nayo.

Mahojiano yake na Star TV yameonyesha wazi na kwa kweli kawaaibisha waliopanga naye mkakati wa damage control. Mathalani:
- suala la vyeti limemshinda kulieleza
- suala la kuvamia studio ameishiwa kubwabwaja maneno
- Ameshindwa kuficha chuki yake dhidi ya Nape na Gwajima
- Ameshindwa kujieleza juu ya mwanamke wa shilawadu
- Ameshindwa kueleza ni kwa nini alienda na silaha studio usiku
- Ameshindwa kujieleza kwa nini aligoma kuhojiwa na tume
- Ameendelea kujilinganisha na mawaziri
- Ameshindwa kuficha siri binafsi na za marafiki zake katika masuala ya fedha za michango
- Ametumia majigambo mengi alivyo karibu na Mungu
- kila anayepingana naye anapewa sifa ya kuuza unga
- DSM ni mkoa na mali yake, na wakazi wa Dar ni kama watoto wake!
- Vicarious liability anaitumia vibaya kuhalalisha madhambi yake
- ukitofautiana naye ni sawa na kutofautiana na Mungu
- kwake matokeo ya kazi ni bora kuliko njia za kufikia matokeo hayo

Kimsingi, DAB ni kituko na Paskali unafanya mzaha kumlinganisha na viongozi wasomi.
Yaani kututaka kuchagua kati ya kiongozi asiye na elimu lakini mchapa kazi na mwenye elimu lakini mangi meza. This is an invalid comparison. Si kila Mbashite ni mchapa kazi na si kila msomi ni mangimeza.
DAB hayuko katika makundi hayo mawili.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali. Kufuatia mahojiano ya jana, kwenye Star TV, imethibitishwa pasi shaka kuwa ni kweli muhojiwa hana vyeti vya elimu zaidi ya cheti cha darasa la saba tuu ndicho chenye jina lake alilopewa na wazazi wake pale alipozaliwa kijijini Kolomije na kuandikishwa Shule ya Msingi ya Kolomije.

Mahojiano hayo yamezua mjadala mkali huku kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakisema ametia aibu.

Hili ni bandiko la swali, Jee sisi Watanzania tunataka Viongozi wa aina gani? . Wajinga wenye zero,na wasio na vyeti lakini ni wachapa kazi na wana deliver, au wasomi wenye macheti hadi ma Ph.D lakini ni Mangi Meza, hukaa ofisini tuu na makabrasha lundo, lakini kwenye delivery ni zero?.

kuna hoja nimesoma mahali kuwa eti muhojiwa ametia aibu kukwepa kuzungumzia elimu yake, vyeti vyake, kufoji vyeti na kulikana jina lake halisi, na badala yake kukumbatia jina la wizi.

Jee ni kweli muhojiwa ametia aibu?. Jee ameaibisha mamlaka yake ya uteuzi?, kipi muhimu kwa muhojiwa kati ya macheti au uchapakazi wake unaodeliver? .

Jibu ni a big No. Muhojiwa hajajiaibisha wala hajaiaibisha mamlaka yake ya uteuzi, kwa sababu amejieleza vizuri kabisa kwa kiwango cha elimu yake ya darasa la saba.

Huyu mtu elimu yake ni darasa la saba, hivyo ameongea kama darasa la saba na kiukweli amejieleza vizuri. Mimi nimeridhika. Amefunika na ndie shujaa wa kipindi hicho. Thamani yake ni uchapakazi wake na sio macheti!.

Ili mteuliwa amuaibishe mteule, only if kauli, maneno na matendo ya mteuliwa, yatamuaibisha mteule na ndipo mteule huchukua hatua kuondoa aibu hiyo kama alivyofanya kwa Mhe. Kitwanga.

Lakini mteuliwa hata akifanya vitendo vya ajabu kiasi gani, au vya aibu kiasi gani, kama mteule hajaona aibu kwa vitendo hivyo, then, mteuliwa huyo anakuwa hajajiaibisha wala hajamuaibisha mteule wake kwa sababu ili mtu kujisikia umeaibika, hatua ya kwanza ni lazima kwanza hiyo aibu iwepo ndipo mtu ujisikie aibu. Lakini ikitokea hiyo aibu haipo, mtu hawezi kujisikia aibu.

Hivyo mhojiwa, hajajiaibisha wala hajamuaibisha yoyote kwa sababu huyo wa kuibishika hata aibu yenyewe hana, ndio maana mpaka leo, mpaka kesho na mpaka keshokutwa mchapakazi huyu anaendelea kuchapa kazi, na wanao aibika ni wanaodhani anaaibisha.

Aibu ni kama kutumia akili au kutumia busara.

Ili mtu kutumia akili, jambo la kwanza ni hiyo akili kwanza iwepo. Ikiisha kuwepo ndipo itaweza kutumika. Inapotokea hata hiyo akili ya kutumika haipo, hawezi kumwambia mtu kuwa hakutumia akili as if akili hiyo ipo na mtu anayo lakini hakuitumia, ikitokea mtu akili hiyo hana kabisa, yaani ni mchapa kazi hodari lakini kichwani ni mtupu kabisa, lakini mamlaka yake ya uteuzi haiuoni huo utupu unaouona wewe, then ujue hicho ndio kiwango cha mamlaka hiyo na imeridhika naye, who are you kuhoji akili za mchapakazi huyo?.

Vivyo hivyo katika matumizi ya busara, ili busara itumike, lazima kwanza hiyo busara iwepo. Kama busara haipo kabisa ndani kichwa cha mtumiaji, ukimtegemea kutumia busara, hiyo busara ya kutumika itoke wapi?.

Natoa wito, tuwaache wachapa kazi wachape kazi, hii ni awamu ya hapa kazi tuu, sio hapa elimu au hapa busara, ni hapa kazi tuu.

Wenye aibu zenu kaeni nazo hizo aibu zenu, wenye akili zenu, kaeni nazo hizo akili zenu na ma vyeti yenu ya elimu zenu, na busara zenu kaeni nazo wenyewe; sisi tunataka kazi tuu na wachapakazi tuu, hata kama hawana vyeti, hawana akili, hawana busara na hawana aibu, thamani yao ni uchapakazi wao tuu.

Namaluzia kwa Hili swali
ili ni bandiko la swali, Jee sisi Watanzania tunataka Viongozi wa aina gani? . Wajinga wenye zero,na wasio na vyeti lakini ni wachapa kazi na wana deliver, au wasomi wenye macheti hadi ma Ph.D lakini ni Mangi Meza, hukaa ofisini tuu na makabrasha lundo, lakini kwenye delivery ni zero?

Jumanne Njema.

Paskali.
Kuna hatar ya mtu kutekwa
 
Una roho ngumu sana!!! Tuseme Yeeeees, ana delivery kuliko kawaida, well, vipi mahakama imeshatuhakikishia kua huyu mtu hana hatia yeyote ya kufoji vyeti na kujipatia mshahara kwa jina hewa?? Unajisikiaje kuongozwa na kiongozi mhalifu?
 
Hatuhitaji wajinga wachapakazi wala mangi meza wenye vyeti bali tunahitaji viongozi wachapa kazi wenye sifa stahiki na sizizo na shaka!!!!

Hatuwezi kuwa na viongozi wajinga, vilaza, wasio na uwezo wa kuchambua mambo, waliofika hapo walipo ujanja ujanja lakini tukaamua kuwafumbia macho eti kwavile tu ni wachapa kazi!!!

Aidha, hatuwezi kuwa na viongozi wazembe, wavivu, wasiowajibika lakini tunaamua kuwafumbia macho eti kwavile tu tangu aanze darasa la kwanza hadi PhD hajawahi kupata maksi nyingine zaidi ya A.

Tunahitaji viongozi ambao ukiwafanya kuwa pivot, system inakuwa kwenye equilibrium... weledi kwenye utendaji unakuwepo hali kadhalika uwajibikaji unakuwepo!

Kinyume chake, ndo yale unaenda kwenye Live TV Coverage na kupiga mayowe dunia mzima kwamba wewe chige unauza dawa za kulevya kwahiyo kesho kutwa uje kuripoti Central Police!! Hiyo kesho kutwa nikienda, nahojiwa kama kweli nauza dawa za kulevya!! Hapo mtu anatarajia nitasema "ndiyo, nauza mihadarati!"

Baada ya hapo napakizwa kwenye ndinga ya polisi eti kwenda kunipekua!! Hapo napo wanatarajia watakuta ushahidi wakati walishanipa tahadhali mapema!!!
 
Back
Top Bottom